Mtazamo mpya wa Lowassa na Urais wa Tanzania

Juwaine

JF-Expert Member
Oct 1, 2013
624
169
Wanasiasa wanaotoswa katika vyama "kwa madai hawafai" wakihamia upinzani hujipatia umaarufu na baadhi hushinda chaguzi. Na leo nitafafanua zaidi juu ya wanasiasa waliotoswa na wakashinda au kuvitikisa vyama tawala ili kusisitiza hoja yangu "Kwa nini Lowassa anaweza kuwa rais wa Tanzania."

Fungua macho na akili. Kuanzia mwishoni mwa mwaka 2010 Tunisia ilitumbukia kwenye machafuko ya kisiasa yaliyotawala hadi mwaka 2011 wakati wa maandamano ya vurugu yaliyouondoa madarakani uongozi wa Rais Zine El Abidine Ben Ali kutokana na sababu kadhaa. Baada ya vurugu kutulia, walifanyia marekebisho katiba na Bunge la Katiba lilimchagua Moncef Marzouki kuwa rais wa mpito.

Hata hivyo, ulipofanyika uchaguzi mkuu Desemba 2014, bado Watunisia walimhitaji na kumchagua, kwa kishindo, Mohamed Béji Caïd Essebsi aliyekuwa waziri mkuu katika serikali ya muda iliyoondolewa madarakani. Caïd Essebsi alikaribishwa kuongoza muungano wa vyama vya siasa chini ya chama chake cha Nidaa Tounes.

Kwa nini vyama vya siasa?

Lengo la chama cha siasa ni kushika dola na lengo la mwanasiasa yeyote duniani ni kushika madaraka ndiyo maana baadhi hupigania urais na wengine ubunge na udiwani. Mwanasiasa akikosa nafasi katika chama kimoja, kwa sababu ya mizengwe, huhamia chama kingine na kushinda japokuwa wengine hushindwa.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa, msomi na mwandishi yeyote anayelaani mwanasiasa kuhamia chama kingine atakuwa anaongozwa na msimamo wa kiitikadi. Hata hivyo, ni kweli kwamba katika kuhama vyama, baadhi ya wanasiasa hufifia na kupotea lakini wengine huibuka kuwa gumzo.

Hadi mwaka 1985 Maalim Seif Sharrif Hamad alikuwa kipenzi ndani ya CCM na mwanasiasa madhubuti. Uamuzi wake wa kuwania urais wa Zanzibar kupambana na Idrid Abdul Wakil uliwachefua CCM. Wakamfitinisha. Januari 1988 alitemwa kwenye Baraza la Mapinduzi na akavuliwa cheo cha Waziri Kiongozi. Mei 1988 akafukuzwa uanachama wa CCM pamoja na wenzake sita kutoka Baraza la Wawakilishi. Mei 1989 alitiwa mbaroni na akafunguliwa kesi kwa madai ya kukutwa na nyaraka za siri za Serikali. Tangu mwaka 1989 hadi 1991 alikuwa kizuizini.

Ilipofika fursa ya kuanzisha vyama vingi "aliasisi" Chama cha Wananchi (CUF). Je, ‘amekufa' kisiasa au ameimarika zaidi?

Kenya ilikuaje?

Mwaka 2008 yalizuka machafuko yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 1000 na wengine kwa maelfu walikosa makazi nchini Kenya. Waliodaiwa kuchochea vurugu za kisiasa ni Uhuru Kenyata aliyekuwa mshirika wa Rais Mwai Kibaki na William Ruto aliyekuwa mshirika wa Raila Odinga.

Kenyatta na Ruto ni miongoni mwa watu waliofikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC). Kesi dhidi ya Kenyatta ni kama ‘imetupwa' baada ya mashahidi wengi kujitoa lakini Ruto pamoja na mwandishi wa habari Joseph arap Sang wana kesi ya kujibu.

Kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2013 Kenyatta na Ruto walielemewa na shutuma za kuhusishwa na machafuko kwamba hawafai lakini Wakenya walipuuza wakawachagua Kenyatta kuwa rais na Ruto kuwa makamu wake kupitia muungano wa Jubilee.

