Msoto mwingine kwa watumishi wa umma waja

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,944
Hello guys wish you are fit!

Watumishi wa umma kuna dalili ladhaa za kula msoto tena kwa mwaka wa fedha unaotarajiwa kuanza hivi punde, yaani 2017/18.
Najua kwa mtumishi kuambiwa hivi hapendi, anataka apewe matumaini kama mtu anayeishi na VVU.
Binafsi mimi nilipoteza au kuchelewa kufanya issues zangu nikisubiri Julai, nilipoona kimya ndiye niliyekuwa front line kujifari pamoja na watumishi wenzangu kuwa soon mambo yatajipa, kumbe holaaaa mpaka leo.
Sasa mdundo wa Mh.rais naujua na step zake nazifahamu. Jipange kidogo unachopata ukizungushe vinginevyo utakula mchanga
-Jana kaanzisha defence mechanism nyingine, ya vyeti feki.
-Kumbukeni ripoti ya watumishi hewa rasmi haijatolewa, licha ya ile inayosomwa wakiwa majukwaani.
-Mpaka leo, hakuna aliyeomba samahani kwa watumishi zaidi ya kuwatisha na kuwataka wafanye kazi kwa bidii.
 
Hello guys wish you are fit!

Watumishi wa umma kuna dalili ladhaa za kula msoto tena kwa mwaka wa fedha unaotarajiwa kuanza hivi punde, yaani 2017/18.
Najua kwa mtumishi kuambiwa hivi hapendi, anataka apewe matumaini kama mtu anayeishi na VVU.
Binafsi mimi nilipoteza au kuchelewa kufanya issues zangu nikisubiri Julai, nilipoona kimya ndiye niliyekuwa front line kujifari pamoja na watumishi wenzangu kuwa soon mambo yatajipa, kumbe holaaaa mpaka leo.
Sasa mdundo wa Mh.rais naujua na step zake nazifahamu. Jipange kidogo unachopata ukizungushe vinginevyo utakula mchanga
-Jana kaanzisha defence mechanism nyingine, ya vyeti feki.
-Kumbukeni ripoti ya watumishi hewa rasmi haijatolewa, licha ya ile inayosomwa wakiwa majukwaani.
-Mpaka leo, hakuna aliyeomba samahani kwa watumishi zaidi ya kuwatisha na kuwataka wafanye kazi kwa bidii.
Nini hasa unachotaka kuongelea? Fafanua tukupate mkulu
 
Wadau nimebaki kinywa wazi kwa kushikwa na bumbuwazi niliyopigwa baada ya mkuu ZittoKabwe kudai kuwa kila wanaopanga kumteka au (kupita nae) kukumbana na kizingiti kizito mbele yake na hivyo kushindwa kutimiza hazma yao,
anadai kila wakifika kwake wanaambulia bila bila , maana mara nyingi wakienda kumsaka , hujikuta wameambulia kukutana na Mti wa Mrumba au Bwawa la Karosho (sio korosho ) au mara nyingine jamaa hao huambulia kukutana na ziwa Tanganyika mbele yao ,na kama hawaamini maneno yake basi wathubutu kuingia anga zake waone mziki wake.
na hiyo inatokana na yeye kama mwana Kigoma wa mwisho wa reli kuwa amekamilika katika idara zote za ufundi (wa anga, majini na nchi kavu) , hali hiyo imepelekea hao jamaa ambao ni wabaya wake kuwa wakipata tabu sana kumkamata kila wakipanga mission yao.
Sasa je, anataka kutuaminisha kuwa alitumia mbinu hizo pia kipindi kile alichodai kulala bungeni wakati alipolalama kuwa (kuna watu) walimsaka ili tu waondoke nae kaajili ya mahojiano..??
Je , kwa mwanasiasa kijana , msomi na nguli kama Zitto anatoa picha gani kwa wale walio nyuma yake au wanaomwamini...?? Maana anaonekana anaamini katika njia mbadala katika kupata uhakika wa ulinzi wake.
Hapo ndipo ninapoona kumbe ile kauli yake ya kusema atayediriki ku deal na yeye basi atapukutka kama ukoo wa panya.
Kwa habari zaid tafuta chanzo cha gazeti la Mwananchi la tarehe 15 April 2017 ,kwani wao wamefafanua kwa kina habari hii.
 
kusoma ripot ya watumishi 9000 itachukua miezi saba mbele..hatuwezi kulipa watumishi wenye vyeti feki
 
Heri ya Pasaka.


Naomba atakayekuwa kiongozi wa heshima, atakayewakilisha serikali katika siku ya 01-05-2017 BK, jumatatu, katika hotuba yake ajibu maswali yafuatayo:-

1.a) Lini serikali italipa nyongeza ya mshahara uliopaswa kuongezwa July 1, 2016?

b) je, tarehe 01-07-2017 kuna nyongeza?


2. Lini uhamisho wa wafanyakazi hasa walioko Mamlaka ya serikali za Mitaa waliokamilisha taratibu za uhamisho hadi June 2016 watapewa au watanyimwa kibali cha kuhamia walikoomba au watakakopangiwa?


3. Ni lini madai ya wafanyakazi yatalipwa?


4. Kwanini nafasi za kazi za wakuu wa idara na vitengo katika wizara, idara, mikoani na wizarani hazitangazwi hadharani ili wenye sifa waombe?

5. Kwa nini kima cha chini hakijawa TSh. 940,000/= kwa mwezi.



Nakutakia maandalizi mema ya hotuba, na kila jema katika utumishi wako uliotukuka.


Tanzania ni kubwa kuliko masilahi yetu.

Yesu amefufuka, Amina.
 
Mbaya zaidi watumishi wanatembezewa redundancy za kufa mtu kisa? "Mamlaka ya juu" imeelekeza taasisi zote zipeleke 5 percent ya mapato kwa Treasurer! badala ya wakurugenzi kubuni vyanzo vipya vya mapato wao wanapunguza wafanyakazi! Mwafwaaa
simakonda alisema kati ya watumishi 70 wenye tija hawazidi watatu, watumishi mizigo wapunguzwe tu. mbona wahitimu wa vyuo wanaambiwa wakajiajiri nyie na pension mnazo mitaji mnayo mulipiga hela wakati wa JK wasiwasi wa nini?
 
Yaani hii Serikeli inatufanya sote hatuna akili kama wao..Nakumbuka PM alimpa ultimatum Kairuki ya kumaliza zoezi la uhakiki hadi Dec mwaka jana lakini mpaka leo kimya
 
Hata tusemeje hakutakuwa na mabadiliko yoyote katika vipato vyenu zaidi ya kupunguziwa kodi kwa 1%. Na hii inatokana na kupungua kwa makusanyo ya kodi kushuka. Japo wahusika hawasemi lolote lakini hali halisi ipo wazi mtaani.
Hata kama vyama vya wafanyakazi vitakwenda mahakamani kama walivyojinasibu last week ili kuwahadaa wafanyakazi na kubuy time biashara iendelee kama kawaida ni hakuna kitakacholipwa iwe nyongeza wala madai.
Mwezi wa march naibu katibu mkuu tamisemi aliwaandikia makatibu tawala wote wa mikoa na wilaya wahakikishe watumishi hasa walimu wanalipwa madai ya likizo na nyongeza za madaraja lakini la kushangaza hakuna mwalimu hata mmoja aliyelipwa licha ya barua ile kuweka ultimatum ya tarehe 5 march.
Hii ni hadaa na fedheha kwa watumishi hawa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom