Mtazamo kuhusu video ya lwakatare

Mtazamo kuhusu video ya lwakatare

tubadilike-sasa

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2012
Posts
681
Reaction score
167
MTAZAMO KUHUSU VIDEO YA LWAKATARE
Nikiri kwamba uwepo wa hii video wa kinachodaiwa kuwa CHADEMA kupanga mauaji ya raia umeumiza sana moyo wangu wa utanzania.Yawe ni mambo ya kupangwa au yaliyofanywa na CHADEMA yameniumiza sana kama raia wa Tanzania. Ni afadhali kama kuumizwa huku kungenifanya hata nilie ili hiyo sumu ya maumivu iweze kwisha,ila kulia nashindwa na maumivu haya hayawezi kutulizwa na panado!
Kama mwananchi wa kawaida,nimejaribu kufutilia juu ya hili sakata la Lwakatare lakini naona haya mambo tunayoambiwa na wenye dola hayajumlishiki na hayaleti mantiki. Hii ni kutokana na kwamba ukijaribu kupiga darubini nyuma katika matukio yaliyowahi kufanyika katika mazingira kama haya,shaka kubwa inaonekana kuzunguka kila kona ya jambo hili na kutoa mwanya mkubwa wa ama kufeli mantiki ya kawaida na au mtihani wa litimasi “litmus test fealuire”
Wakati swala hili linaanza,Mwigulu Nchemba alidai kwamba mtu aliyempa hiyo video ni kiingozi wa CHADEMA ambaye amechukizwa na yale ambayo wanafanya viongozi wa CHADEMAna-yaani kupanga kuuwa raia.
Sasa nianze na huyo kiongozi wa CHADEMA. Katika hali ya kawaida kabisa mtu unapoona kuwa jinai imetendeka au inataka kutendeka na ushahidi unao wa kuweza kuzuia jinai isitendeke, je ushahidi huo unaupeleka wapi? Unaupeleka polisi au unampelekea kiongozi wa kisiasa wa cha pinzani(Mwigulu Nchemba) kama alivyofanya huyu kiongozi wa CHADEMA? CCM na CHADEMA wao ni washindani wa kisiasa au kwa kiingereza “antagonists”. Je huyu kiongozi wa CHADEMA aliyepeleka hii video kwa Mwigulu Nchemba badala ya kuipeleka polisi alilenga nini hasa? Kwani Mwigulu Nchemba yeye ni “criminal investigator” wa jeshi la polisi Tanzania?
Je huyo kiongozi wa CHADEMA ana imani kubwa kwa Mwigulu Nchemba kuliko jeshi la polisi? Kwa maana hiyo huyu kiongozi wa CHADEMA ana ubia gani na Mwigulu Nchemba ambaye ni kiongozi wa CCM chama ambacho CHADEMA wanajiandaa kukiondoa madarakani? Je ni marafiki? Au huyu kiongozi wa CHADEMA ni shushu au jasusi? Na kama ni shushu au jasusi aliwekwa pale CHADEMA na usalama wa Taifa kwa nini asiipeleke hiyo video huko usalama wa Taifa na halafu ikasubiriwa watu kufikishwa mahakamani? Au je huyu kiongozi wa CHADEMA ni shushu/jasusi aliyepelekwa pale na taasisi nyingine? Na je hiyo taasisi nyingine ambayo ina “interest” na mipango ya CHADEMA ni ipi hiyo? Kitendo cha huyu kiongozi wa CHADEMA kumpelekea Mwigulu Nchemba hiyo video kinanyoosha kidole moja kwa moja kwa CCM kwamba ndio taasisi ilyomweka huyu kiongozi wa CHADEMA kwa mambo wanayoyajuwa wao?

