Mtambue balozi katika Diplomasia ya Kimataifa

Mtambue balozi katika Diplomasia ya Kimataifa

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
339
Reaction score
677
Na Elius Ndabila
+255768239284


Wiki iliyopita niliandika kidogo juu Elimu ya Uhusiano wa Kimataifa/DEPLOMATIC RELATIONS .Nilikuwa nimejikita zaidi kwenye kuangazia mambo ya diplomasia ya Kiuchumi. Nilifafanua zaidi juu ya mtu anayeitwa Consular ambaye ndiye anahusika sana na Diplomasia ya kiuchumi kwenye mambo ya mahusiano ya Kimataifa.

Nimepata maombi mengi kutoka kwa wasomaji wangu yanayouliza kunatofauti gani kati ya Balozi(AMBASSADOR) na CONSULAR? Maswali haya yamenipa wasaa wa kutoa majibu ijapo kwa uchache. Leo nitazungumza kinagaubaga juu ya Balozi ni nani, anavyopatikana, kazi zake na anavyoweza kufukuzwa kazi. Fuatana nami kwenye makala hii.

Balozi ni mwakilishi rasmi wa serikali ya nchi yake katika nchi nyingine. Anatumwa huko na wizara ya mambo ya nje akitazamiwa kama mwakilishi wa mkuu wa nchi inayomtuma. Kwa lugha ya kidiplosia kunakuwa na Sending state and Receiving State.

Nchi inayomtuma Balozi kwenda nchi nyingine ni Sending State lakini nchi inayompokea huyo Balozi ni Receiving State, hii ni kwa mjibu wa mkataba wa Vienna wa mwaka 1961. Katika Nyanja ya uteuzi wa Mabalozi kuna mabalozi waaina mbili, mabalozi wanaoteuliwa kwa utashi wa kisiasa na pili wanaoteuliwa kutokana na weledi wao.

Kuna balozi za aina mbili, balozi za kudumu na balozi za nchi na nchi. Balozi za kudumu ni zile zinazofunguliwa na nchi kwenda shirika au taasisi ya kimataifa kwa mfano ubalozi wa Tanzania Geneva unahudumu mahusiano ya Tanzania na Ofisi za Umoja wa Mataifa sambamba na kuhudumu Vienna, Austria. Ubalozi wa Tanzania New York unahudumu katika mahusiano ya Tanzania na Umoja wa Mataifa, lakini pia unahudumu nchi za Jamaica, Trinidad and Tobago, Barbados na Guyana.

Mapendekezo ya kumteua mtu kuwa Balozi hufanywa kwa siri kubwa. Baada ya nchi kupendekeza jina la balozi hutuma jina hilo kwenye nchi wanayotaka huyo Balozi aende jina likishafika nchi receiving state inaweza kumkubali au kumkataa. Kwa lugha ya kidiplomasia balozi anapokuwa amekataliwa wanaita Persona non grata.

Balozi anapokuwa persona non grata nchi inaweza kuwajibu nchi waliopeleka ombi la jina la balozi kuwa hatumtaki au wakamua kukaa kimya kuonyesha kuwa hawamtaki. Mwaka 1997 Brad Pitt alikuwa persona non grata kwenda China, Libya walishawahi kumbwa na hili, George Kenedy wa USA mwaka 1952 alimkata Balozi wa Soviet nion kwa ujumla orodha ni ndefu. Ukisoma the Treaty of Lausane in 1923 inaweza kukusaidia pia.

Kuna balozi za nchi na nchi ambazo hufunguliwa kufuatia makubaliano baina ya pende mbili (mutual consent) kama iliyoainishwa kwenye ibara ya pili ya VCDR 1961. Ufunguaji huu wa balozi kwa mujibu wa ibara hii unahusu pia balozi za mashirika au taasisi za kimataifa kama vile UN, UNDP, FAO, WHO, ILO n.k Mabalozi wa mashirika na taasisi za kimataifa wanaotumwa na taasisi hizo ama mashirika hayo ndani ya nchi zinazowapokea huitwa Wawakilishi Wakazi.

