MSUMBIJI: Watu 6 wafariki katika ajali ya ndege iliyogonga mlima

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,267
ae7f335825cb99d76836ddd88e835110.jpg
78d81af5d66a7f0f000485461c2d5d5f.jpg
Mamlaka ya anga nchini Msumbiji imethibitisha kuwa ndege binafsi iliyobeba watu sita ilianguka na kusababisha vifo vya watu watano, na hali ya mtu mwingine bado haijulikani

Ndege hiyo iliyotoka Beira, Msumbiji na kuelekea Harare, Zimbabwe iligonga mlima Vumba karibu na mpaka kati ya Msumbiji na Zimbabwe na kuangukia nchini Zimbabwe

Idara hiyo imesema hali mbaya ya hewa inaweza kuwa chanzo cha ajali hiyo. Timu ya mafundi inayoongozwa na Zimbabwe imeanza uchunguzi wa ajali hiyo, huku idara hiyo ya Msumbiji ikisema ina wajibu wa kushirikiana na timu hiyo kwa kuwa ina data muhimu zinazoweza kusaidia uchunguzi huo.

Chanzo: CRI/Kiswahili
 
Back
Top Bottom