Mtanzania yoyote anaweza kufungua kesi Mahakamani kupinga uchaguzi wa wabunge wa EALA na akashinda

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,694
149,920
Nilisema tangu jana katika uzi wangu mmoja niliouanzisha hapa mtandaoni kuwa hili Bunge limepoteza uhalali wa kuhoji habari za Bashite kwasababu lenyewe linavunja sheria kwa makusudi kama Bashite na hata Spika hana tofauti na Mkulu katika kusigina kanuni na sheria za nchi hii.

Naamini wengi hawakuelewa lile Bandiko langu ila kwa matokeo haya sasa watakuwa wamenielewa.

Tukirudi kwenye mada.

Naomba nisema mapema kabisa kuwa mimi sio mwanasheria ili hata hivyo nina hoja hizi kulingana na mtazamo /uelewa wangu.

Kwanini mtanzania yoyote anaweza kufungua kesi kupinga uchaguzi huu?

Mtanzania yoyote anaweza kwenda mahakamani kwa hoja kuwa yeye kama mtanzania ana maslahi na kesi hii kwasababu wote wanaochaguliwa hawaendi kuwakilisha vyama vyao bali wanakwenda kuliwakilisha Taifa na hivyo mwananchi yoyote ndani ya Taifa ana maslahi na jambo hili.

Kwanini anaweza kushinda kesi hii na hata kupelekea uchaguzi wote huu kufutwa?

Ni wazi kanuni za uchaguzi huu zilianza kuvurugwa na msimamizi wa uchaguzi ambae ni katibu wa Bunge kabla hata uchaguzi wenyewe haujaanza na ni wazi pia hata spika nae tangu awali alijipanga kutumia madaraka yake kuzima hoja zote zilizotolewa na wapinzani waliotaka kanuni zizingatiwe kabla ya uchaguzi haujaanza.

Hizi ni Sababu chache miongoni mwa nyingine zinazoweza kuishawishi mahakama kufuta uchaguzi huu kuli gana na mtazamo wangu.

Mosi,CUF kupendekeza majina 4 badala ya 4 kama kanuni zinavyotaka kwa mujibu wa maelezo ya mh.Mnyika

Mnyika alitoa hoja kuwa kanuni zinawataka CUF kupeleka majina mayatu lakini spika akapinga kwa hoja kuwa maelezo kuwa yeye ndie mwenye maamuzi na Mnyika akafafanua kuwa spika anakuwa na maamuzi pale tu ambapo kanuni ziko kimya juu ya jambo fulani.

Japo mgombea mmoja wa CUF alikuja kujitoa mwenyewe baadaae kwa hiari yake,hoja hii bado inaweza kutumika kama mfano kwa lengo la kuithibitisha Mahakama juu ya dhamira tata ya Spika katika kuendesha huu uchaguzi bila kufuata kanuni.

Hivyo basi,ni wazi mwananchi yoyoye akipata wakili ambae ni smart anaweza kutumia hoja hizi na kuishawishi mahakama kufuta uchaguzi wote huu au ule wa wabunge wa CUF.

Pili,Chama cha CUF kuteua wagombea walioidhinishwa na makundi tofauti ndani ya chama kimoja tena huku kukiwa na kesi Mahakamani juu ya upi ni uongozi hali wa chama hiki.

Hii ni hoja ambayo hata Lissu aliibua lakini sidhani kama spika na hata msimamizi wa uchaguzi waliweza kuitolea majibu ya kuridhisha na badala yake tulimsikia katibu wa Bunge akitawataja wagombea wa CUF kutoka CUF A na CUF B jambo lililotushangaza wengi

Ni wazi mwananchi yoyote akienda Mahakamani na akapata wakili makini,hoja hii ya chama kimoja kuleta wagombea kutoka makundi tofauti ndani ya chama,anaweza kuishawishi Mahakama kufutilia mbali uchaguzi huu.

Tatu,kabla hata ya uchaguzi kuanza teyari msimamizi wa uchaguzi aliutangazia umma kuwa baadhi ya vyama vilikiuka kanuni za uchaguzi na kuvitaka vyama hivyo kufanya marekebesho kabla ya kuwasilisha majna ya wagombea lakini ghafla tuaona majina yamepokelewa kama yalivyokuwa yamewasilishwa awali na vyama hivyo.

Nne,kanuni ya moja ya tatu katika uwakilisha nayo bado ina utata na mwananchi anaweza kuhoji contradiction iliyopo.

Kama kanuni ya moja ya tatu ni kwa wagombea waliochaguliwa,chama chenye nafasi mbili au moja kikipeleka majina ya watu wa jinsia moj kitakuwa kimekiuka vipi kanuni hii maana hao watakuwa sio wachaguliwa bali ni wagombea tu?

Na kama kanuni hii inatumika katika uteuzi ndani ya chama kimoja,vyama vya CHADEMA na CUF vyenye nafasi mbili na kingine nafsi moja vitapata vipi hii moja ya tatu wakati chama kimoja kina nafasi 2 na kingine nafasi moja?

Mwananchi yoyote anaweza kuiomba Nahakama itafsi kanuni hii na endapo itaonekana ilikiukwa mahala popote au haijitoshelezi basi mahakama inaweza kufuta matokeo yote ya huu uchaguzi na kuagiza kanuni zirekebishwe kwanza kabla ya kufanya uchaguzi mwingine.

Tujiandae kwa uwezekano uwa uchaguzi mwingine na mnaojipongeza nawashauri msubiri kwanza msije kuja kuadhirika hapo baadae kwa kushangilia ushindi ambao mahakama inaweza kuutamka sio halali.

Soon CHADEMA inakwenda kuvuna credits nyingine mbele ya jamii kama alivyovuna Lissu kwenye uchaguzi wa uraisi wa TLS na CCM inakwenda kuvuna aibu nyingine kama ile waliyovuna kwenye uchaguzi wa TLS

Huu ni mtazamo wangu lakini muda nao utasema/utathibitisha.
 
Nilisema tangu jana katika uzi wangu mmoja niliouanzisha hapa mtandaoni kuwa hili Bunge limepoteza uhalali wa kuhoji habari za Bashite kwasababu lenyewe linavunja sheria kwa makusudi kama Bashite na hata Spika hana tofauti na Mkulu katika kusigina kanuni na sheria za nchi hii.

Naamini wengi hawakuelewa lile Bandiko langu ila kwa matokeo haya sasa watakuwa wamenielewa.

Tukirudi kwenye mada.

Naomba nisema mapema kabisa kuwa mimi sio mwanasheria ili hata hivyo nina hoja hizi kulingana na mtazamo /uelewa wangu.

Kwanini mtanzania yoyote anaweza kufungua kesi kupinga uchaguzi huu?

Mtanzania yoyote anaweza kwenda mahakamani kwa hoja kuwa yeye kama mtanzania ana maslahi na kesi hii kwasababu wote wanaochaguliwa hawaendi kuwakilisha vyama vyao bali wanakwenda kuliwakilisha Taifa na hivyo mwananchi yoyote ndani ya Taifa ana maslahi na jambo hili.

Kwanini anaweza kushinda kesi hii na hata kupelekea uchaguzi wote huu kufutwa?

Ni wazi kanuni za uchaguzi huu zilianza kuvurugwa na msimamizi wa uchaguzi ambae ni katibu wa Bunge kabla hata uchaguzi wenyewe haujaanza na ni wazi pia hata spika nae tangu awali alijipanga kutumia madaraka yake kuzima hoja zote zilizotolewa na wapinzani waliotaka kanuni zizingatiwe kabla ya uchaguzi haujaanza.

Hizi ni Sababu chache miongoni mwa nyingine zinazoweza kuishawishi mahakama kufuta uchaguzi huu kuli gana na mtazamo wangu.

Mosi,CUF kupendekeza majina 4 badala ya 4 kama kanuni zinavyotaka kwa mujibu wa maelezo ya mh.Mnyika

Mnyika alitoa hoja kuwa kanuni zinawataka CUF kupeleka majina mayatu lakini spika akapinga kwa hoja kuwa maelezo kuwa yeye ndie mwenye maamuzi na Mnyika akafafanua kuwa spika anakuwa na maamuzi pale tu ambapo kanuni ziko kimya juu ya jambo fulani.

Japo mgombea mmoja wa CUF alikuja kujitoa mwenyewe baadaae kwa hiari yake,hoja hii bado inaweza kutumika kama mfano kwa lengo la kuithibitisha Mahakama juu ya dhamira tata ya Spika katika kuendesha huu uchaguzi bila kufuata kanuni.