Mfano wa vigezo hivyo huwa ni uzalendo, uelewa mzuri wa Balozi juu ya nchi anayoteuliwa, Utamaduni wa huko n.k

Balozi hufanya kazi kwa mujibu wa Mkataba wa Vienna wa Mwaka 1961 unaohusu Mahusiano ya Kidiplomasia. Mkataba huu umeainisha Upendeleo na Kinga anazopata Balozi (Privileges and Immunities) anapokuwa katika nchi aliyopangiwa kufanya kazi zilizoanishwa katika Ibara ya Tatu (Article 3) ya Mkataba huo.

Nikwambie kitu kimoja, Balozi anakinga /immunities kubwa sawa na Rais hii ni kwa kuwa Balozi awapo kwenye nchi Fulani basi basi inahesabiwa kama ni nchi nyingine. Yaani ofisi na makazi ya balozi inakuwa kama nchi yenye territory, Population, sovereighty etc hivyo inajitawala. Hata premises/makazi za mabalozi haziruhusiwi kusogelea. Hurusiwi hata kugusa begi la Balozi wala nguo zake. Ukisoma kuanzia Ibara ya 22 ya VCDR imeeleza vizuri.

Kwa ufupi Ibara ya 22 (Article 22): Ubalozi hauwezi kuingiliwa bila ya ridhaa yake. Kwa mujibu wa Vienna Convention on Diplomatic Relations of 1961 Ubalozi unachukuliwa kama nchi ndani ya nchi. Mfano Ubalozi wa China ni sawa na China ndani ya Tanzania. Hata wakati wa vita makazi ya balozi hayapaswi kuguswa na mtu yeyote.

Ibara ya 24 (Article 24): Kumbukumbu na nyaraka za Ubalozi haziwezi kukaguliwa. Ni siri ya nchi ya hiyo iliyomtuma Balozi. Hii inahusisha mawasiliano mengine pia kama Simu, e-mail n.k Ibara ya 27 (Article 27): Begi la Kidiplomasia/Balozi haliwezi kukaguliwa. Mfano briefcase na pochi. Ndiyo maana viwanja vya ndege vina milango imeandikwa "Diplomats Only".

Ibara ya 29 (Article 29): Mabalozi wana kinga dhidi ya kukamatwa na kuwekwa kizuizini katika nchi wanapofanyia kazi. Ibara ya 30 (Article 30): Makazi binafsi (Nyumba anayoishi akiwa katika nchi anayofanyia kazi) ya mwanadiplomasia/balozi hayawezi kuingiliwa.

Ibara ya 31 (Article 31): Wanadiplomasia/ mabalozi wana kinga dhidi ya mashitaka ya ndani ya nchi isipokuwa kwa mambo yasiyohusu Ubalozi (Mambo yake binafsi kama real estate na biashara).Ibara ya 32 (Article 32): Kinga ya Balozi inaweza kuondolewa na nchi iliyomtuma tu na si nchi ambayo balozi huyo anafanya kazi yake.

Kwa maana fupi ni kuwa Balozi anaweza kuwajibishwa na nchi iliyomtuma (Sending State), mfano Balozi wetu akiharibu huko nje Rais Magufuli ndiye atakayemtumbua. Ninanukuu ibara ya 41(1) Without prejudice to their privileges and immunities, it is the duty of all persons enjoying such privileges and immunities to respect the laws and regulations of the receiving state. They also have a duty not to interfere internal affairs of the state.

Kwa kawaida anaongoza ofisi ya ubalozi ambako anasaidiwa na maafisa wengine wanaotumwa katika utaratibu wa diplomasia. Ifahamike wazi kuwa uteuzi wa mabalozi hufanyika kwa siri mno kufuatia mawasiliano baina ya Marais wa nchi mbili au kadhaa. Wizara ya Mambo ya Nje huweza kupendekeza jina kwa Rais, lakini pia Rais anaweza kumteua yeyote kutokana na vigezo atavyoona vina faa kwa mtu anayetaka kumteua.