Sasa nirudi kwa Mwigulu Nchemba.Yeye alipata video inaonyesha mipango ya mauaji kwa namna alivyoipata anajuwa mwenyewe. Je yeye alipaswa kufanya nini? Kwa mtu mwenye akili timamu baada ya kuipata,yeye angaipeleka polisi na kukaa kimya kabisa hadi atakapoitwa mahakamani kama atahitajika kutoa ushahidi. Lakini badala yake alifanya nini? Yeye alikwenda pale StarTV na kusema kuwa anayo video inonyesha viongozi wa CHADEMA wakipanga mauaji ya raia. Hakusema kuwa alipeleka ushahidi huo polisi ila alisema mimi(yeye) ana video. Je alivyokwenda pale StarTV alishaipeleka hiyo video polisi? Na kama alishaipeleka polisi kwa nini aongelee kwenye chombo cha habari jambo ambalo lipo katika uchunguzi wa polisi? Haoni kwamba hapo alikuwa anaingilia kazi ya polisi na kuwa kisababishi cha uhalifu kutendeka? Haoni kwamba alikuwa anaisaidia CHADEMA kujipanga kupoteza ushahidi?

Kimsingi Mwigulu Nchemba kuwa na video inayoonyesha viongozi wa CHADEMA wakipanga mauaji ya raia na halafu asiipeleke polisi kwa wakati ni kosa. Vilevile yeye kuwa na video na kuipeleka polisi halafu anarudi kuiongelea kwenye chombo cha habari kosa pia. Labada iwe kwamba yeye ni sehemu ya timu ya polisi inayofanya uchunguzi huo.Hata kama angekuwa ni mmojawapo wa timu ya makachero wanaofanya uchunguzi huo bado asingeweza kwenda kuliongelea jambo hilo kwenye luninga.Hii si namna polisi yenye weledi ifanyavyofanya kazi.Je inawezekana Mwigulu alifanya makosa ya kiufundi katika hili?
Kwa kuwa Mwigulu Nchemba ni kiongozi mwandamizi wa CCM na alifanya makosa yote mawili,hii inamkosesha sifa na haki ya kuitwa kiongozi makini na mwadilifu. Kiongozi mwenye upeo wa kuangalia maslahi mapana ya Taifa mabali na chama chake.
Na kufanya mambo kwa namna alivyofanya Mwigulu ndio kunaamsha na kuhalalisha hisia kwamba CHADEMA ni muathirika wa mambo yaliyotengenezwa na CCM kwa kushirikiana na vyombo vya usalama vya dola kwa lengo la kuisambaratisha kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015. Hii inaakisi kauli iliyowahi kutolewa na Waziri mwandamizi iliyendani ya Ofisi ya Rais(Ikulu) kuwa watahakikisha CHADEMA inasambaratika kabla ya mwaka 2015. Hii inatufunua macho sisi wananchi wa kawaida na kuunganisha matukio yaliyowahi kutokea huko nyuma wakati vyama vya NCCR na CUF vilipokuwa na nguvu na juu ya watu mashuhuri ambao kwa nyakati tofauti waliwahi kuipinga CCM na serikali yake waziwazi. Hisia hizi za kwamba CHADEMA ni muathirika wa mipango ya wenye dola unapewa nguvu na msukumo mkubwa kwenda kwenye ukweli na ile kazi iliyofanywa na serikali ya kulifungia gazeti la MWANAHALISI kwa madai ya uchochezi.Sasa sisi tunaofunuafunua mambo kidogo tulisoma yale yaliyoandikwa kwenye MWANAHALISI juu ya utekaji na utesaji wa Dr.Ulimboka na nani alihusika na jinsi kamanda Kova alivyojichanganya kwa sarakasi na yule mkenya wake! Na amepewa tuzo ya kitaifa!!!
Nikumbushe tu kwamba wakati CUF ilivyokuwa na nguvu kisiasa ilisingiziwa kuwa ni chama chenye udini-kwa maana ya chama cha kiislamu. Hii ililenga kuwatisha wakristo kuwa CUF ikiingia madarakani itaongoza nchi kwa mfumo wa sharia,lahaulah!. Kwa wakristo wa kawaida hii inatisha sana. Kalikuwa ni kamchezo kachafu hivi kalikochezwa na watawala na ambako leo hii kameendelea kututafuna kama taifa- kamchezo ka kusingizia udini. Nani achinje kitoweo? Wengine kutoa takwimu za idadi ya wakristo na waislamu walioteuliwa katika baraza la mawaziri na viongozi waandamizi kupinga kwamba Rais rais wetu ni mdini, ndio mambo yanayojadiliwa na wakubwa huko bungeni.Aibu!!Wanasingizia na halafu mambo yanatokea kweli. Ni kama hili la ugaidi. Wanapiga kelele huyu gaidi,hawa magaidi,chama kile cha magaidi halafu hii inakuwa kweli- halafu baadaye unakuja ugaidi kweli tunakosa pa kutokea kama nchi.
