PreGE2025 Mtendaji Mkuu wa TANROADS afanya ukaguzi kwenye Mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Shinyanga na kuagiza Mkandarasi kukamilisha mradi kwa wakati

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Tarehe 16 Juni 2025, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mha. Mohamed Besta amefanya Ukaguzi kwenye Mradi wa Ujenzi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Shinyanga na kuagiza Mkandarasi anaetekeleza Ujenzi wa Uwanja huo (CHICO) kuhakikisha anakamilisha kazi za kufunga taa za kuongozea Ndege pamoja na Kumalizia Jengo la Abiria kwa Wakati.

Aidha, Mtendaji Mkuu amebainisha kuwa, kwa sasa Maendelea ya Mradi kwa Ujumla yemefikia aslilimia 82 huku sehemu ya kutua na Kurukia ndege vikiwa vimekamilika kwa asilimia 100 na Ujenzi wa Jengo la Abiria umefikia asilimia 72.

Amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Mkandarasi CHICO chini ya usimamizi wa Mhandisi Mshauri (SMEC International) pamoja na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) na kusisitiza kuwa Mkandarasi aendelee kusimamiwa vyema ili kazi zilizosalia zikamilike kwa Wakati.

Kazi zinazoendelea kwa sasa ni uwekaji wa miundombinu ya Taa za Kuongozea Ndege (AGL system) na umaliziaji wa Jengo la Abiria (Terminal Building). Uwanja huu utakapokamilika utakuwa na Uwezo wa kuhudumia abiria 120,000 kwa mwaka na unatajaria kukamilika ifikapo Septemba 10, 2025.

Mhandisi Besta ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Dr Samia Suluhu Hassan, Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuhakikisha inaboesha Sekta ya Usafiri wa Anga ili kuchochea ukuaji wa Uchumi kwa Taifa.


Your browser is not able to display this video.
 
Kumbe mtendaji makuu WA Tanroads NI Baba levo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…