Pamoja na kuwa Mabalozi wanayomajukumu makubwa huko wanakokuwa wanaziwakilisha nchi zao, lakini kwa mjibu wa sheria za kimataifa ambazo ndiyo msingi wa mipaka ya Balozi, zimeainisha majukumu matano tu ya Balozi.
Kwa mujibu wa ibara ya tatu ya Vienna Convention on Diplomatic Relations (VCDR 01961 kazi za balozi zimeainishwa kama ifuatavyo:

(a) Kuiwakilisha nchi iliyomtuma (Sending State) ndani ya nchi husika itakayompokea (Receiving State).Kipengele hiki pia kinahusisha uwakilishi wa taasisi au mashirika ya kimataifa ndani ya nchi husika.

(b) Kulinda maslahi ya nchi (dola) iliyomtuma ndani ya nchi iliyompokea pamoja na ya raia wake, bila ya kuathiri mipaka aliyowekewa kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Hivyo Balozi anawajibu mkubwa katika kulinda maslahi lakini bila kuvunja miongozo mbalimbali ya kisheria. Kifungu hiki pia kinahusisha uwakilishi wa taasisi na mashirika ya kimataifa kama EU.

(c) Kujadiliana (negotiating) na serikali ya nchi iliyompokea (katika mambo mbalimbali yenye maslahi baina yao). Kunapotokea jambo lolote basi Balozi ana wajibu mkubwa kuka meza moja na taifa hilo kuangalia namna ya kuondoa changamoto hizo.Kifungu hiki ndicho kinawapa uwezo mabalozi kuingia na kusaini mikataba mbalimbali kwa niaba ya Marais wa nchi husika ama taasisi za nchi husika lakini bada ya mashauriano na nchi yake..

(d) Kuenenda na taratibu zote za kisheria katika kufuatilia yanayojitokeza ndani ya nchi iliyompokea na kutolea taarifa yale yanayojiri kwa nchi iliyomtuma. Balozi awajibu wa kutoa tarifa kwa nchi yake kama kuna jambo aliona kuwa ni lazima lifahamike. Na si kila jambo atalisema hasa ambalo si wajibu wake kulisemea.

Kifungu hiki pia kinahusisha hadi mashirika na taasisi za kimataifa kama EU.Kifungu hiki kinamaanisha kuwa mabalozi au wawakilishi hawa ndiyo macho na masikio ya marais, wakuu wa serikali, taasisi na mashirika ya kimataifa yaliyowateua kwenda katika nchi husika.

(e) Kuendeleza mahusiano ya kirafiki kati ya nchi iliyomtuma (Sending State) na nchi iliyompokea (Receiving State) sambamba na kuendeleza mahusiano ya kiuchumi, kiutamaduni na kisayansi

Balozi anaweza kuachana na kazi yake ya Ubalozi kwa muda wake a utumishi kuisha, kwa kutenguliwa au receiving state kumumfukuza. Na kwa mjibu wa sheria ukikoma kuwa Balozi hapo hapo immunity zako zinakuwa waved/ondolewa kinga.

Nihitimishe kwa kusema Balozi ni mkubwa kuliko Consular, ili Consular aweze kufanya majukumu yake vizuri anahitaji Balozi anayemsimamia vizuri. Uchumi wa dunia ya leo unategemea zaidi diplomasia ya kiuchumi na si vinginevyo. Balozi zinapaswa zisilale wao ndio nguzo ya uchumi hasa kwa fedha za kigeni. Mabalozi wakitimiza vizuri kazi zao Tanzania utalii halitakuwa tatizo na pia nchi itapata wawekezaji wengi ka kuwa kila kitu kipo.
 
Safi sana mkuu, nilitaka kujua faida za kustaafu na kuenderea kuitwa barozi na madhara ya kuvuliwa hadhi ya ubarozi namakosa yanayoweza kuperekea kuvuliwa ubarozi
 
Mada nzuri, lakini huwa mada zenye subsatance ni ngumu kupata wachangiaji. Kwa bahati mbaya wengi miongoni mwetu hawataki kufikiri sana maana kufikiri kunachosha.
 
Mada nzuri, lakini huwa mada zenye subsatance ni ngumu kupata wachangiaji. Kwa bahati mbaya wengi miongoni mwetu hawataki kufikiri sana maana kufikiri kunachosha.
Watu wanapenda hoja nyepesi nyepesi.Ni kweli hizi hazina wasomaji wengi mkuu.
 