Kuelekea uchaguzi mkuu wa rais nchini Afrika Kusini, iliibuliwa kashfa ya ufisadi katika ukarabati wa makazi ya Rais Jacob Zuma yaliyoko Nkandla. Upinzani ulijenga hoja na katika kampeni ulishawishi wananchi kutoipigia kura ANC ya Zuma kwa sababu ya walichoita "Kashfa ya Nkandla." Wananchi hawakuelewa ‘mahubiri ya ufisadi' dhidi ya Zuma bado walimpigia kura nyingi akarudi madarakani.

Nchini Marekani, tajiri mkubwa aliyewahi kuwa meya mara tatu katika jiji la New York, Marekani, Michael Bloomberg alijiwekea historia kwa kushika wadhifa huo kupitia vyama vitatu tofauti. Kila alipofanyiwa mizengwe alihama chama. Hadi mwaka 2001 Bloomberg alikuwa Democrat, alipofanyiwa mizengwe alihamia chama cha Republican. Mwaka 2007 alijiondoa kwenye chama hicho akawania umeya wa jiji hilo akiwa mgombea huru na akashinda.

Kilichombeba Bloomberg kokote alikokwenda ni mtaji wa wapigakura siyo chama. Hata waliowahi kuwa wanadiplomasia maarufu Condoleezza Rice na Hillary Clinton wamekuwa na historia ya kuhama vyama.

Halafu kuna aliyewahi kuwa seneta wa Connecticut, Joe Lieberman. Kwa miaka mingi amekuwa Democrat. Mwaka 2006 alijitoa akawa huru lakini mwaka 2008 alimfanyia kampeni mgombea urais kupitia Republican, John McCain. Alipoulizwa kwa nini aliamua kuhama vyama alijibu, "Chama cha Democrat hakikuwa tena kile chama nilichojiunga kikiwa na taswira ya Rais John Kennedy."

Mtazamo mpya wa Lowassa

Majibu ya Lieberman ni sawa na ya Lowassa anayesema "Hii si CCM anayoijua" na ndiyo kiini cha kuondoka na kujiunga na Ukawa. Je, atashinda katika mazingira anayofuatwa fuatwa na kashfa ya Richmond? Jibu ni ndiyo.

Kashfa ya Richmond iliibuliwa na wapinzani wake wa kisiasa ndani ya CCM ikasababisha akajiuzulu mwaka 2008. Waliotaka kuitumia kashfa hiyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 walishindwa, mbunge huyo mwenye nguvu katika jimbo lake la Monduli na mkoa wa Arusha kwa ujumla, alishinda kwa kishindo.

Rais Kikwete alisema ilikuwa ajali ya kisiasa na mwaka 2010 alimpigia debe akisema ni mtu safi. Hata Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana alipopita Monduli alimsifu Lowassa hukua akidai Lazaro Nyalandu anazurura.

Si hivyo tu, mwaka 2012 bado alichaguliwa kwa kishindo kuingia NEC na ameendelea kuwa na ushawishi mkubwa nchini. Kama kashfa hiyo haikumzuia kushika vyeo ndani ya CCM, itakuwaje na nguvu nje ya chama hicho tawala?

Lowassa amekuwa maarufu katika kipindi chote cha maisha yake na kazi alizofanya, hakika zinamtangaza. Wakati CCM itakuwa inahangaika kumnadi, kwa wananchi, mgombea wake John Magufuli, upande wa pili Lowassa atakusanya mamilioni ya wanachama wa Ukawa pamoja na wafuasi waliokuwa wanamuunga mkono tangu akiwa CCM.

Mbunge huyo wa Monduli si chaguo langu, nimewahi kuandika hivyo katika magazeti mengine niliyofanyia kazi. Sijageuka jiwe. Ninachoeleza "mimi na wewe" tunaompinga, tufungue macho na akili zetu tujiulize CCM ndiyo yenye Serikali na Serikali ya CCM ndiyo yenye Takukuru, polisi na vyombo vingine vya uchunguzi, imeshindwa nini kumfungulia kesi katika kipindi cha miaka saba ambayo hakuwa madarakani?

Sababu moja kubwa ni kwamba bado Serikali ilikuwa inasimamia msimamo wa Takukuru iliyochunguza sakata hilo na kueleza hakukuwa na rushwa.

Je, Serikali ilifanya uchunguzi mwingine au ilibaki kuamini ripoti ileile ya Takukuru kuwa hakukuwa na rushwa katika zabuni ya Richmond?- Ikiwa hawakumshitaki awali itakuwa kazi kumchukulia hatua leo ili kumzuia asiingie ikulu.
 
Kwahiyo maalim Seif alishawahi kua rais wa zenji?

Hajai kuwa raisi wa zenji na wala Mtoa mada hakusema amekua kama umesoma mada vizuri. Ila aichosisitiza ni kwamba tangu awekewe uzushi hadi akafungwa na kufukuzwa ccm! Umaarufu wake umeshuka au umepanda? Jibu umepanda mara 7 x 70

LOWASA DUMEEE! majike yapo ccm
 
Mleta mada hiyo nchi ya Tanazia siioni hapa kwenye atlas, hebu njoo unielekeza halafu tujadili mada yako
 
Ba-ndugu mabadiliko huja kimchezo mchezo, kwani Moi aliondokaje...... ukitaka kumshinda adui mwenye nguvu jenga propaganda mbomoe, mgawanye vipande, tikisa nguzo zake like EDO, kisha kaa pembeni hutoamini......mbona atapiga magoti mwenyewe.
 
Kwahiyo maalim Seif alishawahi kua rais wa zenji?

Ameongelea kuwa kawa maarufu zaidi kisiasa,
Nyongeza ni kuwa alikuwa anaibiwa kura ndiyo maana mwaka 2010 alikomaa mpaka kukawa na mgawanyo wa madaraka vinginevyo kingenuka 2010.
 
Maelezo na mifano uliyoitoa ya viongozi wagombea urais/umeya, pamoja na wapiga kura wao nchini Tunisia, Kenya na Marekani, hayalingani na utamaduni na mazingira ya viongozi na wapiga kura wa Tanzania. Kihistoria na kiutamaduni, na kwa mazingira yaliyopo katika nchi hizo, kwa muda mrefu wananchi wa nchi hizo wamejenga tabia za kimapambano, uthubutu na kujitoa mhanga kwa ajili ya wengine wengi, hata ikibidi kupoteza maisha yao, kitu ambacho kwa wanasiasa/viongozi na wapiga kura wengi wa Tanzania (wa sasa) HAWANACHO kwasababu ya hofu iliyojengwa kwa muda mrefu, malezi, utamaduni na athari za sera za ujamaa na kujitegemea.
Tumeshaona mara kadhaa, mfano serikali inaweza/imeshafanya jambo lisilotakiwa na wananchi wengi, mfano kama kupandisha bei za huduma muhimu kama umeme, petroli, ukosefu wa huduma nzuri ya maji ya uhakika, tiba, barabara, ahadi zisizotimizwa, kupitishwa kwa miswaada bungeni kiujanjaujanja, kuongezewa marupurupu wabunge ili hali wananchi wengi hawaridhii n,k lakini tumeona mara nyingi, na ni kawaida sana kuona watanzania tukiishia kulalamika tu chini chini, maofisini, vijiweni, majumbani, mitandaoni, nk bila kuchukua hatua madhubuti za kupambana na hali hizo. Hii ni kwasababu nilizozieleza hapo juu kwamba malezi, utamaduni na athari za sera za ujamaa na kujitegemea.

Lowasa kwanini amebaki na tuhuma tu kwa miaka yote hii bila kushitakiwa? Kwasababu;
1) Hizo nilizoziweka hapo juu (Hofu, malezi, utamaduni na athari za sera za ujamaa na kujitegemea) kwamba wenye dhamana ya kumshitaki ni watanzania, na kama walivyo watanzania wengi wanazo sifa hizo
2) Wanasiasa walio wengi (sio wote) si waadilifu ki - viiile, na wajuana udhaifu wao, kwamba nani ali cheza wapi.... hivyo hakuna anayeweza kulianzisha kwa Lowasa, kwa kuwa wenyewe si wasafi, huenda mambo yakawagukia wao wenyewe maana Lowasa anayajua mengi, si alikuwa pamoja nao. Hivyo suala la kushitakiwa kwa Lowasa halipo, na hata akishitakiwa kesi yake haitakuwa na nguvu.
 
unayemfanananisha mtu mwenye tuhuma za ufisadi, unatakiwa uongozwe sara ya toba. njoo haraka.
bwana yesu wa nazareth hafananishwi na chchote. labda YESU (Jesus) wa MANchester City FC
 
Back
Top Bottom