True legacy
Member
- Dec 16, 2016
- 76
- 43
Na: Baraka Elias
Kati ya mapendekezo 21 ya kamati ya madini ya iliyoundwa na Mh Rais, Leo nimevutiwa kuyatazama zaid mapendekezo mawili tu, Pendekezo namba 15 na 19.
*Pendekezo na 15 : " Sheria itamke mikataba isiwe ya siri."
*Pendekezo na19. "Serikali ipitie na kufanya marekebisho au ifute kabisa sheria ya madini ili kuondoa masharti yasiyo na tija."
HAYA YAMENIRUDISHA NYUMA KWENYE RASIMU YA KATIBA YA WANANCHI, YA JAJI WARIOBA .
Rasimu ya Jaji Warioba ilipendekeza, mikataba yote ya rasilimali za nchi ikiwemo madini isiwe siri, na ijadiliwe Bungeni kwanza, ibara ya 107(2) g&h, Na zaidi Ibara ya 124 (1) iliweka ZUIO kwa viongozi, ilisema kuwa Mbunge anaweza akavuliwa Ubunge iwapo atakuwa na maslahi yoyote na mikataba.
LAKINI KWENYE KATIBA PENDEKEZWA YA CCM,
Kwenye ibara ya 131 (3) g&h..WALIONDOA KABISA kipengele hicho cha ibara 107 (2) h.
Na hata Ibara 124 WALINGOA MAZUIO YOTE MAKALI KWAO .
Hii ni ili wawe wanafanya mikataba ya rasilimali zetu kwenye mahotelini ya ulaya kwa siri siri, bila kubanwa na sheria.
Na walishangilia sana na kugeuza Bunge ukumbi wa disco kwa kufanikiwa kungoa vipengele hivi vinavyowabana
MAANA YA MAPENDEKEZO YA MAKANIKIA KISHERIA;
Hii ina maana sheria ya madini ifutwe mchakato urudi Bungeni upya!!. Yale yale WALIYOYANGOA kwenye Rasimu ya Jaji Warioba, inabidi WAYARUDISHA TU japo kwa style nyingine.
Ajabu nyingine kwamba, Wale waleee..wapiga kelele vijana wa Lumumba waliyokuwa wakishangilia kuondolewa haya, Walikuwa wakizomea UKAWA kutoka nje ya Bunge la katiba, leo hao hao wanalia tulikuwa tunaibiwam hao wanashangilia kufutwa kwa waliyokuwa wakishangilia awali !!Wakati mwingine inabidi uwe "chizi" kuelewa akili za vijana wa Lumumba kama Magoiga SN.
Hatua alizochukua JPM ni moja ya hatua nzuri kwa maslahi ya rasilimali zetu kama Taifa, lakini BADO TUNA TATIZO KUBWA LA KIMFUMO.
SAMAKI WENGI WAMESHAOZA SANA NDANI TENGA.
#Mtazamo_Wangu