Hii mada ni kwa consular na mabalozi kwa nchi tajiri tu au hata consular na balozi wetu wa Burundi na Msumbiji?!
 
Hizo nchi wanakuja kuwekeza nini kwetu?! Au ndio kununua chakula?!
Tunavitu vingi vya kununua kwao na wao kunnua kwetu. Tunayobandari ambayo tunaweza kutumia kama kitega uchumi, tuna hifadhi zawanyama, tunchakula, tunawasomi wa kiswahili nk
 
Tunavitu vingi vya kununua kwao na wao kunnua kwetu. Tunayobandari ambayo tunaweza kutumia kama kitega uchumi, tuna hifadhi zawanyama, tunchakula, tunawasomi wa kiswahili nk
Hifadhi za wanyama nayo bidhaa huko kwao, unamaanisha watalii watoke msumbiji, Burundi na malawi?!
Kiswahili nacho ni bidhaa au walimu wa kiswahili?! Kuweni serious basi.
Ukweli hao ma consular na mabalozi tunaowapeleka nchi masikini ni kupeana ajira na kupeana kisiasa na kirafiki.
Na wale tunaowapeleka nchi tajiri ni professional OMBA OMBA hakuna cha mahusiano wala uwekezaji.
Muwekezaji ahitaji balozi kuja kuwekeza nchini.
 
13 August 2021
Zanzibar

Mahusiano na Nchi za Nje hasa Diplomasia ya Biashara yatizamwa kwa undani

Karafuu na diplomasia, pia mafungamano ya kale katika ya Zanzibar , Oman, USA, UK n.k na jinsi ilivyopelekea Zanzibar kujulikana kuliko Tanzania. Nini kifanyike ktk diplomasia ya kiuchumi na biashara.


Mwanadiplomasia mkongwe Muhammad Yusuf msomi wa vyuo tajwa vya Strasbourg cha nchini France, degree BA international and comparative law of human rights na American University Washington DC master's in International relations.

Kafanya kazi Kinshasa DR Congo na Naibu balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa / UN New York ktk balozi za Tanzania na baadaye akawa muajiriwa wa Umoja wa Mataifa kitengo cha UN Joint Inspection Unit Geneva Switzerland na sasa ni mkurugenzi wa ZIRPP Zanzibar
Source : Zanzibar Kamili TV

Full personal history:
Ambassador Muhammad Yusuf
M.A. (Degree) in International Affairs, American University, Washington D.C. USA. (1981);
B.A. (Diploma) in International and Comparative Law of Human Rights, International Institute of Human Rights, University of Strasbourg, Strasbourg, France (1978);
Diploma in French Language, Centre Audio Visuel des Langues Modernes (CAVILAM), Vichy, France (1976);
Diploma in Regional Integration and Development; International Institute of Public Administration, Paris, France (1993);

Study Programmes/Seminars

Seminar on “International Political Relations”, International Institute of Public Administration, Paris, France (1977);
Short Course on “Macro-Economic Analysis of Structural Adjustment Programme”, sponsored by the World Bank in collaboration with the Ministry of Finance of Mauritius, Port Louis, Mauritius (1992);
Short Course on “Civil Service Reform and Development”, sponsored by Japan International Cooperation Agency (JICA) Tokyo, Japan (1996);
Seminar on “Peace-keeping, Peace-making and Peace-building”, sponsored by International Peace Academy (IPA), Vienna, Austria (1998);
Workshop on “Art of Public Speaking”, organized by the United Nations Institute for Training and Research (UNITAR) and the Seton Hall University School of Diplomacy and International Relations, New York (November 2000);
Policy Forum on “Zanzibar’s Political Crisis: The Quest for a Lasting Solution”, organized by International Peace Academy, New York, (March 2001);
Workshop by the United Nations Institute for Training and Research (UNITAR) on “Financial Management, Negotiation and the Bretton Woods Institutions”, New York, (April 2001);
Policy Forum on “The Path to Peace in the Democratic Republic of the Congo”, organized by International Peace Academy, New York (April 2001);
Policy Forum on “The G-8 and the United Nations Security Council: Who’s in Charge?” sponsored by International Peace Academy, New York, (April 2001);
Policy Forum on “Smart Sanctions in Iraq, Options for UN Policy”, organized by International Peace Academy, New York (April 2001);
Management Development Foundation Course on the “Impact of Evaluation, Challenges and Approach”; Geneva (February 2005);

