KALYANKOZILE
Member
- Apr 24, 2013
- 19
- 1
MTANZANIA MZALENDO NI YUPI?????
Karibu mwanajf mzalendo.
Kwanza kabisa natoa shukrani zangu za dhati kwa watanzania ambao kila kukicha wako kazini kuakikisha Taifa ili linasonga mbele. Pia napenda kuwakumbusha wale wanaoigiza kufanya kazi na kuishia kula jasho la wengine kuwa kazi ni msingi wa maendeleo(Mwl Nyerere) .Biblia na Msaafu iko wazi kuhusu hilo, hasiyefanya kazi hasile na kufanya hivyo ni kumkufuru Allah /Mungu.
Napenda kuzungumzia mada hii katika Nyanja mbili yaani juu ya Viongozi na Wananchi .Nakuomba wewe mtanzania unaposoma hapa weka Itikadi zako pembeni na utangulize utaifa kwanza kwani katika kujadili mada hii nisingependa uanze matusi na maneno yasiyofaa hasa pale utapoona umeguswa!!!!
VIONGOZI :
Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa na viongozi wengi lakini baadhi yao sio wasafi na wasio wasafi wanaweza kutakata iwapo watazingatia haya iwapo najua kuwa msema kweli ni mpenzi wa MUNGu na si mpenzi wa wanadamu.
Viongozi wa Tanzania tutumia muda mwingi kufikiri jinsi gani Tanzania inawezeza kuendelea na kuepukana na kuwa tegemezi tangu tupate uhuru hadi hapo mwisho wa dunia, kwani naamini kuwa mwisho wa dunia upo.Tanzania iwe na sera na sheria nzuri na zinazotelezeka ambazo zina manufaa kwa watanzania wote badala ya kupoteza muda wa kurumbana kwa mambo yasiyo na maana, baadhi kutetea maslahi binafsiri ,baadhi kufanya biashara isiyo halali hasa ya unga,baadhi kupanga jinsi ya kumwagiana TINDIKALI ,kupigana mabomu,kufunguliana kesi rukuki zisizo na manufaa kwa taifa,baadhi kushambulia,kuteka na kupiga ua watetezi wa haki,baadhi kupanga jinsi ya kuficha mali za watanzania nje ya nchi,baadhi Kupanga vikosi vya kulinda wabadhilifu na wafisili wa Nchi yetu,rushwa kila kona,kila sekunde,kila saa,kila siku,kila wiki,kila mwezi,kila mwaka na miaka,baadhi kutoa ahadi feki,wizi wa kura,kubadilika badilika mithili ya kingonya,kupenda kuitwa waheshimiwa wakati tunayoyatenda hayafanani na kiongozi anayepaswa kuitwa mh,kupenda maisha ya juu sana kana kwamba hakuna kufa! hakuna aliye wahi kuzikwa na mali au kwenda nayo mbinguni!!! ukifa unafuatwa na mazuri au mabaya uliyotenda! tumuige mwl Nyerere na Waziri Sokoine na asiyependa kuweka katika vitendo aliyoyapenda Nyerere na Sokoine hata kusifia na kunukuu maneno yao tusiwasikie!
Msiwafanye watanzania wajutie kupata uhuru na kusema bora tungeendelea kuongozwa na wazungu (Mkoloni) maana baadhi ya viongozi, wananyonya zaidi ya mkoloni !!! ambaye hakubaliani na mimi ajiulize walau kidogo kwa kuangalia suala hili la ununuzi wa rada kwanini pesa ya ufisadi katika ununuzi wa rada inaitwa chenji ya rada! n.k
Pia nguvu zote zinatumika wakati wa kampaini za uchaguzi kama kutembelea wananchi usiku na mchana,kuonesha kuwa mnatupenda! jamani hatukataza jitihada hizo kuendelea katika kuleta maendeleo kwenye jamii zetu.
Baadhi ya wawakilishi wetu tunaona wanavyokwepa bungeni na kujiendea kwenye mambo yao binafsi badala ya kututetea sisi tuliowachagua.Kuhusu hilo huwezi kuniambia kuwa ni dharura, lini robo tatu ,robo ya wabunge mkawa na dharura kwa wakati mmoja.
Na wengine tunawaona wanavyoshangilia tu pale sera mbovu za kutubana sinapojadiliwa mfano mzuri ni katika kupandisha kodi za kutuma na kupokea pesa kupitia simu ambazo kwa asilimia kubwa ndizo tunazozitumia vijijini kwani hakuna benki .Hili limefanyika kwa kuwapandishia wenye makampuni ya simu na wao wakaamua kutubebesha sisi na mbaya zaidi nashangaa! ambao kwa vinywa vyao wanakazana kutubebesha pia kodi laini za simu ambayo kwetu sisi tunaona kama ni sawa na kututwika gunia la misumari bila ha kuweka kata! Pia ni walewale walioshangia wakati wa kuhusu mafao yetu tunayoweka kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii! Na ukifika wakati wa uchaguzi utawaona wanyenyekevu na wengine wakidiliki kuwapigia magoti wapiga kura wao!
Baadhi ya viongozi mkimchagua anahama na kwenda kuishi Dar es salaam! Unakuwa na kero yako unakwenda kwenye ofisi zao huwaoni utamkuta karani na kuanza kukuuliza wewe ni kada wa chama gani kumbe hawajui kuwa baadhi yetu tunachagua mtu kulingana na utendaji wake na si chama tena .
Viongozi wamekuwa wa kuonekana kwenye msimu wa kampeini (Msimu wa kulima )na wakati wa mavuno wanajificha bali misiba wamekuwa hawakosi na si kwamba wanakuwa wameguswa na mziba ila ni ili watu wawaone kuwa ni wema na si kwenye kuleta maendeleo mtanzania.
Viongozi watu sina shaka kama mtayarekebisha hayo mtaongoza vizuri ,mtapendwa na wapiga kura wenu hapatakuwepo na kuvunjiwa vioo vya magari yenu na wananchi kwa kushindwa kuheshimu mkataba mnaowekeana na wananchi kuwa wawachague muwawakilishe na pia ndipo mtabarikiwa japo sina hakika kama ni wote tunaoamini uwepo wa Mungu!
WANANCHI
Ndugu zangu watanzania kuweni waangalifu na viongozi wasiojali maslahi ya Tanzania, epukeni kuwa na upendo wa mshumaa wa kuchagua mtu akuwakilishe wakati unajua fika kuwa si mzalendo,ni mwizi na jambazi,tuache kulalamika,kushadadia mambo yasiyo na maana,kutumiwa na baadhi ya viongozi, tuache kupokea hongo (Zawadi) za wakati wa uchaguzi au zipokee lakini msiwachague bali kufanye kazi kwa bidii na tuchagua viongozi mema (fungu lililo jema) ambao tutashilikiana nao kuleta maendeleo ya Tanzania.
Mwisho namalizia kwa kusema maendeleo ya kweli yanalendwa na wananchi wenye