Mtatiro: Hivi vita vya Prof. Lipumba na idara za hamasa za CCM dhidi ya CUF, mwisho mshindi ni CUF

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
18,632
20,975
HIVI VITA VYA PROF HARUNA LIPUMBA NA IDARA NYENGINE ZA HAMASA ZA CCM DHIDI YA CUF SIKU YA MWISHO MSHINDI NI CUF - JULIUS MTATIRO

Prof. Kitila na wenzako. Sisi sote ni watu wazima na kila mtu ana uzoefu na akili. Itoshe tu kusema kuwa tatizo la CUF litashughulikiwa. Hata kama Msajili, Dola, ACT, CCM watakuwa nyuma ya Lipumba, CUF itashinda vita hii. CUF ingelianza kufanya mambo ya kihuni anayofanya Lipumba leo hii hivi sasa tungezungumza mambo tofauti sana.

Kwani Kitila unadhani hakuna maelfu ya wanachama wa kuvamia ofisi ya CUF, kumtoa Lipumba na kuingiza uongozi unaotambulika na chama? Hao wanachama wapo na wanaomba hata leo waruhusiwe kufanya chochote, wapo kwa maelfu hata hapa DSM, bahati mbaya ni kuwa Lipumba anadeal na watu wanaotaka kufuata taratibu sana, anadeal na sisi tusiohitaji kufanya uhuni n.k. kwa hiyo wewe Kitila na wenzako wachache mtamshangilia sana, kwa sababu mnajua CUF ikipasuka ACT itanufaika, CCM itanufaika na UKAWA itakufa. Lakini nataka ufahamu kuwa sisi ndani ya chama siyo wajinga, tunajua kila kinachoendelea na tunafanya kila kitu kwa kufuata katiba yetu. Mwisho wa mapambano haya ni ushindi mkubwa kwa CUF na si kwa Mtatiro.

Mimi, kwa bahati mbaya sana maishani mwangu, siongozwi na ufuasi. Nilipofika Mkutano Mkuu nilikuwa miongoni mwa wajumbe watatu waliopendekezwa kuwa Mwenyekiti wa Kikao, punde kura zikapigwa na asilimia 75 ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wakanipigia kura niongoze kikao, sikuteuliwa na Maalim Seif. Baraza Kuu lilipokutana baadaye lilinipendekeza kuongoza Kamati ua Uongozi, sikuteuliwa na Maalim Seif, ni Baraza Kuu. Mimi ni mwanasiasa nayekua na kujifunza na bahati mbaya niliyonayo katika maisha yangu ni kuwa kila mara nimekuwa nakabidhiwa majukumu makubwa tena katika nyakati ngumu, lakini mara zote hubezwa na mwisho mimi husimamia misingi na huwa kwenye kundi la washindi.

Mimi ni mwana CUF na hii ni vita ya ipumba+SYSTEM+ACT+CCM vs THE CIVIC UNITED FRONT. Nataka niwaambie kuwa CUF ndiye mshindi wa vita hii na tukishashinda vita hii njooni mniulize kwa nini niliwahi kusema hivyo. Tunazo nguvu za kushinda, sababu na rasilimali za kufanya hivyo. Wakati ni Ukuta.

Chanzo : Mtatiro J.
 
Kua makini kila uchao unaandika mambo meengi mengine unajichanganya mwishoe kila mtu unamwona mmbaya, kwa hali ilivyo sasa bora uwe mtulivu uyo unae shindana naye ni Profesa wewe bado mchanga katika siasa, Jifunze kwa Mnyika kwasasa ametulia ni mwangalifu katika kaulizake, kua makin wakina Maalimu watakutumia na utapotea mazima.
 
Kua makini kila uchao unaandika mambo meengi mengine unajichanganya mwishoe kila mtu unamwona mmbaya, kwa hali ilivyo sasa bora uwe mtulivu uyo unae shindana naye ni Profesa wewe bado mchanga katika siasa, Jifunze kwa Mnyika kwasasa ametulia ni mwangalifu katika kaulizake, kua makin wakina Maalimu watakutumia na utapotea mazima.
***
Tujifunze kuzungumzia jambo kwa uhalisia wake na ukweli halisi./
 
Mimi bado nina wasisi na siasa zinazofanyika kwenye nchi yetu viongonzi wetu mpo mnafanya siasa kwa masilahi yenu siyo kwa masilahi ya taifa hili Tanzania
Ifike mwisho Mmuongope basi ata Mungu
Viongozi mmejaa ubinafsi mioyo yenu inawaka tu tamaa ya madaraka.
Ni nini dhumuni kuu la vyama vya siasa kama sio kukamata madaraka?. Ubinafsi huo ni upi?. Kikubwa uwanja uwe huru na halali tu. Kawaambie haya CCM
 
Hivi hakuna taasisi inayotengua taaluma ya mtu coz huyu prof. anadhalilisha hii kada sasa maprof wote wataonekana Lipumba-vu
kwakweli ata nami naungana na wewe, taasisi ya kutengua taaluma ingekuwepo... anaambisha elimu yake...
 
Kila anayetoa maoni tofauti na kile wanachopenda kukisikia wanamjumuisha kuwa chanzo cha tatizo!!

Ushawishi wa Mtatiro ndani ya CUF ni negligible labda apewa mamluki na washirika wake.

Kwenye hili sakata lote Mtatiro ndiye atakuwa loser sababu ataishia kutimuliwa tu.
 
ACT inaingiaje hapa? watu wa taaluma na kada mbali mbali wanajadili suala hili kwa sababu lipo hot kwa sasa.

Kwa hiyo si kila anayejadili na kuwa na mtazamo tofauti na wa Mtatiro basi ni adui wa CUF.

Mtatiro usitafute mchawi....iondoe ACT katika kundi unalolilaumu.
 
Huyu mzee lipumba nina wasiwasi sn na uprof. wake anadhalilisha sn taaluma hiyo aliyonayo.Mtatiro yuko sawa na nionavyo mimi hiyo ni njama tuu ya kuisambaratisha CUF kwa kuwa Prof alishindwa kisambaratisha alipojiuzulu lengo halikutimia so karudi kwa mabavu ili amalize story
 
14390826_811899288952327_7469812458760100762_n.jpg
 
Tatizo kuu ndani ya vyama vyetu vya siasa ni kujaza MAKAHABA wa siasa ndani ya baadhi ya viongozi, kahaba siku zote hanaga mapenzi bali wao huangalia pesa tu
 
Kumbe act wamo kundi moja la kunufaika na mgogoro wa cuf ehh! Sishangai sanaaa, najua mission iko kazini hao wote kuanzia sisiem, msajiri, act, Lao moja.
 
Huyu mzee lipumba nina wasiwasi sn na uprof. wake anadhalilisha sn taaluma hiyo aliyonayo.Mtatiro yuko sawa na nionavyo mimi hiyo ni njama tuu ya kuisambaratisha CUF kwa kuwa Prof alishindwa kisambaratisha alipojiuzulu lengo halikutimia so karudi kwa mabavu ili amalize story
***
"THE BACK OF DESTROYER TO FINALISE THE MISSION"
 
Ukifuatilia vizuri siasa za hapa kwetu Tz utagundua kuwa vyama karibia vyote vya upinzani ni matawi madogo ya ccm ili tuu Tz ijulikane kuwa kuna vyama vingi vya siasa ila si kweli so lipumba ni lazima arudi ili atimize malengo yaliyokusudiwa na makubaliano tangu uundwaji wa Hivi vyama so pindi Chama cha upinzani kikionekana kinakiuka makubaliano ya kuwa tawi la ccm lazima kisambaratishwe mfano Mrema alikiuka makubaliano hadi kutaka urais wa nchi yuko wapi now??karudi kundini hadi sasa,so kwa lipumba na mrema ni sawa malengo wanayajua tangu hapo.NI MTAZAMO TUU
 
Julius Mtatiro ameandika hivi:

Prof. Kitila na wenzako. Sisi sote ni watu wazima na kila mtu ana uzoefu na akili. Itoshe tu kusema kuwa tatizo la CUF litashughulikiwa. Hata kama Msajili, Dola, ACT, CCM watakuwa nyuma ya Lipumba, CUF itashinda vita hii. CUF ingelianza kufanya mambo ya kihuni anayofanya Lipumba leo hii hivi sasa tungezungumza mambo tofauti sana. Kwani Kitila unadhani hakuna maelfu ya wanachama wa kuvamia ofisi ya CUF, kumtoa Lipumba na kuingiza uongozi unaotambulika na chama? Hao wanachama wapo na wanaomba hata leo waruhusiwe kufanya chochote, wapo kwa maelfu hata hapa DSM, bahati mbaya ni kuwa Lipumba anadeal na watu wanaotaka kufuata taratibu sana, anadeal na sisi tusiohitaji kufanya uhuni n.k. kwa hiyo wewe Kitila na wenzako wachache mtamshangilia sana, kwa sababu mnajua CUF ikipasuka ACT itanufaika, CCM itanufaika na UKAWA itakufa. Lakini nataka ufahamu kuwa sisi ndani ya chama siyo wajinga, tunajua kila kinachoendelea na tunafanya kila kitu kwa kufuata katiba yetu. Mwisho wa mapambano haya ni ushindi mkubwa kwa CUF na si kwa Mtatiro.
Mimi, kwa bahati mbaya sana maishani mwangu, siongozwi na ufuasi. Nilipofika Mkutano Mkuu nilikuwa miongoni mwa wajumbe watatu waliopendekezwa kuwa Mwenyekiti wa Kikao, punde kura zikapigwa na asilimia 75 ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wakanipigia kura niongoze kikao, sikuteuliwa na Maalim Seif. Baraza Kuu lilipokutana baadaye lilinipendekeza kuongoza Kamati ua Uongozi, sikuteuliwa na Maalim Seif, ni Baraza Kuu. Mimi ni mwanasiasa nayekua na kujifunza na bahati mbaya niliyonayo katika maisha yangu ni kuwa kila mara nimekuwa nakabidhiwa majukumu makubwa tena katika nyakati ngumu, lakini mara zote hubezwa na mwisho mimi husimamia misingi na huwa kwenye kundi la washindi. Mimi ni mwana CUF na hii ni vita ya Lipumba+SYSTEM+ACT+CCM vs THE CIVIC UNITED FRONT. Nataka niwaambie kuwa CUF ndiye mshindi wa vita hii na tukishashinda vita hii njooni mniulize kwa nini niliwahi kusema hivyo. Tunazo nguvu za kushinda, sababu na rasilimali za kufanya hivyo. Wakati ni Ukuta.
Mtatiro J.
 
Back
Top Bottom