Professional Experience

Executive Director
Zanzibar Institute for Research and Public Policy (April 2009 to date);

Inspector
Joint Inspection Unit of the United Nations system (January 2003 to December 2007);

Deputy Permanent Representative
Permanent Mission of the United Republic of Tanzania to the United Nations (August 2000-November 2002);

In charge of all Security Council matters in relation to African issues, in particular the Democratic Republic of the Congo, Angola, Sierra Leone, Ethiopia/Eritrea and the Great Lakes. Followed closely Security Council debates and consultations on conflicts in Burundi, the Democratic Republic of the Congo, Angola, Sierra Leone, Ethiopia/Eritrea, and reported to my government, as well as advising on the policy direction and courses of action. Recorded various meetings between the Permanent Representative and the Secretary-General on various issues of interest to Africa in general and Tanzania in particular;

Minister Counsellor
Permanent Mission of the United Republic of Tanzania to the United Nations (1997 – 2000).

In-charge of all the Fifth Committee issues, namely Administrative and Budgetary Questions of the United Nations.

Coordinator and Chairman of the Group of 77 and China of the Fifth Committee (1997/1998)

Actively participated in and contributed to the negotiations with respect to 1996-1997, 1998-1999, 2000-2001 and 2002-2003 proposed programme budgets; scale of assessments for the apportionment of the expenses of the United Nations for 1998/2000 and 2001/2003 periods; actively participated in various meetings of the Committee for Programme and Coordination (CPC) both as an observer and active member.

Director, Chief Liaison Officer of the Zanzibar Government (1990-1996)

In-charge of coordinating all matters related to development and investment issues between the Government of Zanzibar and donor countries/aid and international agencies such as UNDP, the IMF and the World Bank. Actively participated in various Annual Consultation Meetings between Tanzania and donor countries; such as the Nordics, Japan, Italy and France.

First Secretary, Tanzania Embassy, Kinshasa, Zaire (1985-1990)

In-charge of all political, economic and consular matters; namely policy initiatives, preparing weekly and monthly reports on political and economic developments: covering and preparing meetings of officials of the two countries in the context of good-neighbourliness: issuance of visas and passports. Also acted as Chief public relations officer;

Second Secretary and Personal Assistant to the Minister for Foreign Affairs, Salim Ahmed Salim, (1982-1984);

Managing the Minister’s daily programme of work, appointments, recording his discussions with various officials; advising him on his numerous diplomatic initiatives and policy formulations; preparing country briefs, and writing speeches;

Third Secretary, Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam, Tanzania (1981-1982);

Desk Officer for the Nordic countries that included, among other things, preparing country briefs, initiating policies, writing speeches for Ministers and Prime Ministers when travelling abroad or receiving their counterparts on official visits to Tanzania.

Assistant Protocol Officer, Department of Foreign Affairs and International Cooperation, Zanzibar (1978-1983);

Assisting the Chief of Protocol in organizing State ceremonies and government hospitality; granting exemptions for customs taxes and other dues to diplomats accredited to Tanzania as well as the issuance of diplomatic identity cards.

