Mtangazaji Ndimbo wa Times FM acha chuki na klabu ya Simba?

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,252
Nimekuwa nakifuatilia sana kipindi cha michezo kinachorushwa Na Redio ya Times FM Na kutangazwa Mtangazaji Ndimbo.

Mtangazaji huyu aliwahi kuwa Afisa Habari wa Klabu ya Simba Na baadae alifukuzwa. Mtangazaji huyu toka amefukuzwa Klabu ya Simba basi amekuwa anaiponda sana klabu hiyo Na viongozi wake.

Amekuwa anajitahidi kutafuta matokeo mabaya ya Klabu ya simba Na kuyatangaza Kwa nguvu zote hata kama habari yenyewe haina uzito ili mradi akidhi kiu yake hali ambayo inaonyesha chuki aliyonayo dhidi ya hiyo klabu.

Tunapenda kumshauri Bw.Ndimbo klabu ya simba ipo Na itaendelea kuwepo ila yeye Ndimbo kuna siku atakosa kipaza sauti Na hata sikika. Iache Simba Yetu tangaza Kwa kufuata maadili acha chuki binafsi dhidi ya klabu ya simba Na viongozi wake.
 
Hawa watangazaji wa michezo wa redio zetu wana matatizo sana.
 
Mbona hujamsema na yule mwenye ki-blog chake kinachodhaminiwa na Zakaria Hans Poppe ambae yeye kila siku ni kuiponda Yanga hata ifanye vizuri vipi!!!! Sijui anaitwa Mahamoud Zubeiry??????.
 
Mi si msikilaji wa hiyo radio na hiko kipindi ila ilitokea Siku Kama mbili hivi nikasikiliza nikashangaa kuanzia SAA mbili mpaka SAA Tatu kipindi kinazungumzia negative za simba tu mpaka mwisho wa kipindi huku vitu vingine vya kimichezo havitangazwi.
 
Huyo ni shabiki na siyo mtangazaji.Tz tuna marefa mashabiki,chama cha kishabiki yaani kila kitu tunataka kushabikia tuuuuuu!
 
Back
Top Bottom