Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 731
- 659
Ujenzi wa mtambo wa kisasa wa kuchakata maji taka, unaotajwa kuwa miongoni mwa mitambo mikubwa ya aina hiyo katika Ukanda wa Afrika Mashariki, umefikia asilimia 99. Pamoja na vituo vya kusukuma maji, mradi huo unaelekea kukamilika huku kazi ya kuwaunganisha wananchi kwenye mfumo wa huduma ikiendelea, hatua inayotarajiwa kuimarisha usafi wa mazingira na afya ya jamii.