kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,784
- 20,155
Bunge la utawala wa ubaguzi wa rangi wa Israel Knasset, limepasisha kwa haraka katika hatua ya kwanza, mswada wa kibaguzi unaojulikana kama 'Taifa la Kiyahudi.'
Bunge hilo lilipasisha kwa pupa na ushabiki maalumu mswada huo, kwa kura 48 za ndio na 41 za hapana hapo siku ya Jumatano. Mswada huo ambao ulipendekezwa na chama cha Likud unazichukulia ardhi za Palestina ambazo zinakaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu tokea ubuniwe mwaka 1948 kuwa ni taifa la Mayahudi tu. Iwapo mswada huo utapasishwa katika hatua yake ya mwisho, Beitul Muqaddas itahasabiwa kuwa mji mkuu rasmi wa utawala huo bandia na pia lugha ya Kiibrania kuchukuliwa kuwa lugha rasmi ya dola hilo. Kwa kupitisha sheria inayojulikana kama 'Israel, Dola la Mayahudi', utawala huo wa Kizayuni unakusudia kurasimisha siasa zake za ubaguzi wa rangi na hatimaye kuzitwisha jamii ya kimataifa. Kwa kufanya hivyo utawala huo unafuatilia malengo kadhaa.
Kuwafukuza Wapalestina wote wanaoishi katika ardhi zilizotekwa na kukaliwa kwa mabavu na utawala huo mwaka 1948, ambapo wanapata Wapalestina milioni moja na nusu ni moja ya malengo makuu yanayofuatiliwa na utawala huo kupitia harakati zake hizo za kichochezi na kibeberu hivi karibuni katika ardhi za Wapalestina. Hatua hizo za Wazayuni zinathibitisha wazi kwamba hakuna sehemu yoyote ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel ambapo Wapalestina wanasalimika na jinai zake. Kuhusu suala hilo Wapalestina wanaoishi katika ardhi zilizotekwa na kukaliwa kwa mabavu na utawala huo mwaka 1948 ambao hawakuweza kuzihama ardhi hizo na ambao wanaitwa na Wazayuni kuwa ni Waarabu wa Israel, pia wanakabiliwa na siasa haribifu na za ubaguzi wa rangi za utawala huo. Lengo kuu la Utawala wa Kizayuni la kuwasilisha mswada wa kutajwa utawala huo kuwa ni dola la Kiyahudi ni kuandaa uwanja wa kufukuzwa Wapalestina wote katika ardhi zao halali na wakati huohuo kuzuia kuundwa kwa nchi huru ya Palestina.
Kwa miaka mingi utawala huo ghasibu umekuwa ukitumia mbinu mbalimbali kwa ajili ya kuwalazimisha Wapalestina wazihame ardhi zao na mipango mingi ya utawala huo ya kukandamiza, kuua na kuwabagua Wapelstina kwa misingi ya rangi ni sehemu ya mbinu hizo. Wapalestina wanaoishi kwenye ardhi zilizotekwa na kukaliwa kwa mabavu na utawala huo mwaka 1948 kimsingi hawana haki zozote za kiraia katika jamii ya Wazayuni na daima wako kwenye hatari ya kufukuzwa na kubomolewa nyumba zao. Utawala wa Kizayuni ambao una utamabulisho wa ubaguzi wa rangi daima umekuwa ukitekeleza miradi na siasa za kibaguzi katika maeneo wanakoishi Wapalestina na hasa katika ardhi zilizotekwa mwaka 1948, ambapo natija ya siasa hizo imekuwa ni kupungua pakubwa jamii ya Wapalestina wanaoishi katika ardhi zao hizo za jadi. Hatua hii mpya ya siasa za kijitanua utawala haramu wa Israel inathibitisha wazi kuwa aina yoyote ile ya Wapalestina kulegeza msimamo mbele ya utawala huo haina matokeo mengine isipokuwa kuimarisha vitendo vya ubeberu na kujitanua utawala huo katika maeneo ya Wapalestina.
Ni kwa kuzingatia ukweli huo ndipo Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ikasisitiza kwa mara nyingine kuwa hata kama asilimia 99 ya ardhi zote za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel zitakombolewa na kubakia asilimia 1 kwenye makucha ya utawala huo, bado harakati hiyo haitautambua rasmi utawala huo na kwamba itaendelea kupigania ukombozi wa asilimia 1 hiyo iliyosalia. Hii ni katika hali ambayo uzembe wa jamii ya kimataifa katika kupigana dhidi ya ubaguzi wa rangi wa Wazayuni umepelekea kuimarika kwa ubaguzi wa aina hiyo katika ngazi za kimataifa. Matokeo ya ubaguzi wa aina hiyo bila shaka ni mabaya zaidi kuliko matokeo ya ubaguzi mwingine wa rangi kama ule wa apartheid ulioshuhudiwa nchini Afrika Kusini, ufashisti na unazi dhidi ya jamii ya mwanadamu.
Parstoday.com