Mtatiro,CHADEMA; Tatizo la CUF sio Mutungi,Tatizo ni Katiba ya CUF

kamati ya ufundi

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
416
439
e781744acb126e44ac4219106fdd64db.jpg

*MTATIRO, CHADEMA, TATIZO LA CUF SIO MUTUNGI, TATIZO NI KATIBA YA CUF*

Kushambulia mtu ni jambo rahisi Sana kuliko kuelezea ukweli wa mambo.

Ukiwasoma vijana wa CHADEMA, wanavyolalama juu ya sakata la CUF na msimamo wa jaji mutungi kama msajili wa vyama vya siasa nchini,

Ukamsoma Julius Mtatiro anavyolalama kuhusiana na jambo hilo hilo,

Ukapata nafasi ya kupitia maandiko ya wafuasi wa karibu wa maalim seif juu ya suala hilo hilo.

Utagundua jambo moja muhimu kubwa.

Jambo hilo ni kutokuelewa wapi walipojikwaa,
Maalim Seif na timu yake wamejikwaa, wanajua walipojikwaa lakini ama wanajitia upofu au wanajitia uchizi kutokuelewa walipojikwalia ili wainuke wasonge mbele.

WAMEJIKWAA WAPI? .

maalim Seif na wenzake wamejikwaa kwenye katiba ya Chama Chao, katiba yao wenyewe walioitunga na kuisimamia Sasa wamejikwaa nayo na imewaangusha mpaka chini wanampa kazi Jaji Mutungi.

Ukiwasikiliza Kina Mtatiro wanaishia kusema *"alijiuzulu mwenyewe, Sasa kwanini anataka kurudi ".*

au wanasema *"Alituacha kwenye mapambano vitani akatukimbia sasa anarudi kufata nini?".*

Wanaongeza kusema *"Msaliti huyu anatumiwa na CCM na serikali kutupoteza kwenye msingi wetu"..*

Ama wanasema *" Tulimuomba Sana alijiuzulu mpaka mashehe tukawatuma kwake, lakini alikataa akajiuzulu, sasa Leo anataka nini tena CUF? ".*

Hayo ndio maneno na msingi wa malalamiko yao.

Hawajawahi kusema popote kwamba Katiba ya Chama Chao inasemaje kiongozi anapotaka kujiuzulu? .

Hawasemi kwamba katiba ya CUF inamtaka kiongozi mkuu aliyechaguliwa na mkutano mkuu kabla hajakubaliwa kujiuzulu kwake basi mkutano mkuu uliomchagua ukutane kuidhinisha ama kukataa jambo hilo,

Hawazungumzi ukweli, Hawasemi kwamba Maalim Seif na wenzake wamezidiwa maarifa padogo tu na lipumba, pale alipoamua kung'ang'ania kutumia Katiba ya Chama chao,

Kwa hali ilivyotokea Maalim Seif kama katibu mkuu angeweza kuitisha mkutano mkuu wa CUF mapema Sana Mara tu baada ya Lipumba kujiuzulu mwezi wa nane mwaka 2015 na mkutano ule ungeridhia bila ya shida yoyote kumtimua Lipumba hasa kutokana na hali ilivyokuwa ya kisiasa nchini.

Maalim Seif na wenzake hawakutaka kufuata katiba yao, wameruhusu Kwa kusubili Lipumba kaji mobilize kajirudisha kwenye Chama ndio wameshtuka wakaitisha mkutano mkuu kumjadili Lipumba ( Mwaka mmoja baadae, hii wazungu wanaiita Too late )

Yaliyotokea kwenye mkutano yakawa mambo ya aibu Kwa seif, maana ilionyesha dhahiri kwamba Lipumba alikuwa amejiandaa na kujidhatiti kurudi kwenye Chama.

MUTUNGI ANAINGIAJE? .

Mutungi hajajipeleka kutoa maelekezo juu ya mgogoro wa CUF,

Mutungi amepokea malalamiko kutoka Kwa Wana Chama zaidi ya 300 wa CUF yeye akiwa kama mlezi na msajili wa vyama vyote vya siasa hapa nchini,

Akapokea tena na malalamiko ya Lipumba juu ya dhamira yake ya kutaka kurejea kwenye Chama chake Kwa mujibu wa katiba yao.

Mutungi kama msajili akaziita pande zote, upande wa Maalim Seif na Upande wa Lipumba, akajadiliana nao , kila upande ukatoa hoja zao, kwa mazungumzo na kwa maandishi.

Mwisho Mutungi akatoa ushauri kwa mujibu wa katiba ya CUF.

KESI MAHAKAMANI
Kitendo cha Wakina Maalim Seif kwenda mahakamani ni kithibitisho kuwa uamuzi uliotolewa na MUTUNGI ni halali kisheria kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazoongoza usajili na uendeshaji wa vyama vya siasa,

Ndio maana kina Mtatiro wakaenda kukata rufaa mahakamani, maana yake wanaitaka mahakama itengue uamuzi wa msajili wa vyama vya siasa kutokana na hoja walizozitoa ambazo pengine wanaamini zitawasaidia.

Kwa watu wenye hekima na wanaoheshimu utawala wa sheria hii ilikuwa ni hatua muhimu kabisa ya kudai haki.

Lakini kukesha mitandaoni na kwenye magazeti kumtukana msajili wa vyama vya siasa ni UZUZU usio kuwa na kifani,

Kusema tatizo lote la CUF ni msajili ni kumuonea, tatizo la CUF ni wao wenyewe kutokuheshimu na kuifuata katiba yao walioindika wenyewe.

Kama ambavyo akina maalim seif walikuwa na Imani na msajili wa vyama vya siasa na kuitikia wito kujibu malalamiko ya wanachama na msimamo wa Lipumba,

Ndivyo hivyo wanapaswa kumuheshimu na kuyaheshimu maamuzi yake mpaka hapo baadae kama mahakama itaamua vinginevyo.

Nina hakina na ni dhahiri kwamba hata kama maamuzi ya Mutungi yangekuwa upande wa maalim seif basi upande wa lipumba nao ungelalama hivi hivi.

Kuendelea kumtukana Mutungi na kumuhusisha kuihujumu CUF hakuondoi sintofahamu iliyopo ndani ya Chama hicho kikongwe.

Dalili zinaonyesha kwamba hivi sasa pande zote mbili zinavutana zikiwa na mahusiano ya nje ya Chama chao.

Naomba niishie hapa kwa sasa. Namaliza kwa kusema kuwa Kina Mtatiro kumtukana jaji Mutungi sio Dawa, Dawa ni kuitukana katiba yao iliyowafikisha hapo.
 
Mleta mada umeonesha jinsi gani unakusudia kupotosha ukweli au hujui usemamalo.

Lipumba hakuwahi kurudi katika nafasi yake ya uenyekiti wa CUF. Mamlaka zenye kuridhia kujiuzulu kwa Lipumba zilikuwa zimesharidhia kumuondoa Lipumba ndio maana Lipumba alivamia mkutano wa Blue Pearl. Mkutano Mkuu wa CUF ndicho chombo cha juu katika maamuzi ya chama. Ndio maana Lipumba alivamia mkutano mkuu wa CUF ukiwa katika hatua ya kuchagua mwenyekiti mpya. Mkutano mkuu ulikua mbioni kuchagua mwenyekiti mpya kwa sababu chama na mkutano Mkuu vilikuwa vimesharidhia na kuthibisha kuwa Lipumba sio mwenyekiti. Wasingefanya uchaguzi kabla ya kujiridhisha kuwa hakuna mwenyekiti.

Hoja yako ya Msajili wa vyama haina mashiko kwa mujibu wa katiba ya CUF. Ni wapi katiba ya CUF imemtaja Msajili wa vyama kama ni moja ya vyombo vya usuluhishi wa migogoro ya ndani ya chama (internal conflict resolution machineries)? Chama cha CUF kinaendeshwa kwa mujibu wa katiba yake na sheria za nchi. Je, ni sheria ipi inasema msajili wa vyama vya siasa atakuwa msuluhishi wa migogoro ya ndani ya vyama.

Mleta mada waliokutuma uje kupotosha waambie imeshindikana.
 
Sasa kumbavu kwanini yeye mwenyewe akasema anavunja neno lake badala ya kuomba huo mkutano mkuu ukae uamue uendele naye ama la?
Ndiyo ule akaenda kuoiga watu ama?

Bangi iendelee kuharamishwa kwakweli.
 
Katiba ya chama ingekuwa na matatizo Bwana yule asingeomba mazungumzo na Maalim
 
Ripumba runafanya kazi KIINTERAHAMWE tu! Kila mahali ni UVAMIZI. Analeta fujo kisha anaomba usuluhishi!
 
Propesa aliwahi kulalamika popote kuwa haitambui kamati ya uongozi chini ya Twaha Taslima km Kaimu Mwenyekiti wa CUF!!!
Na Jee alipokuwa akitaka kutumia Ofisi Kuu Buguruni kwa kufanya Press alikuwa haombi ruhusa kwa Mwenyekiti Taslima?kama alikuwa akiomba ni kusema alikuwa anamtambua Twaha Taslima kuwa ni Mwenyekiti?
 
Lipumba hana dhamira inayomuongoza, binadamu yoyte mwenye dhamira safi anapaswa kupima namna maamuzi yake yanavyoweza kuwaathiri watu wengine au kupokelewa na wenzake
 
Mkutano wa Blue Pearl wote tuliona bwana. Unawezaje kumzuia kuingia Mkutanoni mtu ambaye zaidi ya 70% ya wajumbe wanamuhitaji aje kujieleza? .
Mleta mada umeonesha jinsi gani unakusudia kupotosha ukweli au hujui usemamalo.

Lipumba hakuwahi kurudi katika nafasi yake ya uenyekiti wa CUF. Mamlaka zenye kuridhia kujiuzulu kwa Lipumba zilikuwa zimesharidhia kumuondoa Lipumba ndio maana Lipumba alivamia mkutano wa Blue Pearl. Mkutano Mkuu wa CUF ndicho chombo cha juu katika maamuzi ya chama. Ndio maana Lipumba alivamia mkutano mkuu wa CUF ukiwa katika hatua ya kuchagua mwenyekiti mpya. Mkutano mkuu ulikua mbioni kuchagua mwenyekiti mpya kwa sababu chama na mkutano Mkuu vilikuwa vimesharidhia na kuthibisha kuwa Lipumba sio mwenyekiti. Wasingefanya uchaguzi kabla ya kujiridhisha kuwa hakuna mwenyekiti.

Hoja yako ya Msajili wa vyama haina mashiko kwa mujibu wa katiba ya CUF. Ni wapi katiba ya CUF imemtaja Msajili wa vyama kama ni moja ya vyombo vya usuluhishi wa migogoro ya ndani ya chama (internal conflict resolution machineries)? Chama cha CUF kinaendeshwa kwa mujibu wa katiba yake na sheria za nchi. Je, ni sheria ipi inasema msajili wa vyama vya siasa atakuwa msuluhishi wa migogoro ya ndani ya vyama.

Mleta mada waliokutuma uje kupotosha waambie imeshindikana.
 
e781744acb126e44ac4219106fdd64db.jpg

*MTATIRO, CHADEMA, TATIZO LA CUF SIO MUTUNGI, TATIZO NI KATIBA YA CUF*

Kushambulia mtu ni jambo rahisi Sana kuliko kuelezea ukweli wa mambo.

Ukiwasoma vijana wa CHADEMA, wanavyolalama juu ya sakata la CUF na msimamo wa jaji mutungi kama msajili wa vyama vya siasa nchini,

Ukamsoma Julius Mtatiro anavyolalama kuhusiana na jambo hilo hilo,

Ukapata nafasi ya kupitia maandiko ya wafuasi wa karibu wa maalim seif juu ya suala hilo hilo.

Utagundua jambo moja muhimu kubwa.

Jambo hilo ni kutokuelewa wapi walipojikwaa,
Maalim Seif na timu yake wamejikwaa, wanajua walipojikwaa lakini ama wanajitia upofu au wanajitia uchizi kutokuelewa walipojikwalia ili wainuke wasonge mbele.

WAMEJIKWAA WAPI? .

maalim Seif na wenzake wamejikwaa kwenye katiba ya Chama Chao, katiba yao wenyewe walioitunga na kuisimamia Sasa wamejikwaa nayo na imewaangusha mpaka chini wanampa kazi Jaji Mutungi.

Ukiwasikiliza Kina Mtatiro wanaishia kusema *"alijiuzulu mwenyewe, Sasa kwanini anataka kurudi ".*

au wanasema *"Alituacha kwenye mapambano vitani akatukimbia sasa anarudi kufata nini?".*

Wanaongeza kusema *"Msaliti huyu anatumiwa na CCM na serikali kutupoteza kwenye msingi wetu"..*

Ama wanasema *" Tulimuomba Sana alijiuzulu mpaka mashehe tukawatuma kwake, lakini alikataa akajiuzulu, sasa Leo anataka nini tena CUF? ".*

Hayo ndio maneno na msingi wa malalamiko yao.

Hawajawahi kusema popote kwamba Katiba ya Chama Chao inasemaje kiongozi anapotaka kujiuzulu? .

Hawasemi kwamba katiba ya CUF inamtaka kiongozi mkuu aliyechaguliwa na mkutano mkuu kabla hajakubaliwa kujiuzulu kwake basi mkutano mkuu uliomchagua ukutane kuidhinisha ama kukataa jambo hilo,

Hawazungumzi ukweli, Hawasemi kwamba Maalim Seif na wenzake wamezidiwa maarifa padogo tu na lipumba, pale alipoamua kung'ang'ania kutumia Katiba ya Chama chao,

Kwa hali ilivyotokea Maalim Seif kama katibu mkuu angeweza kuitisha mkutano mkuu wa CUF mapema Sana Mara tu baada ya Lipumba kujiuzulu mwezi wa nane mwaka 2015 na mkutano ule ungeridhia bila ya shida yoyote kumtimua Lipumba hasa kutokana na hali ilivyokuwa ya kisiasa nchini.