Samahani nimetoka njema ya mada kidogo. Katika lile sakata la CUF ilipoonekana kuwa hiyo sindano ya udini kwa CUF haikuingia sawasawa siku chache kabla ya uchaguzi, IGP mtaafu Omary Mahita akaja kwenye luninga na visu vyenye bendera ya CUF na kusema kwamba CUF wameingiza makontena ya visu na majambia. Hii ilikuwa ni kutisha wapiga kura wahamaki zaidi! Mfano mwingine ni yale yaliyowatokea NCCR Mageuzi na viongozi wao wakati ilipokuwa na nguvu. Mrema na viongozi wenzake waliandamwa waziwazi na hadith ninayokumbuka vizuri ni ile ya Lamwai.Yeye aliandamwa wamkamtoa kule chuo kikuu kama mwizi,akadhibitiwa na kashindwa hata kufanya kazi zake za uwakili Tanzania bara.Sijui kama na kule Visiwani Zanzibar walimfuatilia na kumbana,sina uhakika.Baadaye nadhani alienda kupatana na wenye dola wakati huo mambo yake yakawa shwari. Kuanzia hapo,sijapata kumsikia tena Lamwai akinguruma katika siasa za Tanzania,kimya kabisa!
Mifano ni mingi sana ipo ya akina Horace Kolimba waliodai kuwa CCM si ukuta wa Berlin,kwani hata ukuta wa Berlin ulianguka? Mara yeye akaanguka futi sita china ya udongo! Nimejaribu kuelezea haya matukio machache shabaha ikiwa ni kuonyesha kwamba kuna “behavior pattern” ya namna watawala wetu(chama tawala na serikali)wanavyowashughulikia taasisi na au watu ambao wanaoonekana kuleta hatari(threat) katika maslahi yanayotokana na utawala wao. Kama hatari hii ingekuwa inahatarisha maslahi ya uongozitu kwa maana ya kwamba serikali hiyo ni safi na inaoongozwa kwa usafi yasingewapata hawa wanaojadiliwa hapa. Kwa haya matukio yamekuwa ni kama sindano za ganzi ambazo dola imekuwa ikiwapiga wananchi kila mara pale ambapo wanona mtu ama taasisi inatoa hatari za waziwazi.
Hizi sindano za ganzi wananchi wa Tanzania wamepigwa kwa muda mrefu sana. Wanapigwa ganzi na halafu wanakuta wameshafanyiwa upasuaji sehemu ambayo sipo penye ugonjwa. Sasa tabia ya ganzi ikizoea mwili upasuaji mgonjwa anasikia maumivu makali. Hii itatokea ikiwa hiyo dozi ya gazi itapigwa kwa kiwango kilekile ambacho mwili umezoea. Ili yasiwepo maumivu na mgonjwa asishituke kuwa anafanyiwa upasuaji sehemu ambayo sipo penye ungonjwa inabidi dozi iongezwe. Kwa maana nyingine lazima hiyo dozi impeleke huyu mwananchi kwenye mbingu nyingine tofauti na ile alipo sasa. Yaani awe pale waingereza wanapopaita “next level” Je kwa mantiki tu haiwezekani kuongeza dozi tafsiri yake ni kuteka, kutesa,kung’oa watu meno,kucha? Kwamba msanifu mkuu “chief Architect” ameagiza watu wasiuawe bali wapewe vilema vya maisha ili iwe ni onyo kwa wengine wote ambao wanaleta kiherehere cha kutaka kuibalisha CCM iwe chama cha upinzani? Sioni ni kwa nini hi isiwe uwezekano.
Kwa namna swala la ugaidi lilivyohusishwa na CHADEMA,makandokando yanayolizunguka , jinsi ambavyo siasa imehuishwa na swala zima nachelea kusema hii ni jinai nyingine kama ile ya CUF kutenda jinai ya kuingiza makontena ya visu na majambia. Kama kweli CUF wakati huo wakiwa na nguvu waliingiza makontena hayo ni nani katika CUF alipata kupelekwa mahakamani kwa kutenda jinai hiyo? Shida kubwa ninayoiona hapa ni kwamba uchaguzi wa 2015 umeanza mapema sana. Na kuna chama hakitaki kufika siku ya kupiga kura kikiwa dhaifu kama ilivyokuwa mwaka 2010. Na kwamba kwa vyovyote vile CHADEMA lazima isambaratike na isahaulike mapema iwezekanavyo kabla ya uchaguzi.Kwamba bila kusambaratika kwa CHADEMA itakuwa hatari.Je CHADEMA watakubali? Je kuisambaratisha CHADEMA ni kazi inayofanywa kwa maslahi ya Taifa la Tanzania au ni kwa maslahi ya kikundi cha watu wachache? Kama ni ndio hayo maslahi ni yepi hasa? Na wenye maslahi haya ni kina nani?
Kwa mtazamo wangu naona kuwa Video ya Lwakatare ni kitu cha kutengenezwa ili kuwababaisha wananachi wa hali ya kawaida ambao huwa hawatumii muda wao mwingi kusoma habari na kuzichambua ili kupata ukweli. Na kuwa utengenezwaji huu wa propaganda unalenga pale ambao watanzania walio wengi wana udhahifu napo- ile hali ya kutopenda kujisomea na kutafuta ukweli juu ya mambo mbalimbali pamoja na ile silka kusikia mambo,kuyaamini na kuyafanyia kazi bila kufanya utafiti-tabia ya majungu na umbea.Je kama sio kitu cha kutengenezwa ni kwa nini basi kinajisiwe na kisiasishwe kuanzia pale StarTV hadi bungeni na kinara akiwa Mwigulu Nchemba? Hii haiingi akili wala kuwa na mantiki na kwamba ni ubabaishaji unaolenga kuwababaisha wananchi wa kawaida-wale ambao wanatumia nguvu nyingi sana kufanya kazi kwa ujira mdogo na kutokuwa na uhakika na mlo wao wa kesho! Huu ni mtazamo nakaribisha kokosolewa
 
CHADEMA tishio sana... yani umeitaja zaidi ya mara mia moja.

Kalale sasa.
 
Movie ishachuja hiyo, sasa tunageukia upande wa pili.Tunataka video ya Kinana akiwa na majangili wakipanga njama za kuua tembo.Au Mwigulu hana hii episode?
 
Chadema hivi sasa kinaweweseka kuchafua watu ili kujisafisha na video ya kigaidi waliyoshikwa nayo
 
vijana wa buku 7 mna matatizo sana.
muda wa kujadili chadema umeisha tekelezeni ahadi zenu
mtajikuta mnajifunika shuka kushakucha
wenzenu chadema wanachanja mbuga.
watanzania hawataki pumba wanataka kuona maendeleo.
kalale sasa.
 
Walivyo wabaya wameamua kuitafuta roho ya mama yake zitto baada ya juhudi za kuipata ya zitto mwenyewe kushindikana
 
vijana wa buku 7 mna matatizo sana.
muda wa kujadili chadema umeisha tekelezeni ahadi zenu
mtajikuta mnajifunika shuka kushakucha
wenzenu chadema wanachanja mbuga.
watanzania hawataki pumba wanataka kuona maendeleo.
kalale sasa.
Tulia dawa iingie vizuri, waambie na wenzako
 
Wamehangaika kupotosha wananchi kuhusu ile video eti ugaidi hauwezi kupangwa na watu wawili, hawa jamaa hamnazo kweli kweli
 
kuna watu humu hawatumii ubongo kujibu hoja
hawa ni wale form 4 failure na wachumia tumbo
ama kweli ukiwa mwana CCM lazima uwe na akili pungufu
wako bize kujibizana na wanaowapinga badala ya kutimiza ahadi zao.
kuna watu watajinyonga sana 2015 kuiba kura haitawezekana tena
 
