Mtaji wa Laki 3 kwa Mwanza

balyeb

Member
Sep 21, 2015
74
18
Habari za muda

Nina mtaji wa Tsh Laki 3.

Nipo Mwanza

Naombeni mnisaidie kunipa business ideas kulingana na mtaji huo nilo nao.

Mbarikiwe sana

Serious answers please kuna vijana wengi watafaidika na hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
balyeb,
Mwanza kubwa na mawazo ya biashara huwa yanakuja kwa kuangalia changamoto zilizo kwenye mazingira yako ambazo wewe kama mjasiliamali utaziangalia kwa jicho la FURSA.
 
Kwenye hiyo laki 3
Chukuwa laki moja hapo nenda lango moja siku ya jumatatu uwa wanafungua marobota ya viatu vya mitumba

Wewe chagua viatu vyako vya kutosha nenda kanunue brashi ya buku sabuni yako na unga na maji vionyeshe vizuri viatu vyako tafuta gepu linalopita watu panga hapo au tembeza huku mjini mbona utauza Sana tu

Angalizo

Akikisha lango unachukuwa viatu vya 4000 paka 8000 vipo vingi Sana alafu chagua viatu vizuri vipo vibovu vingi usije kupata vibovu ukajapata hasara

Nashukuru sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mwanza tafuta mkokoteni na jiko , choma au tafuta mtu wa kuchoma mishikaki na ndizi ,unaweza pita maeneo ya liberty,soko kuu zamani,uhuru ,soko jipya kote huko.

Kikubwa weka price nzuri
Unaweza fanya mishikaki 3 tsh1000 ,ndizi 3 tsh1000 au ukaweka 500

Angalizo mwanza sio watumiaji sana kwenye kula. Fanya analysis with Good price.

2:unaweza fungua kigenge cha kuuza zile pombe za 500 banana ,waleweshe vijana kadri unavyoweza. Tafuta eneo lenye mzunguko piga kazi.

Ukifanikiwa tukumbuka au toa ata shukrani

It is never too late to begin. Start now
 
Back
Top Bottom