Mtaji wa million kumi, wazo la biashara

hemedi miraji

Member
Feb 16, 2010
46
10
Jaman naomba ushaur me nipo mkoa wa Kilimanjaro , Nina mtaji wa milion kumi, nan mwenye wazo LA biashara itakayo nilipa.
NB. Pesa ya kula na kujikimu nategemea hapo hapo.
 
Aisee njoo nayo huku baadhi tulime vitunguu. Nyingine 30% utanunua kibajaj kikuletee hiyo hela ya kula daily!
Otherwise peleka utt au kanunue dhamana za serikali walau 70% ya huo mpunga!
Usipokuwa makini walah inaisha fasta make mbesa ndogo sana hiyo ikiwa hukuwa na wazo la mradi kabla hujaipata.
 
Nami ninawazo la biashara na machine sio ya kusagia unga niyahiyo plan ya hiyo biashara tatizo mtaji.kama upon tayari ni pm tuyajenge
 
Habari wakuuu

Naimani humu kuna figher kibao wa fursa mbalimbali

Leo nawaletea fursa ya kutengeneza pesa kupitia mitandao ya kijamii.


Ni kupitia kuwa na simple blog tu ambayo utaweka habari au chochote unachopenda then hiyo post yako utaisambaza kwenye mitandao ya kijamii kama facebook.... pale watazamaji watakavyoingia utajipatia pesa

Kampuni ya google adsense ndio itakayokulipa kutokana na matangazo yao kuonekana kwenye blog yako...

Kama unafahamu vizuri mambo ya komputa utaanza fursa hii bila kutumia hata sh mia kwani utafungua blog na kisha utajisajilo kwenye website yao...

Lakini kama mambo ya internet hufahamu vizuri basi tutakuelekeza namna ya kufanya kwa gharama nafuu sana.


Karibuni 0713774746
 
kwa upande wangu sitakushauri biashara gani ila ni vema uzingatie haya kwa uchache:
MOJA ni vema ujiulize binafsi kuwa hiyo pesa umeipta kwa njia gani eidah kwa kudunduliza kutoka katika biashara ndogondogo ndipo ukapata, je kwa msaada wa ndugu au mikopo? au bahati nasibu?? au mirathi??? m
swali hili ni la msingi sana kabla hujaitumia pesa yako. maana kuna biashara zenye mrejesho baada ya kitambo kirefu na zenye muda mfupi.
MBILI katika mawazo yote uliyopewa na utaklayopewa kuwa makini katika kuutumia mtaji wako, wataalam wa masuala ya biashara hushauri kuto tumia pesa yote uliyonayo ktk kuanzisha biashara maana ikianguka ndipo na ww anguko lako litakuwepo.
TATU ni lazima ujichunguze ww kuwa una interest na biashara na je biashara gani??? maana kama unfanya biashara eti kwa kuwa una mtaji tuu imekula kwako. na kama unafanya biashara fulani eti umeambiwa ina faida nzuri nawe ukafanya hivyo bila reseach ya ulipo kuwajua ni aina gani ya soko na wateja wanaokuzunguka basi utaptea.
kwa uchache tuuuu,
 
Me niko Moshi pia ninawazo la biashara tena inalipa kinoma,, ila mtaji sina kama utakua tayari ni pm tufanye kazi
 
Fanya mishe za utalii ama nenda mitaa ya majengo fungua carwash pale karibu na shule ya majengo sec. Ama mitaa ya KNCU ama KCMC makutini pale milion 3.5 inatosha inayobaki fungua duka la nafaka sehemu nzuri tumia 3million mengineyo ni laki 5 utabakiza balance 3m Nunua pikipiki 1.8million kwa ajili ya kurahisisha mambo yako na mda mwingine utaifanya kama bodaboda. Ukishindwa vyote nenda kwenye biashara za samaki na madini usisahau kuleta mrejesho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom