Mtazamo wa Rais Magufuli katika uchumi ni wa kipekee lakini kwenye uteuzi bado anaiga

dostum

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
215
110
Katika mambo mageni na ya kipekee kwa mh JPM ambayo watangukizi wake walishindwa ni pamoja na Sera ya kuimarisha uchumi kwa kuwapunguzia kodi viwanda nchini na wale watakaoagiza toka nje ya nchi kulipa kodi nyingi.

Na mingoni mwa mambo ambayo anayoendelea nayo yaani ameyarithi ni muendelezo wa kuona kuwa baadhi ya jamii nchi hazina Uzalendo kwa nchi, Elimu, Uchapakazi, Weledi.

Kimsingi mtazamo huo umepitwa na wakati.

Kuna wakati mh Mramba alipata kutamka kuwa eti wachaga Wapo Wengi TRA kwakuwa amesomea sana masuala ya kodi na jamii iliamini.
Kwenye utawala Huu kwasasa TRA inaonekana ni ya kitaifa zaidi.

Tunaamini hata hili mh JPM atalifanyia kazi kwa kuwa yy mwenyewe ana mapambio yake kuwa hatobagua jamii yyt.

Mh JPM bado tunamuunga mkono na tunamuombea dua na tunahitaji asizibe pamba masikioni bali atuonyeshe kwa vitendo Umoja na mshikamano huo kwa kuonyesha kuna utaifa ktk teuzi anazozifanya.

What di u think
 
Back
Top Bottom