Rashid Mfaume Kawawa Alikuwa na busara ya kukaa kimya kuhusu mambo yanayoendelea ndani ya ccm. Alijua kabisa kuwa si rahisi kutoa maoni na yakakubaliwa na kufanyiwa kazi katika kipindi hiki ambacho wengi hawaelewi kinachoendelea zaidi ya kupata maoni ya vyombo vya habari. Subirini mwaka huu mtashuhudia mwanzo wa mabadiliko makubwa ndani ya nchi kwani, kumekuwa na demokrasia kubwa ya kutoa maoni kiasi cha watanzania kuelezana ukweli bayana. Pamoja na yote, ni jukumu la kila mtanzania kufanya jitihada ya kuwa mzalendo katika naafasi yake. Ni nani asiyejua kuwa, wengi wapatapo naafasi wanasahau walikotoka, wanabadilika, wanakuwa Mi-Ungu watu na kuanza Ufisadi? Mafisadi wa mawazo ni wabaya kuliko mafisadi waliokwiba tayari katika madaraka. Tubadilike na tuanze jitihada za mabadiliko kwa kubadilika kwanza sisi wenyewe watanzania. Ni nani asiyejua kuwa watanzania wengi wana roho mbaya, hawapendi maendeleo ya wenzao, wanajilimbikizia mali na hatuna uzalendo na nchi yetu.
Kwa mfano, nani anajali kuzorota kwa kilimo Tanzania, Nani anajali rasilimali za nchi zinavyoporwa kwenda nje ya nchi, nani anajali wanafunzi wasio na uwezo wa kujisomesha? Badala ya kuhoji kauli za Mzee Kawawa, tubadilike. Tuache tabia za kufanya mambo yasiyo ya msingi. Tuache Maharusi ya gharama wakati hatuna vitega uchumi. Tuache sifa za kujenga majumba ya fahari ya mamilioni ya shilingi badala ya kuwekeza katika kilimo na biashara. Ni Mtanzania gani amewekeza na kuajiri watanzania wenzake? Ni mtanzania anatumia pesa kwa busara na kuwasaidia watanzania wenzake kwa namna yoyote ile iwayo. Bila kuwa na mabadiliko ya sisi wenyewe kwanza hatuta fika mbali. Tuwe wabunifu, tuanze kutumia akili zetu na kufanya mambo ya kufanya wengine waige. Tuongee kidogo na tutafute miradi ili mwisho wa siku tuwe watanzania wenye ubunifu, miradi, rasilimali na kauli zenye nguvu. Tutabadilisha nchi kwa kuanza na mabadiliko ya sisi wenyewe. Kinyeme na hapo, tutakuwa watu wa kuzungumza tu. Mimi ni mtoto wa mkulima lakini nimejitahidi nina taasisi yenye wanafunzi takribani mia nane hivi. Tukiwa wengi katika secta mbali mbali mwisho wa siku tutasikilizwa tu. Tuwe na uwezo katika maeneo tafauti ya kusema wewe hautufai kuwa mbunge nk. Msisahau Tunapiga kelele za mafisadi wakati sisi na wazazi wetu ndo tuliowachagua. Tumemchagulia JK Wabunge gani wa kupewa uwaziri? Au sisi hatishiriki uchaguzi na tunabaki kulalamika. Mimi Kwa mfano nina uchukuwa mkoa wa Iringa na kuangalia ni nani wenye sifa ya kuwa mawaziri. Ni hawa: Mh. Lukuvi - Isimani, Mh. Mbega - Iringa Mjini, Mh. Prof. Msolla - Kilolo, Mh. Mungai - Mufindi, Mh. Malangalila - Kalenga, Mh. Makweta sehemu ya Njombe, Mh. Ann Makinda Sehemu ya Njombe, Mh. Kivela - Sehemu ya Njombe, Pro. Mwalyosi, Ludewa, Makete nimemsahau. Ni nani katika hao atakuwa waziri mzuri ambaye ataleta mabadiliko katika nchi? Nadhani wengi wao wamepata naafasi na hawana jipya. Yafaa tujue namna nchi inavyopata viongozi, tushiriki na tuone kama kweli sisi tunastahili kutoa maoni.