Mtatiro: Viongozi wa CUF Rufiji, wanazidi kukamatwa na dola na kupelekwa kusikojulikana

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
VIONGOZI WENGINE WA CUF WAMEKAMATWA JANA!

Jana Ijumaa usiku Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilumike, Ikwiriri - Rufiji (CUF), amechukuliwa na vyombo vya dola kwa staili ile ile ya utekaji na hajulikani yuko wapi.

Jana hiyo hiyo, viongozi wawili wa CUF (Wenyeviti wa Kata tofauti), wamechukuliwa na vyombo vya dola (hawajulikani waliko). Naposema hawajulikani walipo nina maana kuwa asubuhi hii tayari tumepata uhakika kuwa hawapo kwenye vituo vya Polisi vya Rufiji.

Bado natoa wito kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama, kwamba viongozi hawa wapatikane wakiwa salama, lakini pia wasiteswe kama wale wengine 25, wahojiwe kwa njia sahihi na kama kuna ushahidi wowote muhimu wapelekwe mahakamani.

Kwa kweli tumechoka kuona viongozi wetu wanatekwa/kukamatwa na vyombo vya dola, wanateswa na kisha wanaachiwa. Oparesheni bubu za namna hii zinazolenga kuumiza watu wasio na hatia haziwezi kulisaidia taifa letu.

Viongozi wetu wa Rufiji/Mkuranga/Kibiti wote wanaripoti kuwa hivi sasa wale wenzao wa CCM ndiyo wanavielekeza vyombo vya dola viwakamate. Na wanaokamatwa ni viongozi wa kiserikali waliochaguliwa kupitia CUF pamoja na wale viongozi wa CUF (Matawi na Kata) wanaotoka maeneo ambayo CUF ina nguvu kisiasa.

Chama chetu kinataka Oparesheni ya kuwasaka wauaji na makundi mabaya katika wilaya hizi iendelee, lakini hatukubaliani na APPROACH ya kukamata viongozi wa kiserikali wa CUF kila mahali ambako CUF ina nguvu. Oparesheni ikiendelea kwa mtindo huu itaanza kuchukua mkondo wa kisiasa na itapoteza maana. Ukizungumza na raia wa Rufiji/Kibiti/Mkuranga - wanakueleza dhahiri kuwa mauaji ya viongozi zaidi ya 30 wa CCM hayakufanywa wala kupangwa na viongozi wa chama chochote cha siasa.

Sasa leo wanapokamatwa viongozi wa CUF wa kuchaguliwa almost kila mahali, tunasema kwa uwazi kuwa oparesheni hii itapoteza mashiko. Na Polisi haijiulizi kwa nini tangu ianze kukamata viongozi wa CUF haijawakuta na chochote? Kwa nini hadi jana iendelee kuwakamata? Ndugu zangu, hali hii haikubaliki kabisa. Vyombo vyetu vya Usalama hebu vifanye kazi zake kwa weledi na utaratibu unaozingatia haki, sheria na wajibu.

[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J.
 
Mbaya sana hiyo. Hiyo ndiyo intelijensia ambayo huwa wanatwambia wanapozuia mikutano na maandamano? Kwanini intelijensia hiyo haifanyi kazi kwenye mauaji huko Kibiti?!
 
Wanakoelekea wataanza kuwabambikia ushahidi wa Silaha na mabomu ili kuwatisha wananchi, matokeo yake watawaacha wahalifu wa kweli wakiendelea na uovu, hiyo ndiyo intellegencia ya polisi wetu
 
Hizi akili zimeenda likizo.

Wanatumia mabavu badala ya akili kutatua hili jambo.

Wanadhani watu wa CUF ndo wanahusika kumbe hata sio.

Wawakamate wote basi tuone kama hayo mauaji yatakoma.
 
Izo ndio akili za kamanda sirro alizokuja nazo

Kuna watu watakuja kushangalia hata huu upumbavu unaofanywa na polisi
 
VIONGOZI WENGINE WA CUF WAMEKAMATWA JANA!

Jana Ijumaa usiku Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilumike, Ikwiriri - Rufiji (CUF), amechukuliwa na vyombo vya dola kwa staili ile ile ya utekaji na hajulikani yuko wapi.

Jana hiyo hiyo, viongozi wawili wa CUF (Wenyeviti wa Kata tofauti), wamechukuliwa na vyombo vya dola (hawajulikani waliko). Naposema hawajulikani walipo nina maana kuwa asubuhi hii tayari tumepata uhakika kuwa hawapo kwenye vituo vya Polisi vya Rufiji.

Bado natoa wito kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama, kwamba viongozi hawa wapatikane wakiwa salama, lakini pia wasiteswe kama wale wengine 25, wahojiwe kwa njia sahihi na kama kuna ushahidi wowote muhimu wapelekwe mahakamani.

Kwa kweli tumechoka kuona viongozi wetu wanatekwa/kukamatwa na vyombo vya dola, wanateswa na kisha wanaachiwa. Oparesheni bubu za namna hii zinazolenga kuumiza watu wasio na hatia haziwezi kulisaidia taifa letu.

Viongozi wetu wa Rufiji/Mkuranga/Kibiti wote wanaripoti kuwa hivi sasa wale wenzao wa CCM ndiyo wanavielekeza vyombo vya dola viwakamate. Na wanaokamatwa ni viongozi wa kiserikali waliochaguliwa kupitia CUF pamoja na wale viongozi wa CUF (Matawi na Kata) wanaotoka maeneo ambayo CUF ina nguvu kisiasa.

Chama chetu kinataka Oparesheni ya kuwasaka wauaji na makundi mabaya katika wilaya hizi iendelee, lakini hatukubaliani na APPROACH ya kukamata viongozi wa kiserikali wa CUF kila mahali ambako CUF ina nguvu. Oparesheni ikiendelea kwa mtindo huu itaanza kuchukua mkondo wa kisiasa na itapoteza maana. Ukizungumza na raia wa Rufiji/Kibiti/Mkuranga - wanakueleza dhahiri kuwa mauaji ya viongozi zaidi ya 30 wa CCM hayakufanywa wala kupangwa na viongozi wa chama chochote cha siasa.

Sasa leo wanapokamatwa viongozi wa CUF wa kuchaguliwa almost kila mahali, tunasema kwa uwazi kuwa oparesheni hii itapoteza mashiko. Na Polisi haijiulizi kwa nini tangu ianze kukamata viongozi wa CUF haijawakuta na chochote? Kwa nini hadi jana iendelee kuwakamata? Ndugu zangu, hali hii haikubaliki kabisa. Vyombo vyetu vya Usalama hebu vifanye kazi zake kwa weledi na utaratibu unaozingatia haki, sheria na wajibu.

[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J.
Taarifa iliyotolewa na Mke ni Mume kutekwa na watu wasiojulikana na ametoa taarifa Polisi.

Mtatiro unasema wamechukuliwa na vyombo vya dola na hakuna taarifa Polisi!!

Umeuliza Polisi wamesema hawajui chochote zaidi ya kutekwa!! Sasa wakipatikana Maiti utasemaje Mtatiro??
 
Tangu mauaji yaanze sijawahi kumsikia huyu jamaa anaongea, Mario I do leo ameguswa sasa...
 
Back
Top Bottom