simba29
Senior Member
- Jun 22, 2011
- 193
- 67
MSOMI.
Shika kalamu itulize,
Andika karatasini usijiulize,
Nakufunza kuandika vyema uweze,
Usikawie utafeli sauti yangu itekeleze,
Somo ni imla ,habari ni ndefu,
Ongeza kasi jioni mwanga hafifu,
Andika vyema mwalimu nijisifu,
Hati ya kuumba fupi au ndefu,
Hakuna kama Mimi kunipata si rahisi,
Sana najiamini Mwingi ujuzi na ufanisi,
Nishauriwe na nani? Simba wengine fisi,
Endelea kuandika utasoma badae notsi,
Mwanafunzi mzembe simtamani,
Mjuaji hatupatani,
tulia darasani usome kwa amani,
Mbishi narudisha nyumbani,
Napenda wanaoniamini,
Ntakuondosha usipokua na Mimi,
Funzo la nguvu ya ulimi,
Jifunze hifadhi akilini,
Wachukia hilo somo,
Tazama karatasi ziba mdomo,
Nitamaliza ukishaelewa somo,
Usisahau elimu haina ukomo.
S1mba
©2016
Shika kalamu itulize,
Andika karatasini usijiulize,
Nakufunza kuandika vyema uweze,
Usikawie utafeli sauti yangu itekeleze,
Somo ni imla ,habari ni ndefu,
Ongeza kasi jioni mwanga hafifu,
Andika vyema mwalimu nijisifu,
Hati ya kuumba fupi au ndefu,
Hakuna kama Mimi kunipata si rahisi,
Sana najiamini Mwingi ujuzi na ufanisi,
Nishauriwe na nani? Simba wengine fisi,
Endelea kuandika utasoma badae notsi,
Mwanafunzi mzembe simtamani,
Mjuaji hatupatani,
tulia darasani usome kwa amani,
Mbishi narudisha nyumbani,
Napenda wanaoniamini,
Ntakuondosha usipokua na Mimi,
Funzo la nguvu ya ulimi,
Jifunze hifadhi akilini,
Wachukia hilo somo,
Tazama karatasi ziba mdomo,
Nitamaliza ukishaelewa somo,
Usisahau elimu haina ukomo.
S1mba
©2016