Msimamo wa serikali ni nini??

Msimamo wa serikali ni nini??

Navoyne

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2010
Posts
874
Reaction score
373
Habari zenu wana bodi.

Naomba kuuliza kuhusu msimamo wa serikali kuhusu "Ushoga" maana nimeangalia mitaani hali inazidi kuwa mbaya na tatizo jingine ni kwamba raia hawajui nini cha kufanya maana kuna sheria ya kukataza kwa kifungo kikubwa tu ila hakuna watu wa kusimamia hii sheria.

Mkuu wa mkoa wa Dar alisimama kifua mbele kwamba yeye ni bingwa wa vita alipotangaza vita ya ushoga lakini sijasikia hata mtu mmoja katiwa hatiani na ile kauli ni kama iliwapa motisha mashoga kujitangaza hadarani ila mpaka naandika mada hii hakuna hatua wala mtu aliyekamatwa.Mbona mambo mengine yanafanikiwa kama hayafanikiwi kuna mijadala kwanini yameshindwa kufanikiwa.

Polisi walisema wao watasimamia sheria kwa kukamata shoga yeyote yule lakini kuna yule shoga maarufu Kaoge alijitangaza yeye ni shoga na hawezi kuacha kwenye tv lakini sikusikia amekamatwa na polisi wala kuhojiwa na polisi kwa kosa hilo ila Zamaradi alipewa adhabu na mammlaka husika, Je tatizo ni nini hasa??
Maoni: Naona ifike mahali tuwe wakweli kama taifa na tuweze kuzungumza kama matatizo yanayokumba jamii yetu ila inabidi tuchague upande hatuweze kuendelea kukwepa kufanya maamuzi. Ushoga Tanzania ni tatizo na je sheria zetu zinafanya kazi na kama hazifanyi kazi kuna umuhimu wa kuwa nazo??
 
Makonda alikuwa anatafuta SIFA za kijinga kama ilivyo kawaida yake.

Vita hii kwa mtazamo wangu ni rahisi sana kama kweli walioianzisha wana dhamira ya dhati ya kupambana na ushoga.

Hii ni kwasababu vijiwe na sehemu zote wanapopatikana mashoga kunajulikana.

Sheria dhidi ya vitendo vya ushoga ipo very clear lakini hakuna kinachofanyika.

Ama labda kuna some external forces linazuia hii vita. Maana ina fahamika baadhi ya mataifa makubwa yana support haya majamaa yaliyolaaniwa.
 
Sasa kwanini tusikubali tu kwamba tumefuta sheria za ushoga na kuangalia jinsi ya kuishi pamoja kwenye jamii yetu, maana kuna wengine bado wanabakwa na kunyanyaswa. Kwanini ni kama mwiko kwa viongozi kuongelea hili??
 
Polisi hawawezi kupoteza muda kutafuta mashoga wakati mitaani kuna wezi na vibaka. Hizi sheria zimewekwa tu ili kufurahisha watu kama wewe ila serekali inajua kwamba kukamata mashoga italeta hasara kuliko faida ndio mana sheria zipo ila hazitumiki.
 
Ni upuuzi kuwa na sheria isiyokuwa na meno.......kwanini tusiifute??
 
Mi naona hakuna sheria ktka hili wasingekuwa wanajitangaza ktka vyombo vya habari kuwa wao ni mashoga wakongwe
 
Mi naona hakuna sheria ktka hili wasingekuwa wanajitangaza ktka vyombo vya habari kuwa wao ni mashoga wakongwe
Hapa ndio panapo nitatiza mimi kwanini hatuwakamati na kuwachukulia hatua za kisheria maana sheria ipo...... na kama tunaona hakuna umuhimu wa kuwachukulia hatua kwanini tusifute hizi sheria kuliko kusimama kwenye majukwaa na kukemea bila kuchukua sheria. je sheria zetu zinatusaidia nini??
 
Back
Top Bottom