WilsonKaisary
JF-Expert Member
- Apr 4, 2017
- 392
- 947
.................
Siku zote mimi huwa nachagua mtu sio chama.
Ni kweli kabisa sasa hivi hali ya kimaisha imekuwa nzito.
Wanasiasa wamepamba moto kukosoana ili mradi kuijenga nchi.
Lakini pia katika haya tuwe makini tusijikute tunatetea uovu badala ya wema.
Ni kweli hakuna asiyekuwa na mapungufu:
Hata Nyerere alikuwa nayo;
Hata Rais wangu wa sasa anayo.
…………..
Lakini, hivi inawezekana kupata kiongozi anayemridhisha kila mtu?
Mimi naamini uzuri wa mtu hautokani na kwamba YEYE NI MKAMILIFU (100%)
bali unatokana na kwamba nia yake ni njema; licha ya mapungufu yake.
Na nia njema ya mtu inatambulikana tu; kama ilivyo nia mbaya ya mtu.
……………
Ni nani asiyejua kuwa nchi hii imeporwa na mafisadi sana?
Nani asiyejua kuwa nchi hii imeliwa na wageni sana?
Nani asiyejua kuwa tulifika mahali watu wako tayari kuuza nchi na watu wake kwa faida yao na familia zao?
Je, neno “UTANDAWIZI” japo ni la kimzaha, halikutokana na iliyokuwa hali halisi?
…………….
Hivi ni kweli tunaweza kusema kwa ujasiri kuwa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli anafanana na mafisadi wa enzi zile?
Au tunamlaumu tu kwa sababu ya uchungu wa kukosa kile tulichokuwa tukikipata?
Hivi ni kweli hatuoni tofauti kati ya sasa na zamani kwa habari ya maendeleo?
…………….
Ni kweli yeye kama binadamu hatakosa mapungufu.
Lakini kwa anayeangalia nchi kwa mbele; hauoni nuru kule mbele?
Hivi kuna mazuri yanayokuja bila gharama?
…………….
Mimi naamini Rais Magufuli anafanya kazi nzuri sana.
Ni kweli naumia kama mtu binafsi kwa sababu za kiuchumi;
Lakini huu si ni wakati wa kuweka msingi?
Unapoweka msingi wa nyumba, kuna uwezekano kabisa wa kulala nje.
Lakini unalala nje kwa sababu unajua kesho, utakuwa chini ya dari yako.
……………
Kwa miaka mingi tulilia na ufisadi;
Mungu ametujibu kwa kutupa Magufuli;
Lakini nahisi hatujatambua.
Naiona Tanzania tofauti kule mbele kwa sababu ya yanayotendeka sasa.
……………
Cha msingi, pamoja na juhudi na nia yake njema kwa nchi yetu;
Namwomba Rais wetu aweke sheria bora; Katiba bora; maana asipofanya
hivyo; siku akiondoka tu; wapo mafisi waliokaa tayari tayari;
Watarukia kwa nguvu zote na kulamba kila kitu ambacho atakuwa
amekitolea jasho namna hii.
…………….
Sijapata sababu ya kutompenda Rais Magufuli maana hatukosi mapungufu na serikali takatifu ni MBINGUNI TU
japo mimi sina chama kwa sasa,ananishawishi niende C.C.M
lakini huwa nachagua watu; sio vyama.
Mungu Ibariki Tanzania.
Mungu mbariki Rais wangu Magufuli;
kwa Jina La Yesu.