Mtei ampongeza rais Magufuli kwa kutekeleza ilani ya CHADEMA

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,819
49,016
Muasisi wa Chadema ndugu Edwin Mtei ameupongeza utendaji wa rais John Pombe Magufuli kwa vile anatekeleza kabisa ilani ya Chadema waliyoinadi wakati wa kampeni.

Utumbuaji wa majipu yaliyojaa serikalini, kwenye halmashauri na kwenye mashirika ya umma ni moja ya kero zilizokuwa zinapigiwa kelele na Chadema kwa muda mrefu si bungeni si majukwaani.

Kila siku tumekuwa tunasema kuna wafanyakazi hewa, kuna wizi bandarini, Shirika la ndege limeoza, kuna ufisadi mkubwa kwenye madini, ufisadi kwenye halmashauri zetu, hizi zote ni ajenda za Chadema, kwa hiyo rais anapofanyia kazi hayo kwa niaba ya Chadema na wananchi kwa ujumla hatuna budi kumpongeza.

Nini maoni yako.
 
Muasisi wa Chadema ndugu Edwin Mtei ameupongeza utendaji wa rais John Pombe Magufuli kwa vile anatekeleza kabisa na ilani ya Chadema waliyoinadi wakati wa kampeni.

Utumbuaji wa majipu yaliyojaa serikalini, kwenye halmashauri na kwenye mashirika ya umma ni moja ya kero zilizokuwa zinapigiwa kelele na Chadema kwa muda mrefu si bungeni si majukwaani.

Kila siku tumekuwa tunasema kuna wafanyakazi hewa, kuna wizi bandalini, Shirika la ndege limeoza, kuna ufisadi mkubwa kwenye madini, ufisadi kwenye halmashauri zetu, hizi zote ni ajenda za Chadema, kwa hiyo rais anapofanyia kazi hayo kwa niaba ya Chadema na wananchi kwa ujumla hatuna budi kumpongeza.

Nini maoni yako.
Mkubwa dawa
 
Mwasisi amesema kitu cha maana tunatakiwa tuunge mkono mazuri ambayo mueshimiwa Magufuli.nimemsikia hata mueshimiwa Lema akikubaliana na kuiunga mkono serekali yenye nia ya kujenga tz ya viwanda.watanzania tuzidi kumuunga mkono Ndugu yetu katika vipaumbele vyake
 
Source please....
Ndio maana Chadema sasa hiv hawana ajenda kumbe mtunga ajenda na mwenye chama amewaambia hizi anazozifanya Magufuli ndizo zilikuwa ajenda zetu, now wamebakia kudandia matukio ya msimu tu.
Baadae asije kukanusha kuwa ni uzushi.
 
Rais Magufuli ana mapungufu yake kama binadamu lakini kikubwa zaidi ninachokipenda kutoka kwake ni kuwa na msimamo usioyumba. Siasa za Tanzania kwa sasa zinahitaji Rais wa nchi asiyeyumba katika maamuzi.

The guy is firm and fair.

Tulihitaji sana kama taifa kwa kipindi hiki kupata Rais wa aina ya Rais Magufuli.

Rais Magufuli is the man!
 
Kama wanatumbuana na kusomeshana wenyewe kwa wenyewe sisi haituhusu kazi yetu ni kuongeza kuni.
 
Rais Magufuli ana mapungufu yake kama binadamu lakini kikubwa zaidi ninachokipenda kutoka kwake ni kuwa na msimamo usioyumba. Siasa za Tanzania kwa sasa zinahitaji Rais wa nchi asiyeyumba katika maamuzi.

The guy is firm and fair.

Tulihitaji sana kama taifa kwa kipindi hiki kupata Rais wa aina ya Rais Magufuli.

Rais Magufuli is the man!
He is not fair, alimuonea sana aliyekuwa mkurugenzi wa jiji Wilson Kabwe na mama Malecela alivyowatumbua was not fair at all ukilinganisha na anaowakumbatia leo.
 
Soma vizuri habari yote ktk gazeti lenye habari hiyo utapata kujua kijembe ambacho mzee Mtei amemrushia jpm. Hajamsifia kama unavyodhani. Lumumba ni janga la taifa
 
Back
Top Bottom