Mwandishi alitengeneza title nzuri na nikavutiwa nayo kwa kujua ni mpigania haki na c mwathirika wa itikadi yyt isiyo ya kichama wala Dini,nami nikaona nipitie nijue kama tunaweza ku-share mawazo ili kujuzana kama hiyo clip ni ya kutengenezwa ama lah, lkn nilichobaini humo ndani ni siasa isiyojenga wala kutafuta ukweli bali ni kuchanganya mambo kibao na c Lwakatale tena,kikubwa tujitahidi kuibua mambo yenye kuleta mantiki na kumsaidia kila mtanzania wa leo,kuna mambo mengi yenye manufaa,fanya tukukumbuke na c hoja za kuchochea uadui baina ya Watanzania
 
CHADEMA ni nguvu ya umma. CCM mnaweza kushindana na umma wa watanzania? Achen propaganda fanyen kaz watanzania twashwawajua nyie ni waongo, mafisad, majangili kila kukcha mnapanga kuiba raslmal na kukandamiza haki za wanyonge. Acheni kuichafua CHADEMA .kwan mchezo wenu ushajulikana na watanzania wote wanajua badala yake fanye maendeleo. Tumechoka propaganda, uzushi hatutak na naomba vijana tuhamasishane tujiandikishe katka daftar la kupga kura kwa ajil ya ukomboz dhabt
 
Chadema hivi sasa kinaweweseka kuchafua watu ili kujisafisha na video ya kigaidi waliyoshikwa nayo

Vipi bwana unajisikiaje chama chako kuongozwa na katibu JANGILI na kwamba kwenye baa wateja WANAAGIZA TU"NIPE KI...A MOJA BARIDI".
 
MTAZAMO KUHUSU VIDEO YA LWAKATARE
Nikiri kwamba uwepo wa hii video wa kinachodaiwa kuwa CHADEMA kupanga mauaji ya raia umeumiza sana moyo wangu wa utanzania.Yawe ni mambo ya kupangwa au yaliyofanywa na CHADEMA yameniumiza sana kama raia wa Tanzania. Ni afadhali kama kuumizwa huku kungenifanya hata nilie ili hiyo sumu ya maumivu iweze kwisha,ila kulia nashindwa na maumivu haya hayawezi kutulizwa na panado!
Kama mwananchi wa kawaida,nimejaribu kufutilia juu ya hili sakata la Lwakatare lakini naona haya mambo tunayoambiwa na wenye dola hayajumlishiki na hayaleti mantiki. Hii ni kutokana na kwamba ukijaribu kupiga darubini nyuma katika matukio yaliyowahi kufanyika katika mazingira kama haya,shaka kubwa inaonekana kuzunguka kila kona ya jambo hili na kutoa mwanya mkubwa wa ama kufeli mantiki ya kawaida na au mtihani wa litimasi “litmus test fealuire”
Wakati swala hili linaanza,Mwigulu Nchemba alidai kwamba mtu aliyempa hiyo video ni kiingozi wa CHADEMA ambaye amechukizwa na yale ambayo wanafanya viongozi wa CHADEMAna-yaani kupanga kuuwa raia.
Sasa nianze na huyo kiongozi wa CHADEMA. Katika hali ya kawaida kabisa mtu unapoona kuwa jinai imetendeka au inataka kutendeka na ushahidi unao wa kuweza kuzuia jinai isitendeke, je ushahidi huo unaupeleka wapi? Unaupeleka polisi au unampelekea kiongozi wa kisiasa wa cha pinzani(Mwigulu Nchemba) kama alivyofanya huyu kiongozi wa CHADEMA? CCM na CHADEMA wao ni washindani wa kisiasa au kwa kiingereza “antagonists”. Je huyu kiongozi wa CHADEMA aliyepeleka hii video kwa Mwigulu Nchemba badala ya kuipeleka polisi alilenga nini hasa? Kwani Mwigulu Nchemba yeye ni “criminal investigator” wa jeshi la polisi Tanzania?
Je huyo kiongozi wa CHADEMA ana imani kubwa kwa Mwigulu Nchemba kuliko jeshi la polisi? Kwa maana hiyo huyu kiongozi wa CHADEMA ana ubia gani na Mwigulu Nchemba ambaye ni kiongozi wa CCM chama ambacho CHADEMA wanajiandaa kukiondoa madarakani? Je ni marafiki? Au huyu kiongozi wa CHADEMA ni shushu au jasusi? Na kama ni shushu au jasusi aliwekwa pale CHADEMA na usalama wa Taifa kwa nini asiipeleke hiyo video huko usalama wa Taifa na halafu ikasubiriwa watu kufikishwa mahakamani? Au je huyu kiongozi wa CHADEMA ni shushu/jasusi aliyepelekwa pale na taasisi nyingine? Na je hiyo taasisi nyingine ambayo ina “interest” na mipango ya CHADEMA ni ipi hiyo? Kitendo cha huyu kiongozi wa CHADEMA kumpelekea Mwigulu Nchemba hiyo video kinanyoosha kidole moja kwa moja kwa CCM kwamba ndio taasisi ilyomweka huyu kiongozi wa CHADEMA kwa mambo wanayoyajuwa wao?

