Mtanzania: Serikali yanuka damu

matumizi mabaya ya kalam ya uandishi na rasilimali, vyombo vya habari badala ya kuandika habari za kuelimisha, kuchochea maendeleo vinaandika chuki na hasama. jinga sana

Vipi kuhusu matumizi mabaya ya vyombo vya dola kama kuua watu,kung'oa watu kucha na meno,kubambikizia watu kesi za ugaidi n.k?
 

Ukweli unauma!
 
nachukia udhalimu, nachukia uchochezi nachukia chuki na hasama. kweli kabisa. mtz sio gazeti la kusoma

wewe hapo unachukia? mwongo mkubwa, nani hakuoni kuwa unapenda, acha hizo eti ifweeeeroooo
 

Swali ni je, serikali itaendelea kunuka damu mpaka lini?
na nini kifanyike kuisafisha serikali?
 
mbona unatoka nje ya mada?
 
Swali ni je, serikali itaendelea kunuka damu mpaka lini?
na nini kifanyike kuisafisha serikali?

Jibu:Kajiandikishe kwenye datfari la kupiga kura kama hujajiandikisha na ikifka 2015 ukiwa hai kapige kura na muhimu zaidi usisahau kulinda kura yako.
 
matumizi mabaya ya kalam ya uandishi na rasilimali, vyombo vya habari badala ya kuandika habari za kuelimisha, kuchochea maendeleo vinaandika chuki na hasama. Jinga sana

unataka kusema magazeti ya uhuru na mzalendo ya akili? Wakati huku kwetu hata kufungia vitumbua tu hatuyatumii kwani yatachafua na kutia najisi kwenye vitumbua
 
Udaku hakuna habari ya ukweli hapa

udaku upo katika magazeti ya UHURU NA MZALENDO TU,ndo maana huku kwetu hayauziki na siku hizi hata vibanda vya magazeti hawayauzi baada ya kuwa yanadoda daily
 
mtanzania damu damu na tanzania daima. full udaku na uchochezi
Inaelekea hujui tofauti ya udaku, uchochezi na ukweli. Gazeti limeandika matukio ambayo yametokea na ushahidi wa picha za waathirika zipo na baadhi ya waathirika wapo na makaburi ya waliouawa yapo utaitaje ni udaku?! Hivi ukiambiwa Mwangosi kule Iringa aliuawa kwa bomu lililolipuliwa na askari na picha zikaoneshwa, kwamba kule Arusha polisi waliua watu watatu wakati wa maandamano ya CHADEMA, kule Songea polisi waliua watu, Morogoro, Mtwara na mabomu yaliyolipuliwa mara mbili Arusha utaitaje ni udaku?! Watu wameteswa na kuuawa itakuwaje ni udaku na uchochezi?Tatizo ni kuwa wewe unamuangalia mtoa hoja badala ya hoja! Matukio yote hayo yamethibitishwa na polisi na vyombo mbali mbali vya haki utasemaje ni udaku na uchochezi? Nipo tayari kukupa darasa ili ujue maana ya udaku na uchochezi na tofauti yake na habari za matukio ya kweli. Wakati mwingine ni vizuri ukanyamaza ili watu wadhani wewe ni mjinga kuliko useme halafu uthibitishe kuwa ni mjinga!
 
udaku upo katika magazeti ya UHURU NA MZALENDO TU,ndo maana huku kwetu hayauziki na siku hizi hata vibanda vya magazeti hawayauzi baada ya kuwa yanadoda daily
Mkuu hayo magazeti bado yapo? Yanasomwa na akina nani?!
 

You are a real great thinker!
 
Do you know the power behind this newspaper?
 

Mkuu inaonekana umepanda basi la kwenda Arusha wakati wewe unaelekea Kariakoo!
 
inafahamika kwamba tz tunafuata misingi ya utawala wa sheria.Inawezekanaje watanzania wasiokuwa na hatia kuuawa au kuteswa ndani ya kisiwa cha amani bila wahusika kujulikana na kukamatwa?

hapa kuna waliojuu ya sheria na chini ya sheria,walalaheri na walalahoi
 
Mkuu nasoma sana uchangiaji wako humu JF,huwa unanishangaza sana.....
..........huyo jamaa ni kati ya Binadamu wachache sana hapa duniani wasiotumia vizuri ubongo wao. Akili zake hazina tofauti sana na Nape.
 
matumizi mabaya ya kalam ya uandishi na rasilimali, vyombo vya habari badala ya kuandika habari za kuelimisha, kuchochea maendeleo vinaandika chuki na hasama. jinga sana

Hivi unaishi karne ya ngapi!?
Yaani kufichua uovu na kupigania haki ni moja ya kazi za vyombo vya habari.
Labda kwa kuwa umezoea kuendeshwa kibabe ndio maana unaona hilo gazeti ni jinga. Serikali inatakiwa itolee majibu ya matukio yote haya.
Ila kwa kuwa kuna watu kama wewe kwenye kundi la waTZ utasikia hilo gazeti limepewa karipio na limeambiwa lijieleze kwa uchochezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…