Kibanga Ampiga Mkoloni
JF-Expert Member
- Aug 9, 2007
- 19,093
- 9,261
ExactlyHuyo boss wa Takukuru anadhani watu watakaa kimya bila kumshinikiza, ni nani asiyejua vyombo vingi vya nchi hii vinavyofanya kazi kwa kujivuta? Cdm walitangaza miezi kadhaa nyuma kwamba hao madiwani wameondoka kwa kupewa rushwa, ni hatua gani walichukua mpaka sasa. Sawa tuchukulie ndio utendaji wao wa kizembe, sasa ushahidi umeletwa ni hatua gani mpaka sasa wanechukua? Sanasana ni vitisho visivyo na maana. Hao Takukuru kazi imebaki kuchunguza watu wenye kutofautiana na watawala.
Baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, kutoa onyo kwa Mbunge Nassari kuhusu ushahidi anaoutoa kuhusu wateule wa Rais kuwanunua madiwani Arusha, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, (CUF) Julius Mtatiro ameitaka taasisi hiyo kuchukua hatua na na siyo kumtishia mbunge huyo.
Mtatiro ametumia ukurasa wake wa Facebook, kwa kusema kwamba alitegemea TAKUKURU ingempongeza sana Nassari kwa kazi aliyofanya lakini kinyume chake wanamtisha na kumshtaki kwa kauli yake aliyoitoa jana kuwa ataendelea kutoa series ya matukio hayo yanayohusisha rushwa.
Mtatiro ameendelea kusema kwamba TAKUKURU ni chombo cha wananchi, siyo watawala na Nassari ni kiongozi na ni mwananchi, ana haki zote za kuikosoa na kuishinikiza taasisi ya kiuchunguzi ichukue hatua stahiki.
"TAKUKURU siyo mahakama na kwa kweli haina kinga dhidi ya "kulaumiwa na kushinikizwa na umma". TAKUKURU ijibu mashinikizo haya kwa kuchukua hatua, aidha kuwafikisha mahakamani wale watoa rushwa au kuwasafisha. Na iache kumtisha Nassari" ameandika Mtatiro
Aidha Mtatiro amehoji kwamba "Kwani Nassari akiendelea kutoa hizo video za ziada anafanya kosa gani kisheria. Kama ni kosa kwa nini wale watuhumiwa (watoa rushwa na wapokeaji) hawajampeleka mahakamani"?
Pamoja na hayo Mtatiro amesema kutokana na kauli za Mkurugenzi wa TAKUKURU haitabaki salama kwa kauli na mienendo ya namna hiyo ikiendelea kutolewa.
Kesi ya mihogo unampelekea nguruwe unategemea mini?
hamuwezi kumaliza siku bila kumtaja Lowasa, inaonyesha huko hakupo salama kama Lowasa yupo nje ya chama chenu.Mtatiro anakurupuka TAKUKURU haifanyi kazi kwa mitulinga.
Kama TAKUKURU ingekua inafanya kazi kama Mtatiro na bendera fuata upepo wa chadema wanavyotaka,basi mfalme Mbowe angekua matatani saa hizi kwa kuuza chama kwa Lowassa kwa bilioni tano
Lipumba tulishamalizana naye siku nyingi, sasa anawatumikia bwana zake.Kama hakuelewa maelezo ya Mkurugenzi wa takukuru basi huyu Mtatiro naye ni mburura. Kwanza aende akamalizane na Professor Lipumba.
Huyu kateuliwa na mwenyekiti wa ccm, unategemea atachukua hatua.? Tulishasema ccm ileile wote wahalifu hakuna mkweliBaada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, kutoa onyo kwa Mbunge Nassari kuhusu ushahidi anaoutoa kuhusu wateule wa Rais kuwanunua madiwani Arusha, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, (CUF) Julius Mtatiro ameitaka taasisi hiyo kuchukua hatua na na siyo kumtishia mbunge huyo.