Mstahiki Meya Boniface Jacob afukuza na kusimamisha kazi watendaji kata na mitaa Manispaa ya Kinondo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob leo akihutubia watendaji wote wa kata 34 na mitaa 197,siku ya jumamosi 4/6/2016 amewafukuza na kuwasimamisha kazi watendaji Kata na Mitaaa wa wilaya hiyo sita kwa kosa la ubadhirifu wa zaidi sh. milion 400 katika maeneo yao ya kazi.
Watendaji Kata waliosimamishwa kazi ni Ernest Misa, Ally Bwamkuu na Mtendaji wa Mtaa Aneth Lema ambao walitenda makosa ya ubadhirifu wa fedha kwa kila mtendaji na idadi yake mwaka 2014,huku Mtendaji Dustan Kikwesha na watendaji wa mitaa Shaban Kambi na Richard wakisimamishwa ili kupisha uchunguzi.

Akizungumza na watendaji hao katika ukumbi wa manispaa hiyo,Mstahiki Meya Jacob alisema hatua za kuwafukuza watendaji hao zimefwatia baada ya kuwa na makosa mengi hata wakati mwingine kusimamishwa lakini sasa uongozi wa manispaa umeamua kuwafukuza ili iwe fundisho kwa watendaji wengine." kazi hii ya kufuatilia ndiyo tumeianza sasa na itaendelea mpaka kila mtendaji aendane na kasi yetu ya uadilifu wa kuwasimamia wananachi bila kufanya ubadhilifu... na wale waliosimamishwa nitahakikisha wanachunguzwa makosa yao na hatua zaidi zitachukuliwa juu yao"alisema Meya Jacob.

Pamoja na hayo ameagiza timu ya wakaguzi wa ndani manispaa ya kinondoni kwenda maramoja kupita na kukagua mahesabu ya fedha katika akaunti na ofisi zote 34 za kata za manispaa ya kinondoni,(special auditing) kabla ya mwaka wa fedha kuisha,aidha amewataka watendaji hao kuhakikisha wanakusanya mapato ya serikali katika Kata zao kwa uangalifu bila kumwonea mfanyabiashara aibu na kwamba watakaoshindwa watachukuliwa hatua ama aseme kashindwa kazi.

Aidha alizitaja na kuzisifia Kata zilizokusanya mapato vizuri kuwa ni Msasani,Sinza,Mikocheni,Mbezi Juu na Bunju na kueleza kuwa Kata zilizofanya vibaya hata kukalia kuti kavu kwa watendaji wake kwa kukusachanya mapato chini ya kiwango kuwa ni Mburahati,Kibamba,Mabibo,Mabwepande na Kimara.

Katika hatua nyingine Meya Jacob alitoa agizo kwa watendaji wa mitaa,kuwatambua na kuhakikisha WANAKUSANYA UPYA ORODHA ZOTE ZA MAJINA YA MABALOZI NYUMBA KUMI NA MISINGI KUTOKA KILA CHAMA NA KUWASILISHA KWA MKURUGENZI HADI KUFIKIA JULAI MOSI MWAKA HUU,VIONGOZI WA UKAWA NA CCM WAWASILISHE MAJINA YA MABALOZI WAO HARAKA ili kuwa na orodha yao kwa wilaya ya kinondoni itakayo tambuliwa na manispaa rasmi, Hata hivyo aliwataka watendaji kuhakikisha wanalifuatilia suala la usafi ikiwamo kuwapanga wafanyabishara ndogo ndogo ambao wamekaa bila mpangilio huku wakihakikisha wanakusanya mapato na kuwachukulia hatua wale wote wasiotaka kufuata maagizo.
 

Attachments

  • 13332942_1018972038138044_2380152306569566102_n.jpeg
    13332942_1018972038138044_2380152306569566102_n.jpeg
    12 KB · Views: 37
yaani haya yanayofanywa na ukawa,..ingekuwa tangu tumepata uhuru nchi ndo iko hivi.inaendeshwa namna hii kwa kuangalia maslahi ya taifa na wananchi kwa ujumla,..bsi leo tungekuwa tunashindana na south afrika kwa maendeleo na kuwekeza kwenye viwanda pia
tz ukiiwazia sana inatia hasira yani........hawa ma ccm wametufikisha hapa leo,.then leo wanajifanya watetez wa masikini pia kuleta nchi ya viwanda,tangu uhuru mlikuwa wapi???
hivi unawezaje kuleta viwanda huku upo katika system iliyofelisha hivyo viwanda miaka50 sasa na ushei,.
nchi ya viwanda bila reforms???maneno matupu2
hivi usa ingefika pale bila kuwa na reforms zilizoeleweka baada ya GED?????
Tusidanganyane,...ndani ya ccm,.hamna kitu........
ni wale wale2,ni ileile2
mfia chama hawez kuleta changes nchi hii
 
hembu weka uchama pembeni,hivi huoni mkuu wa wilaya happi anayoyafanya au ndo upofu wa uchama??

hawa combination yao ipo vizuri
Na hii fukuza fukuza na kusimamisha, si ndiyo yanayofanywa serikali kuu na watu wengine kulalamikia, ila huyu tunampongeza.
 
Mbona nimeona kwenye tv muda c mrefu kuwa chadema watazunguka nchi nzima kupinga watu kufukuzwa kazi ovyo? Watajipinga co?
 
Mbona nimeona kwenye tv muda c mrefu kuwa chadema watazunguka nchi nzima kupinga watu kufukuzwa kazi ovyo? Watajipinga co?
Hao wakija huku kwetu tunawapopoa na mayai viza..wamekaa bungeni miaka kumi ya jk walikuwa wanasafiri..
 
Hahahahah.....Daaaaah Aiseee.....Yani Chadema wanachekesha saaaana....Sasa wanampinga magu kuhusu nini na wao wanafanya nini?.....Atakayejibu kuwa huyu mayor kafuata taratibu za kuwafukuza kazi aniambie ni taratibu zipi
 
Mayor Jacob akifukuza ni sawa.....ila Dr. Magufuli akifukuza si sawa....
 
Huyu meya atakuwa anatumia ujeuri tu ila chama kitakuwa kilishamzuia..maana anawaharibia ajenda..
 
Back
Top Bottom