Msitakabali wa dhana ya itikadi litengwe darasa


M

mwakajilae

Member
Joined
Mar 11, 2011
Messages
58
Likes
0
Points
0
M

mwakajilae

Member
Joined Mar 11, 2011
58 0 0
Natambua umuhimu wa suala la itikadi,ambapo natambua kuwa ndiyo msingi mkubwa juu dira ya Taifa ,lakini pengine kupitia itikadi tunaweza kupata muafaka juu ya ni nini uwe utumbulisho wetu katika jamii ya kimataifa na hata ndani ya nchi ambapo leo tupo njia panda juu ya miiko ya uongozi na mipaka yake.,ambapo endapo kama hatutakuja kwa pamoja kama Taifa,naona kuna vita inalinyemelea Taifa itakayo kuwa ngumu na hatari kuliko tikisiko la vita ya Kagera1978.

Masuala yote ambayo tumeyajadiri na pengine vyama vya wafanyakazi na Taasisi za wanafunzi vyuo vikuu kuchukua hatua ya kufanya shinikizo la migomo katika kudai maslahi bora na mikataba isiyo na uadilifu kwa Taifa,ni daili tosha kabisa kwamba kuna ombwe kubwa juu ya itikadi itakayounda mifumo yetu ya uchumi,siasa na jamii.,kwasababu Taifa liko kwenye mkanganyiko ni nani anawajibika kwa lipi?na yupi anawajibika kwa hili?na namna gani.,kwa maana hiyo hata sera zetu nyingi tunazozitunga lazima zitafuata mfumo wa itikadi ya nchi.
Kwamfano wakati kuna mgogoro mkubwa juu ya ninani anagharimia elimu yetu na kwa namna gani?chukulia mfumo wa itikadi ya ujamaa isome na uielewe,chukua Itikadi ya ubepari uisome na uielewe vizuri na kupitia sera ya elimu ya juu,hususani na utungwaji wa sheria ya utekelezaji wa sera hiyo katika eneo la bodi ya mikopo nchini.
utagundua uwapo wa sheria ya cost sharing,ambapo mwanafunzi anapewa mkopo asilimia miamoja ama vinginevyo na ana lazimika kurejesha mkopo wote alio kopeshwa!!!!,sasa najiuliza mzigo wa serikali upo wapi hapo?kwa maana hiyo serikali imejiondoa katika kusomesha wanafunzi wake katika Taifa linalojali wananchi wake kubaki kuwa mdhamana tuu na siyo mdau katika maendeleo ya elimu!!wanafunzi wenyewe hawakuhusishwa katika utungwaji wa sera hii.
karibu tujadili itikadi na uhusiano wa sera zetu pamoja na miiko ya Taifa ,nadhani mpaka sasa watanzania tunajadiri ufisadi pamoja na mengine mengi pasipo kujadiri mifumo yetu,ikiwa itikadi ni mfumo mama.,nenda Marekani na pengine pengi ambako ni mataifa ya itikadi ya kibepari lakini nao wana maadili yao kama Taifa,,sisi tutajadiri maendeleo juu ya malengo ya milenia,juu ya mpango mkakati kuelekea2015 kamwe hatufiki kama hatujarudi kwenye mpagharanyiko wa kiitikadi.
 

Forum statistics

Threads 1,249,419
Members 480,661
Posts 29,697,542