Mvumbo
JF-Expert Member
- Aug 20, 2015
- 3,483
- 12,091
Tarehe kumi na tatu ya mwezi huu nilinunua kifurushi cha mb cha shilingi elfu tano kupitia account yangu ya Tigo pesa, lakini hakijafika kifurushi na pesa yangu mmechukua.
Nikaona rabda kitakuja ni mambo ya mtandao tu hivyo ninunue kingine kidogo cha 500 lakini hali ikawa ile ile hata baada ya kusubiri mpaka kesho yake.
Nimewasiliana na ninyi karibu kila leo na mmekiri nimefanya muamala huo na kusema hilo si tatizo langu pekee kwani limewakumba wengi na mnalishughulikia.
Cha kushangaza ni siku tisa sasa hamjanirudishia haki yangu wala kunipa taarifa yeyote ya kinachoendelea mpo kimya! Mbona mkimdai mteja wenu mnamtumia sms kila muda, hili ugumu upo wapi kutoa taarifa?
Tafadhali sana nataka haki yangu au mnipe maelezo ya kuridhisha sio uongo uongo wa wahudumu wenu ambao kila ukiongea nao wanasema tatizo litaisha muda si mrefu halafu kimyaaa!!!