Hivyo basi,ni wazi mwananchi yoyoye akipata wakili ambae ni smart anaweza kutumia hoja hizi na kuishawishi mahakama kufuta uchaguzi wote huu au ule wa wabunge wa CUF.

Pili,Chama cha CUF kuteua wagombea walioidhinishwa na makundi tofauti ndani ya chama kimoja.

Hii ni hoja ambayo hata Lissu aliibua lakini sidhani kama spika na hata msimamizi wa uchaguzi waliweza kuitolea majibu ya kuridhisha na badala yake tulimsikia katibu wa Bunge akitawataja wagombea wa CUF kutoka CUF A na CUF B jambo lililotushangaza wengi

Ni wazi mwananchi yoyote akienda Mahakamani na akapata wakili makini,hoja hii ya chama kimoja kuleta wagombea kutoka makundi tofauti ndani ya chama,anaweza kuishawishi Mahakama kufutilia mbali uchaguzi huu.

Tatu,kabla hata ya uchaguzi kuanza teyari msimamizi wa uchaguzi aliutangazia umma kuwa baadhi ya vyama vilikiuka kanuni za uchaguzi na kuvitaka vyama hivyo kufanya marekebesho kabla ya kuwasilisha majna ya wagombea lakini ghafla tuaona majina yamepokelewa kama yalivyokuwa yamewasilishwa awali na vyama hivyo.

Nne,kanuni ya moja ya tatu katika uwakilisha nayo bado ina utata na mwananchi anaweza kuhoji contradiction iliyopo.

Kama kanuni ya moja ya tatu ni kwa wagombea waliochaguliwa,chama chenye nafasi mbili au moja kikipeleka majina ya watu wa jinsia moj kitakuwa kimekiuka vipi kanuni hii maana hao watakuwa sio wachaguliwa bali ni wagombea tu?

Na kama kanuni hii inatumika katika uteuzi ndani ya chama kimoja,vyama vya CHADEMA na CUF vyenye nafasi mbili na kingine nafsi moja vitapata vipi hii moja ya tatu wakati chama kimoja kina nafasi 2 na kingine nafasi moja?

Mwananchi yoyote anaweza kuiomba Nahakama itafsi kanuni hii na endapo itaonekana ilikiukwa mahala popote au haijitoshelezi basi mahakama inaweza kufuta matokeo yote ya huu uchaguzi na kuagiza kanuni zirekebishwe kwanza kabla ya kufanya uchaguzi mwingine.

Huu ni mtazamo wangu lakini muda nao utasema/utathibitisha.

Na bado hakuna Kanuni inayosema.kupigwa kura za hapana.Imesema kila mjumbe ata"tick" majina Tisa tu.Hata hapa imekiukwa pia.
 
ni simple tu,nenda kapinge ndugu tutakuchangia gharama na lissu atakua pembeni yako akikupa support...
 
Na bado hakuna Kanuni inayosema.kupigwa kura za hapana.Imesema kila mjumbe ata"tick" majina Tisa tu.Hata hapa imekiukwa pia.
Uzuri mahakamani hakuna siasa.Hawa watu wataishia kuumbuka tu na hapa CHADEMA itavuna credits nyingi tu katika hii kesi.
 
Na bado hakuna Kanuni inayosema.kupigwa kura za hapana.Imesema kila mjumbe ata"tick" majina Tisa tu.Hata hapa imekiukwa pia.
Naiona hoja yako, nilikuwa napitia idadi ya kura kuna mgombea wa CCM ambaye amepita amepata idadi ya kura ambazo ni sawa na alizopata nadhani Masha. CCM wanaipeleka shimoni hii nchi!
 
Na bado hakuna Kanuni inayosema.kupigwa kura za hapana.Imesema kila mjumbe ata"tick" majina Tisa tu.Hata hapa imekiukwa pia.
Kwa kifupi option ya hapana haikutakiwa iwemo kwenye ballot paper. Na kama huku tick wagombea 9, kutokana na masharti ya category basi kura ni void. As bold as that.

Suala la 1/3, however, sikubaliani na Chadema. Walitakiwa watowe atleast 1/3 ya either gender. Ikiwa na maana isiyopunguwa 1/3 ya aidha mwanamke ama mwanamme. Kwa kesi yao ni 50/50 is the only option.
 
Back
Top Bottom