ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 79,084
- 84,973
Mozambique na Tanzania ziko kwenye vita Kali ya ushindani wa Kutawala soko la Nishati Kwa kutumia gesi asilimia yaani LNG.
Kila Nchi inapambana kuhakikisha inajenga viwanda vya kusindika gesi asili Kwa Ajili ya Mauzo ya Nje na ndani ya Nchi.
Mozambique ilikuwa tayari imeshaanaa ujenzi hapo kabla ila ukisimama Kutokana na vita ya Waasisi ambapo Sasa Wawekezaji wamesema wanatarajia kurudi site mwisho wa mwaka Ili kuendeleza ujenzi baada ya Hali kutulia.
Mradi wa Mozambique LNG utakuwa na thamani ya $20 Bilioni (Trilioni 52).
Ambapo Kwa upande wa Tanzania kazi ya kuwarudisha mezani wawekezaji Kwa Ajili ya mashauriani ya mgawanyo wa Mali Iko Mbioni kukamilika ambapo wakati wowote Serikali na wawekezaji watasaini HGA.
Mradi wa Tanzania inaonekana kusuasua huku Kila upande ukimtupia lawama mwenzio kukwamisha kuanza utekelezaji wa mradi mapema.
Mradi wa Tanzania una thamani ya $ 42 Bilioni (Trilioni 109) huku ukitarajiwa kuwa ndio mradi mkubwa zaidi wa LNG Duniani.
View: https://www.instagram.com/p/DMcbvNsoNhY/?igsh=MXVvdHIxdnE1c21tOA==
My Take
Mradi huu ukifaulu ndio itakuwa chachu ya kufikia malengo ya Dira ya 2050. Pia soma Mradi wa gesi-Lindi LNG Wa Thamani ya Trilioni 105 Hatihati Kukwamishwa na Michakato Isiyoisha. Ulitarajiwa Kuwa Legacy ya Samia | JamiiForums Mradi wa gesi-Lindi LNG Wa Thamani ya Trilioni 105 Hatihati Kukwamishwa na Michakato Isiyoisha. Ulitarajiwa Kuwa Legacy ya Samia