Habarini za mida wanajamii wenzangu
Leo nimeona tuchangie mawazo pamoja kwa yale yanayoendelea mtaani kwa sasa njaa imekuwa kali sana kiasi kwamba kila mmoja anailaumu serikali.
Je, ni kweli serikali yetu inapaswa kulaumiwa kwa hali ngumu ya maisha kwa sasa mtaani kila unaekutana naye anadai utawala wa serikali hii umebana kila kona mpaka watu wanashindwa kupumua si kwa waajiriwa,wafanyabiashara,vibarua,mafundi,madaktari,walimu wote kwa pamoja wanapata maumivu ya sindano hii bila kuchagua anaepaswa kuugulia maumivu.
Sasa wabongo wenzangu tufanye nini? tuikimbie nchi yetu au tuendelee kula kipigo cha mbwa mwizi, mpaka tujue mbivu na mbichi zilizompoza bwana sungura mjanja.
Ahsante kwa kusoma