Mtazamo wa Makinda kuhusu bunge hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtazamo wa Makinda kuhusu bunge hili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by banyimwa, Mar 5, 2011.

 1. b

  banyimwa Senior Member

  #1
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Makinda: Bunge halikuwa na agenda nyingine


  na Bakari Kimwanga


  [​IMG]
  SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, amefafanua juu ya hisia zilizojengeka miongoni mwa makundi ya jamii kuwa kikao cha Bunge kilichopita kilikuwa na agenda maalumu.
  Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Makinda ambaye yuko Njombe kaskazini, mkoani Iringa kwenye jimbo lake alisema: “Watu wengi walikuwa na hisia kuwa kikao cha Bunge kilikuwa na agenda maalum…lakini mimi nawaambia kuwa lilikuwa Bunge la kazi hasa katika uundaji wa kamati za kudumu na wajumbe wa bodi sasa kazi tumemaliza Bunge liko katika sura iliyokamilika.”
  Akizungumzia migogoro iliyojitokeza katika kikao cha Bunge hilo ikiwa ni pamoja na hatua ya wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kususia kikao na kutoka nje kwa hisia ya kuwapo kwa njama za kuwachakachua kupitia kanuni za Bunge, Makinda alisema hali iliyojitokeza kwa baadhi ya wabunge kutoka nje katika kikao cha Bunge kilichopita ni haki yao kwa mujibu wa kanuni hasa wanapokuwa bungeni.
  Spika Makinda alisema kuwa kuibuka kwa tofauti hizo hakumaanishi kuwa Bunge hilo linapingana kwa kuwa wabunge hao wakitoka nje ni wamoja ila wanashindana kwa hoja.
  Kauli hiyo aliitoa jana katika mahojiano maalum na Tanzania Daima kwa njia ya simu na kusema kuwa hivi sasa Bunge la Kumi limekuwa na changamoto kwa wabunge wengi wao kuwa na uwezo wa kujenga hoja na kuzitetea.
  “Bunge ni moja na hakuna mgawanyiko ila mbunge kuonyesha hisia zake ni haki yake na anakuwa hajavunja kanuni zinazoendesha Bunge; jamani hii ni nchi yetu na ni lazima tutambue Bunge huendeshwa kwa kanuni,” alisema Spika Makinda.
  Alisema kuna haja kwa wabunge kujifunza uvumilivu hasa wanapokuwa wanawasilisha hoja zao mbele ya Bunge na kupingwa kwa hoja na wabunge wengine.
  Alisema Bunge ni moja na hakuna Bunge la pili katika kuwasilisha mawazo au hoja zinazohusu sheria za nchi na kutoa rai kwa wabunge kutumia uhuru huo kwa kutoa mijadala huru wawapo bungeni kwa kuzingatia kanuni zinazoongoza Bunge la Tanzania.
  Alisema Bunge la kumi katika katika kikao chake kilichopita lilikuwa la kazi hasa katika uundaji wa kamati za kudumu za Bunge na kuchangua wajumbe wa bodi mbalimbali za mashirika ya umma yaliyopo kwa mujibu wa sheria.
  Makinda, alisema kuwa tofauti na migongano ya mawazo inayojitokeza bungeni ni hali ya kawaida na mara nyingine hutokea kwenye mabunge yote duniani. Spika Makinda alitoa wito kwa wabunge kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwao katika kutatua matizo mbalimbali yanayolikabili taifa na watu wake hasa katika kipindi hiki cha mgawo wa umeme.
   
 2. k

  kukubata Member

  #2
  Mar 5, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyo kicheche wa ccm najifanya anabana sana ataachia mwanya ndio atajua nini chadema wanafanya
   
 3. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mbona hilo liko wazi kwamba ajenda maalum ya kikao kilichopita ilikuwa ni ya kuwakabidhi mafisadi utawala wa bunge kwa kuwapa washikilie kamati zote muhimu za bunge na kuwasukumia mbali wale wote ambao ni mwiba kwao. Hilo spika huyu amelifanikisha vizuri na watu wake wamempongeza sana kwa "kazi nzuri" aliyoifanya. Kwa kujua kwamba umma umeshamshtukia, ndiyo maana anaweweseka na sasa kujitolea majibu ambayo watu hawayahitaji. Kwanza tulishaanza kusahau, yeye tu ameamua kutukubushia machungu.
   
Loading...