Mtafutaji hachoki, akichoka kashapata

Mtafutaji hachoki, akichoka kashapata

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
4,042
Reaction score
16,872
Habari jamii Africa.

Kwakweli kuna namna nawaza nashindwa kujua haswa kusudi letu wanadamu ni nini kuwepo hapa Duniani.

Yaani kila siku ni hekaheka tu zisizoisha,hakuna siku utakuta watu wamepungua barabarani haswa mijini kwamba labda mtu kaamua kupumzika,ni harakati tu zisizoisha wakuu.

Ama kweli umasikini ni laana.
Hata wezi wote,au majambazi wote
Hawapendi kuiba kila siku,wanajua wanachofanya ipo siku kitahatarisha Uhuru au maisha yao,wanawaza wangeotea pigo moja takatifu kisha wafanye biashara.

Hata mtu mwenye wivu na vipato vya wenzie naye nafsi huwa inamsuta Kwa Hali aliyonayo naye huwaza ifike siku ajikute ana Billions of money ili aishi maisha fulani safi,lakini bahati mbaya ni ngumu.

Maisha ni mpango unaoanzia mbali, unahitaji msoto fulani,maisha hayataki uoga,uvivu na kukata tamaa,bali mtu anayerisk maisha.

Kuna watu Kwa Imani zao wametoa kafara wazazi,watoto,ndugu na jamaa,wapo waliofanikiwa,wapo ambao hawajafanikiwa yote Kwa yote ni namna watu tunahangaika,.

Kupandishwa vyeo,
Kukuza biashara zetu,
Kung'arisha nyota zetu,
Na hata kuzindika nyumba na kuwahandle wake zetu, ndoa imara n.k.

Ndugu zangu Rai yangu ni kuwakumbusha tu kuwa yote tunayoyafanya au kuwaza kuyafanya ni ubatili tu,wakati mwingine maisha mazuri si matokeo ya kujituma tu bali yanachagizwa na bahati pia ,kikubwa ni kumuomba MUNGU mkuu yeye ndiye anayejua na kutoa riziki zetu.

Chunga tamaa mbaya,
Kubali mapungufu yako,
Ridhika na unachopata.

Jack Daniel
 
Fact pia binadamu in nature hatuliziki ata ukipewa utajili wa mo utataka uwe kama Elon musk .......

Hakuna mtu anaishi na stress kama mwenye hela bora wewe kajamba nani unapata hata usingizi.....

Mwisho wa siku wote tunakufa...
 
Back
Top Bottom