Maalim Seif na wenzake hawakutaka kufuata katiba yao, wameruhusu Kwa kusubili Lipumba kaji mobilize kajirudisha kwenye Chama ndio wameshtuka wakaitisha mkutano mkuu kumjadili Lipumba ( Mwaka mmoja baadae, hii wazungu wanaiita Too late )

Yaliyotokea kwenye mkutano yakawa mambo ya aibu Kwa seif, maana ilionyesha dhahiri kwamba Lipumba alikuwa amejiandaa na kujidhatiti kurudi kwenye Chama.

MUTUNGI ANAINGIAJE? .

Mutungi hajajipeleka kutoa maelekezo juu ya mgogoro wa CUF,

Mutungi amepokea malalamiko kutoka Kwa Wana Chama zaidi ya 300 wa CUF yeye akiwa kama mlezi na msajili wa vyama vyote vya siasa hapa nchini,

Akapokea tena na malalamiko ya Lipumba juu ya dhamira yake ya kutaka kurejea kwenye Chama chake Kwa mujibu wa katiba yao.

Mutungi kama msajili akaziita pande zote, upande wa Maalim Seif na Upande wa Lipumba, akajadiliana nao , kila upande ukatoa hoja zao, kwa mazungumzo na kwa maandishi.

Mwisho Mutungi akatoa ushauri kwa mujibu wa katiba ya CUF.

KESI MAHAKAMANI
Kitendo cha Wakina Maalim Seif kwenda mahakamani ni kithibitisho kuwa uamuzi uliotolewa na MUTUNGI ni halali kisheria kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazoongoza usajili na uendeshaji wa vyama vya siasa,

Ndio maana kina Mtatiro wakaenda kukata rufaa mahakamani, maana yake wanaitaka mahakama itengue uamuzi wa msajili wa vyama vya siasa kutokana na hoja walizozitoa ambazo pengine wanaamini zitawasaidia.

Kwa watu wenye hekima na wanaoheshimu utawala wa sheria hii ilikuwa ni hatua muhimu kabisa ya kudai haki.

Lakini kukesha mitandaoni na kwenye magazeti kumtukana msajili wa vyama vya siasa ni UZUZU usio kuwa na kifani,

Kusema tatizo lote la CUF ni msajili ni kumuonea, tatizo la CUF ni wao wenyewe kutokuheshimu na kuifuata katiba yao walioindika wenyewe.

Kama ambavyo akina maalim seif walikuwa na Imani na msajili wa vyama vya siasa na kuitikia wito kujibu malalamiko ya wanachama na msimamo wa Lipumba,

Ndivyo hivyo wanapaswa kumuheshimu na kuyaheshimu maamuzi yake mpaka hapo baadae kama mahakama itaamua vinginevyo.

Nina hakina na ni dhahiri kwamba hata kama maamuzi ya Mutungi yangekuwa upande wa maalim seif basi upande wa lipumba nao ungelalama hivi hivi.

Kuendelea kumtukana Mutungi na kumuhusisha kuihujumu CUF hakuondoi sintofahamu iliyopo ndani ya Chama hicho kikongwe.

Dalili zinaonyesha kwamba hivi sasa pande zote mbili zinavutana zikiwa na mahusiano ya nje ya Chama chao.

Naomba niishie hapa kwa sasa. Namaliza kwa kusema kuwa Kina Mtatiro kumtukana jaji Mutungi sio Dawa, Dawa ni kuitukana katiba yao iliyowafikisha hapo.
UMESEMA KWELI . MAALIM SEIF KASABABISHA YOTE HAYA KWA KUTOFUATA TARATIBU BAADA YA LIPUMBA KUJIUZURU. LAKINI MBUMBUMBU WANAOMFUATA HAWATA KUELEWA.
 
Kama kweli Lipumba alikuwa amerudi chamani kama unavyodai, kulikuwa na haja gani ya kuvamia mkutano tena akisindikizwa na polisi? Huwezi kuhudhuria kikao usichoalikwa.Alialikwa cha awali hakufika, kikao cha pill ambacho hakualikwa akavamia! Halafu anataka tumwite profesa.Mhuni.
Utetezi wako umegonga mwamba mkuu.
 
Umeongea sawa kabisa. Kuna watu wanapenda kuambiwa wanayotaka kuambiwa hata kama si ya kweli. Ukweli ni kwamba wanasheria wa CUF walilala na hawakutimiza wajibu wao. Kulalamika na kutukana hakuwasaidii chochote, ni kupoteza muda tu. Option waliyonayo ni kukubali kukaa meza moja ili wazungumze. Swala la kwamba Prof. Lipumba aliwakimbia wakati wa vita na sababu zote wanazotoa hazina mashiko kisheria.
 
Back
Top Bottom