Mtazamo: Mungu na Shetani ni vitu vya kusadikika

Mimi kabla sijakubaliana na wewe au kuukataa msimamo wako ningependa unisaidie kujibu maswali haya 2.
1. Kwani shetani ndio kitu gani na Mungu je nacho ndio kitu gani?
2. Hivi hapa duniani kuna kitu kina JINA halafu chenyewe hakipo?

Ukinijibia hayo maswali yangu vizuri then nitaungana na wewe kwenye msimamo wako but laa ukishindwa then nitajua kumbe hata wewe unaongea usio yaamini.
 
Napenda kuwakumbusha watu kua Mungu hayupo na shetani hayupo...kwahiyo watafakari upya dhana ya dini na imani
hakuna kitu kigumu kama kuamini kuwa hakuna Mungu. ila sasa ni vigumu kuamini kama kunakitu ama nguvu ya kuyaweza yote
 
Napenda kuwakumbusha watu kua Mungu hayupo na shetani hayupo...kwahiyo watafakari upya dhana ya dini na imani
Unaposema hakuna Mungu wala shetani unamaanisha nini?Unatumia vigezo gani kusema Mungu na Shetani ni vitu ambavyo havipo?

Naomba nikusaidie kidogo kukuza ufahamu wako.
Katika ulimwengu wa leo kila kitu kinachoonekana hutokana na kitu ambacho hakionekani.Mfano mzuri ni kupanda mbegu na baadaye mbegu kuwa mti, swali la msingi ambalo unapaswa kujiuliza ni kuwa,je ule mti ulikuwa ndani ya mbegu au?
Jibu litakuwa ni hapana kwa maana ya kuwa mti haukuwa ndani ya mbegu ila wazo la mti lilikuwa tayari lipo ndani ya mbegu na baada ya kupanda mbegu ndipo lile wazo likapata kujitokeza kuwa kitu kionekanacho.
Mfano mwingine ni kumkata miguu mwanadamu na kuiweka sehemu.Miguu hiyo ikiwekwa sehemu pekeyake haiwezi kutembea kamwe,bali ukiiludisha kwenye mwili wa mwanadamu,basi mwanadamu ataanza kutembea.Hii humaanisha kuwa miguu sio kitu kinachosababisha mwanadamu kutembea bali kuwa wazo la kutembea ndani ya mwanadamu na miguu kazi yake ni kutekeleza wazo hilo.
Nije kwenye mada husika sasa,kutokana na mifano ya hapo juu unaweza kuona kuwa mawazo ndo kitu ambacho huongoza maisha ya mwanadamu,lakini mawazo hayaonekani au kusikika au hata kushikika ila hutumia viungo vya mwili ili kuweza kuonekana,kushikika au kusikika.
Unapozungumzia mwanadamu basi unazungumzia mambo matatu ambayo ni Roho( utashi,hekima,busara,akili),Nasfi na Mwili.
Kazi ya roho ni kutofautisha mambo ya nasfi na mambo ya kimwili.Kazi ya mwili ni kutoa taarifa za nje ya mwili na kuziingiza ndani ya mwili na kazi ya nafsi ni kumuunganisha mwanadamu na mambo yasiyo onekana kwa kutumia mwili ( milango ya fahamu).
Sasa unapozungumzia Mungu au shetani unazungumzia vitu visivyoonekana au kutambulika na milango ya fahamu.Sasa kwakuwa havitambuliki na milango ya fahamu haimaanishi kuwa havipo ila inakupasa wewe kutafuta milango mipya ya fahamu ya kiroho ambayo itaweza kukutambulisha kwenye uwepo wa Mungu na shetani.
Tatizo nionalo kwako ni kutaka kumpora sifa Mungu kwa kutaka atambulike na milango yako ya fahamu ya kimwili,jambo ambalo haliwezekani.
Kama unashindwa kugeuza mboni ya jicho lako na kuona vitu vilivyo ndani ya mwili wako ndo unataka umwone Mungu kwa jicho hilo hilo,Kama unashindwa kusikia sauti ya damu ikiwa inapita kwenye mishipa ya damu ndo unataka kutumia sikio hilo hilo kusikia uwepo wa mungu?
Katika maana nyepesi ni kwamba kutokuwa na uwezo kwa wewe kusikia damu ikipita kwenye mishipa yake au maji yakipita kwenye mishipa yake haimaanishi kuwa damu au maji havisafiri ndani ya mwili wako bali humaanisha kuwa mlango wa fahamu ambayo huweza kutambua jambo hilo wewe bado hujaanza kuutumia.
Nadhani shida kubwa kwako ni jinsi unavyomtafsiri Mungu na Shetani.Kama ukiwa na maana sahii ya Mungu na Shetani basi lazima ujue kuwa vyote hivyo vipo.
Naomba kuishia hapo.
 
Mimi kabla sijakubaliana na wewe au kuukataa msimamo wako ningependa unisaidie kujibu maswali haya 2.
1. Kwani shetani ndio kitu gani na Mungu je nacho ndio kitu gani?
2. Hivi hapa duniani kuna kitu kina JINA halafu chenyewe hakipo?

Ukinijibia hayo maswali yangu vizuri then nitaungana na wewe kwenye msimamo wako but laa ukishindwa then nitajua kumbe hata wewe unaongea usio yaamini.
Pembe tatu duara ina jina lakini yenyewe haipo.....swali la kwanza ni nonsense.
 
Back
Top Bottom