Mechanist
JF-Expert Member
- Jan 31, 2015
- 724
- 491
Wanajamvi habarini za asubuhi.
Katika siku ya leo nnapenda kuwashirikisha katika mada hii kuhusu huduma za afya katika nchi yetu ya Tanzania hususani zitolewazo katika hospitali na vituo vya afya vya umma.
Tukienda katika uhalisia huduma zinazotolewa na hospitali na vituo vya afya vya umma ni mbovu mbovu mbovu.
Unakuta hospitali inaitwa hospitali ya rufaa lakini inaishiwa vifaa tiba tena vile vidogovidogo kama clean gloves, sterile gloves, syringes na catheters! Halafu inaitwa hospitali ya rufaa!
Mbona huduma zake hazina tofauti na zahanati? Ilikuwaje ikapandishwa hadhi na kuiita hospitali ya rufaa? Je zinapandishwa hadhi kisiasa?
Kama umesomea mambo ya tiba, Katika hospitali utakuta watu wanatibiwa katika mazingira hatarishi na ndo maana complications kama sepsis kwa post - operative pts ni kawaida. Ndipo nikakumbuka maneno ya mwalimu wangu "kutibiwa Tanzania ni hatari sana" na ndo maana hao wanasiasa wanaowadanganya wamewazidi akili wao huenda nje ya nchi kutibiwa.
Hatari hii hutokana na watu waliopewa kusimamia mfumo wa afya kuwa na udhaifu mkubwa katika kusimamia majukumu yao. Bahati nzuri naibu wa wizara hii tunaye humu naye ni medical doctor(MD)! tunamwomba aje humu atwambie.
Je, ni sahihi Intern doctor kuachiwa ward, kupita ward round bila usimamizi wa specialist?
Yaani ni nchi hii tu ambapo intern doctor ambaye hata kucanulate anatetemeka ndiye anayeona mgonjwa na kudiagnose bila supervision, unapewa midawa halafu kesho specialist akija anaitataa diagnosis, anabadilisha na kwa sababu wewe huna shule ya haya mambo unafikiri matibabu yameboreshwa kumbe ndo wanakuongezea shida! Hivi Mh waziri hujui sababu zinazochangia Anti - microbial resistance?
Kwa nini watu wanamezameza dawa bila prescription? Hata hivyo tatizo haliko kwa watu bali mfumo mbovu uliopo ndo unasababisha hayo.
Watanzania tunaishi na hatuangamii kwa sababu ya huruma za Mwenyezi MUNGU.
Aluta continua, victoria 'e certa. Ahsanteni sana.