Mtandao wa majangiri waitisha serikali....

Mtandao wa majangiri waitisha serikali....

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
[h=3]MTANDAO WA MAJANGIRI WAITISHA SERIKALI....[/h]



SERIKALI imesema mtandao wa majangili wanaoua tembo

mkubwa wenye watu walio na uwezo kifedha ambapo wapo ndani

na nje ya nchi .Siri hiyo ilifichuliwa Dar es Salaam jana na Waziri

wa Mali Asili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, wakati

akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii
.Alisema tayari Serikali ina majina ya mtandao unaojihusisha na biashara ya ujangili wa meno ya tembo na baadhi yao wapo pia wafanyabiashara wakubwa waliopo ndani na nje ya nchi."Tayari majina tunayo ya mtandao wa watu wanaojishughulisha na ujangili wa meno ya tembo huu ni mkubwa ambao una pesa nyingi, hauna tofauti na ule wa dawa za kulevya,"alisema
Alisema sio kwamba wameshindwa kufanya kazi bali wanaendelea

kupata taarifa na wameandaa operesheni hai itakayosaka wale

wote ambao wanahusika na ujangili huo.Aliongeza kuwa

wanaendelea kufuatilia nchi inayonunua meno hayo ambapo

nchi zilizopo Bara la Asia ni miongoni mwa zinazo husikana

biashara hiyo.Ali sema siorahisi ku shinda vita hiyo kwa

kutumia vyombo vya habari.

"Mnajua hii ni vita kubwa na ni waambie kuwa vita hii huwezi

kushinda kwa kutumia vyombo vya habari, hivyo Watanzania

kuwe ni na amani na tunajitahidi kuhakikisha tunamaliza tatizo

hili,"alisema.Katika hatua nyingine,alisema

mfumo wademokrasia uliopo unachangia kurudisha nyuma

jitihada mbalimbali zinazofanywa, kwani watu wakikamatwa na

kupelekwa mahakamani kesho yake wanaonekana mtaani.

Alisema wanaobainika kufanya biashara hiyo ya ujangili hata

Polisi wamo na wengine wameshafukuzwa kazi na wengine

kusimamishwa, hivyo hizo zote ni jitihada za Wizara

yake.Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo John Lembei alisema

kuwa kamati yake imeiomba Serikali kuondoa kodi ya asilimia

tatu ambayo ilipitishwa na bunge kwa ajili ya mfuko wa

maendeleo ya utalii na asilimia kumi ambayo yalikuwa

yanawasilishwa Serikalini kwani inachangia kuondoa huduma za

jamii zilizokuwa zikitolewa kwenye jamii inayozunguka hifadhi

hizo.
Alisema kamati imeomba serikali kama kweli wanataka kuendeleza sekta ya utalii basi kodi

hiyo ifutwe vinginevyo hifadhi hazitakuwa salama na ujangili utaongezeka kwa kiasi

kikubwa."Hifadhi hizi za TANAPA na ngorongoro ilikuwa miradi ya kusaidia jamii

inayowazunguka kwa kuwajengea shule, hospitali, maji, pamoja na huduma zinginezo hivyo

kutokana na bunge kupitisha kodi hiyo wameondoa huduma hizo,"alisema Lembei.



chanzo.Alvin Collections: MTANDAO WA MAJANGIRI WAITISHA SERIKALI....
 
Serikali ikili wazi imetekwa na Mafisadi,majangari na wauza dawa za kulevya.

tunahitaji uongozi madhubuti kupunguza haya Majanga na huo uongozi haupo ndani ya ccm.!!
 
Sasa anatuwekea matarajio ya kufanya operation? Kwa maana nyingine Ana wa alert wahusika? Angefanya hiyo operation nasi tukaona matokeo. This is utter.....
 
Ni ujinga huu! tuambieni mmewakamata leo mnatuambia mna majina yanatusaidia nn hayo majina pia wakati mwingine haiko na haja ya kupost mambo ambayo hayana maana kama haya
 
Back
Top Bottom