private agent
Member
- Apr 6, 2016
- 83
- 103
Habari zenu wakuu.
Modes naomba hii thread msiunganishe na nyingine nataka kujifunza kitu.
kama mnavyojua wakuu kwa sasa ajira zimekuwa ngumu na hata ukipata hiyo ajira utaishia kupewa laki tano tu as a net salary. Sasa katika pitapita zangu nikaotea kama ka millioni tatu hivi.
Nimeamua kuingia katika kilimo kwa kuwa kilimo nahisi ndo utajiri japo inabidi ukomae hasa, na mimi nimeshajitoa, na kilimo nilichoona kinafaa kwa kuanzia ni mpunga kwa kuwa nilishafanya biashara ya mchele kwa maana hiyo soko kidogo nalifahamu. Ila kama utakuwa na ushauri mwingine na mchanganuo wa uhakika naweza pia kufikiria kubadili, maana hapa niko katika upembuzi yakinifu.
Katika hizi millioni tatu nimetenga laki tano kwa ajili ya kukodisha ardhi hivyo nimebaki na millioni mbili na nusu. Naomba kwa wataalamu kwa hela hii naweza kuanza na hekari ngapi japo kwa kuanzia tu.