Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 52,160
- 162,583
Gazeti la leo la Mtanzania(Mtanzania Jumatano) limebeba habari kubwa chini ya kichwa cha habari "Serikali yanuka damu".Habari hiyo katika gazeti hilo limeelezea mlolongo wa matukio ya kigaidi wanaofanyiwa raia kama kutobolewa baadhi ya viungo vya mwili,mauaji katika mikusanyiko ya kisiasa na matukio ya watu kumwagiwa tindikali huku likilaumu serikali kwa kushindwa kuwakamata na kuwachukulia hatua wahusika wa vitendo hivyo.
Mbali na kuelezea matukio hayo,gazeti hilo pia limechapisha picha za waathirika wa vitendo hivyo vya kigaidi.Picha hizo katika ukurasa wa mbele ni zile za akina Dr.Ulimboka,Absalom Kibanda na picha kadha za watu waliomwagiwa tindikali.
Katika habari hiyo, gazeti linadai kuchapisha maelezo ya watu mbalimbali ambao wametafsiri vitendo hivyo kuwa ni sawa na kusema serikali nanuka damu kwani vyombo vya dola ndio vinavyolaumiwa kutenda unyama huo na kuishangaa serikali kwa kutokuchukua hatua dhidi ya wahusika.
MY TAKE:
GAZETI LIKO SAHIHI KABISA KUCHAPISHA HABARI HIYO NA KUCHAMBUA MATUKIO HAYO.LAKINI SITASHSNGAA KUSIKIA GAZETI HILO LIKIPATA VITISHO KUTOKA SERIKALINI NA PENGINE HATA KUTUHUMIWA KWA UCHOCHEZI.
HII NDIO KAZI NZURI YA VYOMBO VYA HABARI.
BIG UP MTANZANIA JUMATANO KWANI UJUMBE UMEFIKA!