Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Maumivu wakati wa kukojoa ,,,maumivu makali ya kiuno,,,,maumivu ya kichwa na fluu ya mara kwa mara,,,,kutokwa na ute kama maziwa kwenye uumee,,
Hospital wamepima mkojo (u.t,i na mengine siyakumbuki) na kipimo kingine waliisema sijui biology napo hakukuonekena kitu ....masaada wako tafadhali amekata tamaa
 
1 Maumivu wakati wa kukojoa = Pendelea kunywa sana Maji,madafu,Juisi ya mananasi,Juisi ya muwa na Matikiti.
2 Maumivu ya kiuno = Kama kijana fanya mazoezi ya siteup unapofanya nenda moja kati moja kulia moja kushoto baada ya siku tatu tu nipe mrejesho. Lakini kama mtu mzima jaribu kulala chini kifua juu halafu kunja mguu mmoja goti lifike kifuani zuwia kwa dakika mbili kisha badilisha mguu mwengine rejea hivyo hivyo kwa dakika 15 hadi 30. Pia unaweza kununua dawa ya kupaka inaitwa KIPASI hii dawa nzuri sana.
3 Maumivu ya kichwa na Flu = Hio itakuwa ni Allergy tu unahitaji kutumia Cleritin kidonge kimoja kwa siku baada ya siku mbili au tatu utapata nafuu. lakini ushauri wangu tumia kwa wiki moja mpaka siku 10.
4 Kutokwa na Ute kwenye uume = Kama ni teenager mpaka 25y hio ni kukuwa kwa mwanaume ushajua unachokihitaji(mke) lakini unaweza kufanya mazoezi kupunguza kidogo hiyo kitu. Unaweza kuruka kamba au kukimbia. Lakini kama mtu mzima basi ukinywa hivyo vinywaji vya namba moja vitasaidia sana.
 
Vidonda vya tumbo hutokana na tatizo la acidity. Ni muhimu kujuwa kwanza kama unayo acidity pekee au umeambiwa na daktari kwamba unayo vidonda vya tumbo. Kama unayo vidonda vya tumbo, unaweza kuwa na bakteria ya "H.Pylori". Madawa zake ni tofauti na mtu aliyokua na acidity pekee.

Je uliambiwa nini na daktari?
Mie dr alithibitisha akaandika na omiprazole
 
Malaria, malaria, malaria. Nakumbuka tangu nikiwa secondary hadi sasa nina miaka 43 nikijitahidi sana mwezi. Kila aina ya dozi nimetumia kasoro quinine ya vidonge. Kila aina ya precaution nimechukua. Maji nakunywa mengi, chakula nakula mno. Bia ilibidi niache
Nipe tiba dk
kuna wakati huwa najaribu kuiacha, lakini maumivu huzidi naamua kunywa dawa
 
Dawa ya kutoa kitambi both for men and women

Mkuu, Hamna dawa ya kutoa kitambi. Hizo dawa zakupunguza kitambi na unene ni uwongo tu. Kitambi hupungua kwa ulaji bora, kupunga kunywa pombe na kufanywa mazoezi wa nusu saa kila siku. Chakula bora ni mboga na matunda. Samaki na nyama ya kuku ni nzuri. Jaribu kupunguza nyama ya ngo'mbe pamoja na vitu vya kukanga.
 
Hivi Dr sometimes najisikia kama nawashwa tumboni kwa ndani,itakuwa ni nini?

Hiyo unaweza kuwa
Samahani kama nimekukwaza kujibu wagonjwa kwenye uzi wako lakini hayo majibu nimekosea au?

Ndiyo kijana umekosea na ndiyo maana sijaelewa ulichopata bali kuharibu mazingira na jina lako tu. Maumivu ya kichwa na flu kama ni pamoja na homa au maumivo kwenye koo inaweza kuwa infection. Lazima huwa tunamuuliza mgonjwa nakupata historia kivizuri.

Maumivu wa kukojoa inaweza kuwa UTI. Sasa mtu akinywa maji tu haisaidii.

Tafadhali tuheshimu elimu na taluma za watu.
 
Dr Sajjad mimi nina hiyo H.pylori na nimeshatumia sana HELIGO KIT for H.Pylori mfululizo nne kwa mwezi mmoja na nusu ila nimepima damu naambiwa bado Bacteria wapo kny damu. Nifanyeje?
 
Hivi Dr sometimes najisikia kama nawashwa tumboni kwa ndani,itakuwa ni nini?

Kama hiyokuwashwa inaongezeka baada ya kula chakula ya mafuta au unaihisi kifuani pia inaweza kuwa tatizo la acidity na itabidi uchukuwe vidonge vya pantoprazole 40mg kila siku kwa muda wa wiki mbili. Lakini kama kuwashwa siyo hivyo basi niandikie ikoje.
 
Dr Sajjad mimi nina hiyo H.pylori na nimeshatumia sana HELIGO KIT for H.Pylori mfululizo nne kwa mwezi mmoja na nusu ila nimepima damu naambiwa bado Bacteria wapo kny damu. Nifanyeje?

Lakwanza mkuu, Bakteria wa H.Pylori wanakuwa tumboni na siyo kwenye damu. Unaweza kupima damu kujua kwamba wapo tumboni lakini hawakui ndani ya damu. Mbali na test hiyo, je unadalili yeyote?
 
Hiyo unaweza kuwa

Ndiyo kijana umekosea na ndiyo maana sijaelewa ulichopata bali kuharibu mazingira na jina lako tu. Maumivu ya kichwa na flu kama ni pamoja na homa au maumivo kwenye koo inaweza kuwa infection. Lazima huwa tunamuuliza mgonjwa nakupata historia kivizuri.

Maumivu wa kukojoa inaweza kuwa UTI. Sasa mtu akinywa maji tu haisaidii.

Tafadhali tuheshimu elimu na taluma za watu.
Mimi nilikwenda kumuona daktari wangu mwezi nyuma kutokana mimi nina sinus allergy alinipa dawa moja nimesahau jina lakini nakumbuka hio dawa ina ingredients ya steroids nimeitumia kwa wiki moja na nusu kichwa,homa na makamasi yalizidi nikaamua kuwacha ndio nikarudia kutumia Cleritin ambayo huyo mchumba wangu ndio aliniambia nitumie. Baada ya siku mbili kichwa,homa na mafua yote yalikwisha ndio maana nikamwabia ajaribu hio Cleritin sikujua kama nimekosea kuingilia taalamu isiokuwa yangu.
 
Maumivu wakati wa kukojoa ,,,maumivu makali ya kiuno,,,,maumivu ya kichwa na fluu ya mara kwa mara,,,,kutokwa na ute kama maziwa kwenye uumee,,
Hospital wamepima mkojo (u.t,i na mengine siyakumbuki) na kipimo kingine waliisema sijui biology napo hakukuonekena kitu ....masaada wako tafadhali amekata tamaa

Maumivu wakati wakukojoa, kama ulivyoambiwa hospitalini unayo UTI. Dawa zake hizi hapa:

1. Amoxiclav 500mg kutwa mara mbili kwa wiki moja. (inaondoa vimelea)
2. Cital liquid kunywa kutwa mara mbili kwa wiki moja. (inapunguza maumivu kwenye mkojo)
3. Kunywa maji kwa wingi (inapunguza idadi ya vimelea.

Maumivu ya kichwa na flu. Je unayo homa pia? na ukoo inauma pia?

Maumivu makali ya kiuno inatokea saa ngapi?
 
Back
Top Bottom