Sasa nirudi kwa Mwigulu Nchemba.Yeye alipata video inaonyesha mipango ya mauaji kwa namna alivyoipata anajuwa mwenyewe. Je yeye alipaswa kufanya nini? Kwa mtu mwenye akili timamu baada ya kuipata,yeye angaipeleka polisi na kukaa kimya kabisa hadi atakapoitwa mahakamani kama atahitajika kutoa ushahidi. Lakini badala yake alifanya nini? Yeye alikwenda pale StarTV na kusema kuwa anayo video inonyesha viongozi wa CHADEMA wakipanga mauaji ya raia. Hakusema kuwa alipeleka ushahidi huo polisi ila alisema mimi(yeye) ana video. Je alivyokwenda pale StarTV alishaipeleka hiyo video polisi? Na kama alishaipeleka polisi kwa nini aongelee kwenye chombo cha habari jambo ambalo lipo katika uchunguzi wa polisi? Haoni kwamba hapo alikuwa anaingilia kazi ya polisi na kuwa kisababishi cha uhalifu kutendeka? Haoni kwamba alikuwa anaisaidia CHADEMA kujipanga kupoteza ushahidi?

Kimsingi Mwigulu Nchemba kuwa na video inayoonyesha viongozi wa CHADEMA wakipanga mauaji ya raia na halafu asiipeleke polisi kwa wakati ni kosa. Vilevile yeye kuwa na video na kuipeleka polisi halafu anarudi kuiongelea kwenye chombo cha habari kosa pia. Labada iwe kwamba yeye ni sehemu ya timu ya polisi inayofanya uchunguzi huo.Hata kama angekuwa ni mmojawapo wa timu ya makachero wanaofanya uchunguzi huo bado asingeweza kwenda kuliongelea jambo hilo kwenye luninga.Hii si namna polisi yenye weledi ifanyavyofanya kazi.Je inawezekana Mwigulu alifanya makosa ya kiufundi katika hili?
Kwa kuwa Mwigulu Nchemba ni kiongozi mwandamizi wa CCM na alifanya makosa yote mawili,hii inamkosesha sifa na haki ya kuitwa kiongozi makini na mwadilifu. Kiongozi mwenye upeo wa kuangalia maslahi mapana ya Taifa mabali na chama chake.
Na kufanya mambo kwa namna alivyofanya Mwigulu ndio kunaamsha na kuhalalisha hisia kwamba CHADEMA ni muathirika wa mambo yaliyotengenezwa na CCM kwa kushirikiana na vyombo vya usalama vya dola kwa lengo la kuisambaratisha kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015. Hii inaakisi kauli iliyowahi kutolewa na Waziri mwandamizi iliyendani ya Ofisi ya Rais(Ikulu) kuwa watahakikisha CHADEMA inasambaratika kabla ya mwaka 2015. Hii inatufunua macho sisi wananchi wa kawaida na kuunganisha matukio yaliyowahi kutokea huko nyuma wakati vyama vya NCCR na CUF vilipokuwa na nguvu na juu ya watu mashuhuri ambao kwa nyakati tofauti waliwahi kuipinga CCM na serikali yake waziwazi. Hisia hizi za kwamba CHADEMA ni muathirika wa mipango ya wenye dola unapewa nguvu na msukumo mkubwa kwenda kwenye ukweli na ile kazi iliyofanywa na serikali ya kulifungia gazeti la MWANAHALISI kwa madai ya uchochezi.Sasa sisi tunaofunuafunua mambo kidogo tulisoma yale yaliyoandikwa kwenye MWANAHALISI juu ya utekaji na utesaji wa Dr.Ulimboka na nani alihusika na jinsi kamanda Kova alivyojichanganya kwa sarakasi na yule mkenya wake! Na amepewa tuzo ya kitaifa!!!
Nikumbushe tu kwamba wakati CUF ilivyokuwa na nguvu kisiasa ilisingiziwa kuwa ni chama chenye udini-kwa maana ya chama cha kiislamu. Hii ililenga kuwatisha wakristo kuwa CUF ikiingia madarakani itaongoza nchi kwa mfumo wa sharia,lahaulah!. Kwa wakristo wa kawaida hii inatisha sana. Kalikuwa ni kamchezo kachafu hivi kalikochezwa na watawala na ambako leo hii kameendelea kututafuna kama taifa- kamchezo ka kusingizia udini. Nani achinje kitoweo? Wengine kutoa takwimu za idadi ya wakristo na waislamu walioteuliwa katika baraza la mawaziri na viongozi waandamizi kupinga kwamba Rais rais wetu ni mdini, ndio mambo yanayojadiliwa na wakubwa huko bungeni.Aibu!!Wanasingizia na halafu mambo yanatokea kweli. Ni kama hili la ugaidi. Wanapiga kelele huyu gaidi,hawa magaidi,chama kile cha magaidi halafu hii inakuwa kweli- halafu baadaye unakuja ugaidi kweli tunakosa pa kutokea kama nchi.
Samahani nimetoka njema ya mada kidogo. Katika lile sakata la CUF ilipoonekana kuwa hiyo sindano ya udini kwa CUF haikuingia sawasawa siku chache kabla ya uchaguzi, IGP mtaafu Omary Mahita akaja kwenye luninga na visu vyenye bendera ya CUF na kusema kwamba CUF wameingiza makontena ya visu na majambia. Hii ilikuwa ni kutisha wapiga kura wahamaki zaidi! Mfano mwingine ni yale yaliyowatokea NCCR Mageuzi na viongozi wao wakati ilipokuwa na nguvu. Mrema na viongozi wenzake waliandamwa waziwazi na hadith ninayokumbuka vizuri ni ile ya Lamwai.Yeye aliandamwa wamkamtoa kule chuo kikuu kama mwizi,akadhibitiwa na kashindwa hata kufanya kazi zake za uwakili Tanzania bara.Sijui kama na kule Visiwani Zanzibar walimfuatilia na kumbana,sina uhakika.Baadaye nadhani alienda kupatana na wenye dola wakati huo mambo yake yakawa shwari. Kuanzia hapo,sijapata kumsikia tena Lamwai akinguruma katika siasa za Tanzania,kimya kabisa!
Mifano ni mingi sana ipo ya akina Horace Kolimba waliodai kuwa CCM si ukuta wa Berlin,kwani hata ukuta wa Berlin ulianguka? Mara yeye akaanguka futi sita china ya udongo! Nimejaribu kuelezea haya matukio machache shabaha ikiwa ni kuonyesha kwamba kuna “behavior pattern” ya namna watawala wetu(chama tawala na serikali)wanavyowashughulikia taasisi na au watu ambao wanaoonekana kuleta hatari(threat) katika maslahi yanayotokana na utawala wao. Kama hatari hii ingekuwa inahatarisha maslahi ya uongozitu kwa maana ya kwamba serikali hiyo ni safi na inaoongozwa kwa usafi yasingewapata hawa wanaojadiliwa hapa. Kwa haya matukio yamekuwa ni kama sindano za ganzi ambazo dola imekuwa ikiwapiga wananchi kila mara pale ambapo wanona mtu ama taasisi inatoa hatari za waziwazi.