Meetings attended

Member of the Tanzania delegation to the 51st Session of the United Nations General Assembly, New York. (1996);
Member of the Tanzania delegation to the 52nd Session of the United Nations General Assembly, New York. (1997);
Member of the Tanzania delegation to the 53rd Session of the United Nations General Assembly, New York, (1998);
Member of the Tanzania delegation to the 54th Session of the United Nations General Assembly, New York, (1999);
Member of the Tanzania delegation to the 55th Session of the United Nations General Assembly, New York, (2000);
Member of the Tanzania delegation to the 56th Session of the United Nations General Assembly. New York, (2001);
Member of the Tanzania delegation to the COMESA/PTA Meetings, Lilongwe, Malawi (1992); these included meetings of government officials, Ministerial and the Summit;
Member of The Tanzania delegation to the Annual SADC meetings in Namibia, Botswana, Swaziland, Malawi, Zimbabwe and South Africa (1992-1996 respectively); the meetings included Sector Coordinators, Group of Experts/Officials, Council of Ministers, and Summits (meetings of Heads of State of the SADC Member States);
Member of the Tanzania delegation to the 27th Annual Meeting of the African Development Bank (ADB), Abidjan, Côte d’Ivoire (1991);
Member of the Tanzania delegation to the 13th Ministerial Meeting of Pan African Telecommunications Union (PATU), Kinshasa, Zaire (1989);
Member of the Tanzania delegation to the African Experts Meeting on Cartography, Kinshasa, Zaire (1988);
Member of the Tanzania delegation to the 12th Ministerial Meeting of Pan African Telecommunications Union (PATU), Kinshasa, Zaire (1987);
Member of the Tanzania delegation to the 19th session of the Organization of African Unity Heads of State and Governments, Addis Ababa, Ethiopia (1983);
Member of the Tanzania delegation to the 40th Ordinary Session of the Organization of African Unity (OAU) Liberation Committee, Arusha, Tanzania (1983);
Member of the Tanzania delegation to the Organization of African Unity Contact Committee Meeting on Chad, Addis Ababa, Ethiopia (1982);

Publications

Deborah M. Wynes and Muhammad Yussuf, “Common Services at the United Nations Office in Nairobi (UNON)”; Note of the Joint Inspection Unit, Geneva 2008;
Muhammad Yussuf, “Review of the Progress Made by the United Nations System Organizations in Achieving the MDG aimed at Combating HIV/AIDS”; Report of the Joint Inspection Unit, Geneva 2007;
Muhammad Yussuf, Juan Luis Larrabure and Cihan Terzi, “Voluntary Contributions in United Nations System Organizations: Impact on Programme Delivery and Resource Mobilization Strategies”. Report of the Joint Inspection Unit, Geneva 2007;
Even Fontaine-Ortiz and Muhammad Yussuf; “Review of the Implementation of the Result-Based Management in the Pan American Health Organization (PAHO)”. Note of the Joint Inspection Unit, Geneva 2005;
Muhammad Yussuf and Guangting Tang; “Further Measures to Strengthen United Nations System Support to NEPAD”. Report of the Joint Inspection Unit, Geneva 2005;
Muhammad Yussuf, “Procurement Practices within the United Nations System”. Report of the Joint Inspection Unit, Geneva 2004;
Victor Vislykh, Deborah M. Wynes and Muhammad Yussuf, “Review of the United Nations Budgetary Process”. Report of the Joint Inspection Unit, Geneva 2003;
Muhammad Yussuf, “The United Nations is Working”; A Paper published in Philosophy-Humanities Magazine, Volume 24, No.1, Farmingdale State University, New York 2003;
Muhammad Yussuf, “The Challenges of Democracy and Human Rights in Africa”; A Paper presented to the Students at East Strousburg University (ESU), Pennsylvania, June 2009.

Computer Skills
Proficient in the use of:
o Microsoft: Word, Access, Excel, Outlook, PowerPoint.
o Prentice Hall: Statistical Package for the Social Sciences (SPSS).
Basic knowledge of GIS software: Arc View and Arc info.

Languages

Mother Tongue: Kiswahili;
Working Knowledge: English & French
 
Mkubwa hebu tusaidie Tanzania foreign policy na utekelezaji wake , Je tumefanikiwa na changamoto ni zipi?

Kuna kipindi wakati wa Kikwete Salah wa GSM alichaguliwa kuwa Consular wa Tanzania Guangzouh nafikiri unadhani uteuzi ule ulikidhi viwango vya Foreign and Diplomatic affairs ?

Kuna habari ilizunguka mtandaoni Allegedly balozi wa Tanzania Rwanda miaka hiyo ya JK alihusika na uuzwaji wa silaha kwa waasi wa DRC hili kidiplomasia linatatuliwaje? Steps za kuchukua ukiachia kumpumzisha mhusika na kazi??
 
Back
Top Bottom