Hizi sindano za ganzi wananchi wa Tanzania wamepigwa kwa muda mrefu sana. Wanapigwa ganzi na halafu wanakuta wameshafanyiwa upasuaji sehemu ambayo sipo penye ugonjwa. Sasa tabia ya ganzi ikizoea mwili upasuaji mgonjwa anasikia maumivu makali. Hii itatokea ikiwa hiyo dozi ya gazi itapigwa kwa kiwango kilekile ambacho mwili umezoea. Ili yasiwepo maumivu na mgonjwa asishituke kuwa anafanyiwa upasuaji sehemu ambayo sipo penye ungonjwa inabidi dozi iongezwe. Kwa maana nyingine lazima hiyo dozi impeleke huyu mwananchi kwenye mbingu nyingine tofauti na ile alipo sasa. Yaani awe pale waingereza wanapopaita “next level” Je kwa mantiki tu haiwezekani kuongeza dozi tafsiri yake ni kuteka, kutesa,kung’oa watu meno,kucha? Kwamba msanifu mkuu “chief Architect” ameagiza watu wasiuawe bali wapewe vilema vya maisha ili iwe ni onyo kwa wengine wote ambao wanaleta kiherehere cha kutaka kuibalisha CCM iwe chama cha upinzani? Sioni ni kwa nini hi isiwe uwezekano.
Kwa namna swala la ugaidi lilivyohusishwa na CHADEMA,makandokando yanayolizunguka , jinsi ambavyo siasa imehuishwa na swala zima nachelea kusema hii ni jinai nyingine kama ile ya CUF kutenda jinai ya kuingiza makontena ya visu na majambia. Kama kweli CUF wakati huo wakiwa na nguvu waliingiza makontena hayo ni nani katika CUF alipata kupelekwa mahakamani kwa kutenda jinai hiyo? Shida kubwa ninayoiona hapa ni kwamba uchaguzi wa 2015 umeanza mapema sana. Na kuna chama hakitaki kufika siku ya kupiga kura kikiwa dhaifu kama ilivyokuwa mwaka 2010. Na kwamba kwa vyovyote vile CHADEMA lazima isambaratike na isahaulike mapema iwezekanavyo kabla ya uchaguzi.Kwamba bila kusambaratika kwa CHADEMA itakuwa hatari.Je CHADEMA watakubali? Je kuisambaratisha CHADEMA ni kazi inayofanywa kwa maslahi ya Taifa la Tanzania au ni kwa maslahi ya kikundi cha watu wachache? Kama ni ndio hayo maslahi ni yepi hasa? Na wenye maslahi haya ni kina nani?
Kwa mtazamo wangu naona kuwa Video ya Lwakatare ni kitu cha kutengenezwa ili kuwababaisha wananachi wa hali ya kawaida ambao huwa hawatumii muda wao mwingi kusoma habari na kuzichambua ili kupata ukweli. Na kuwa utengenezwaji huu wa propaganda unalenga pale ambao watanzania walio wengi wana udhahifu napo- ile hali ya kutopenda kujisomea na kutafuta ukweli juu ya mambo mbalimbali pamoja na ile silka kusikia mambo,kuyaamini na kuyafanyia kazi bila kufanya utafiti-tabia ya majungu na umbea.Je kama sio kitu cha kutengenezwa ni kwa nini basi kinajisiwe na kisiasishwe kuanzia pale StarTV hadi bungeni na kinara akiwa Mwigulu Nchemba? Hii haiingi akili wala kuwa na mantiki na kwamba ni ubabaishaji unaolenga kuwababaisha wananchi wa kawaida-wale ambao wanatumia nguvu nyingi sana kufanya kazi kwa ujira mdogo na kutokuwa na uhakika na mlo wao wa kesho! Huu ni mtazamo nakaribisha kokosolewa

kwa taarifa yako ccm haikubaliki c mtaani ,vijiweni ,makazini nk watu hawamini propaganda tena hii video watu wanajua ukweli
 
Back
Top Bottom