Msimamo wa Mzee Kawawa kuhusu yanaoendelea Nchini ni upi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msimamo wa Mzee Kawawa kuhusu yanaoendelea Nchini ni upi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, Jan 2, 2010.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Wadau, juzi nikiwa safarini huko kwenye mapori mazito ya Kibondo-Kahama kutoka mwisho wa reli kurudi makazi yangu, nilipokea ujumbe wasimu kutoka kwa rafiki yanku kuwa Mzee Kawawa katutoka. Kwa kweli nilihuzunika sana, si kwa kuwa Mzee wetu katutoka, hapana (maana najua umri wake ulikuwa umesogea sana na afya yake haikuwa nzuri).

  Huzuni yangu kubwa ilisababishwa na jinsi nilivyokuwa nikiisubiri kwa hamu kauli yake kuhusu mambo yanayoendelea nchini mwetu tangu Uongozi wa awamu ya 4 uingie madarakani. Nilisubiri kwa shauku kauli na msimamo wake kuhusu yafuatayo:-

  1. Tuhuma za Ufisadi zinazowakabili viongozi wetu- EPA, RICHMOND, nk
  2. Mparanganyiko/Msigano ulioanzishwa na Mtandao uliomuingiza JK madarakani
  3. Ombwe la Uongozi linalodaiwa kuwepo nchini
  4. Msimamo wake kuhusu Mdahalo wa MNF na maazimio yake kuhusu hatima ya Uongozi wa nchi yetu na nchi yetu
  5. Mengineyo mengi

  Kwa kuwa wazee wetu walokuwa viongozi enzi za MWalimu hadi Awamu ya wamezungumza na kutoa maoni yetu, Mzee Kawawa nilitarajia naye angetoa msimamo wake lakini kwa bahati mbaya sikubahatika kumsikia, maana mara nyingi imekuwa ni vigumu kwangu kupata habari za mambo yanayojiri kwa haraka kutokana na kuwa pembezoni-pembezoni mwa nchi ambapo hata mitando ya simu inapatikana kwa taabu.

  Wadau namomba mnijuze, Mzee wetu Kawawa alituachia kauli gani kuhusu mambo yanayoendelea nchini mwetu?
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Jan 2, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,562
  Likes Received: 3,858
  Trophy Points: 280
  Kawawa ameshafariki, ametimiza siku zake, mzee alilijenga taifa.Hakuwa mtu wa dini, kabila wala makundi.

  Kama angesema angesema kama mwananchi yeyote yule, hakuna jipya ambalo angesema, angesema JK na serikali ni mafisadi kamwe Kawawa asingemfagilia JK! na kama angesema hivyo nini kingefanyika? kura yake moja ingemtoa JK madarakani?

  Aliona kuna watanzania milioni 40 wana nguvu na afya kuliko yeye , hao ndio wakisema kitu kwa umoja hakuna wa kupinga!

  Unaishi wewe na tunataka kauli na vitendo vyako kwa taifa la sasa na lijalo, yeye emeshamaliza wajibu wake.
   
 3. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  ukweli utabaki pale pale asingekuwa na jipya zaidi ya kuijenga ccm asingekuwa tayari kusema ukweli kama ulivyo na kuibomoa ccm yao ccm aipendi ukweli na ukiwa mkweli utakuwa kinyume chao
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,594
  Trophy Points: 280
  Kama ana suPport JK na Mtandao atakuwa na neno la kupinga ufisadi kama analo hana support...muda wake ulishapita...hana nguvu maana Mchonga hayupo atamshitaki kwa nani JK akihariibu!!???amekufa nalo moyoni!!!Kama aliacha wosia na msimamo wake wa kweli aulizwe Prof Mwafongo!!
   
 5. k

  kibananhukhu JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Rashid Mfaume Kawawa Alikuwa na busara ya kukaa kimya kuhusu mambo yanayoendelea ndani ya ccm. Alijua kabisa kuwa si rahisi kutoa maoni na yakakubaliwa na kufanyiwa kazi katika kipindi hiki ambacho wengi hawaelewi kinachoendelea zaidi ya kupata maoni ya vyombo vya habari. Subirini mwaka huu mtashuhudia mwanzo wa mabadiliko makubwa ndani ya nchi kwani, kumekuwa na demokrasia kubwa ya kutoa maoni kiasi cha watanzania kuelezana ukweli bayana. Pamoja na yote, ni jukumu la kila mtanzania kufanya jitihada ya kuwa mzalendo katika naafasi yake. Ni nani asiyejua kuwa, wengi wapatapo naafasi wanasahau walikotoka, wanabadilika, wanakuwa Mi-Ungu watu na kuanza Ufisadi? Mafisadi wa mawazo ni wabaya kuliko mafisadi waliokwiba tayari katika madaraka. Tubadilike na tuanze jitihada za mabadiliko kwa kubadilika kwanza sisi wenyewe watanzania. Ni nani asiyejua kuwa watanzania wengi wana roho mbaya, hawapendi maendeleo ya wenzao, wanajilimbikizia mali na hatuna uzalendo na nchi yetu.

  Kwa mfano, nani anajali kuzorota kwa kilimo Tanzania, Nani anajali rasilimali za nchi zinavyoporwa kwenda nje ya nchi, nani anajali wanafunzi wasio na uwezo wa kujisomesha? Badala ya kuhoji kauli za Mzee Kawawa, tubadilike. Tuache tabia za kufanya mambo yasiyo ya msingi. Tuache Maharusi ya gharama wakati hatuna vitega uchumi. Tuache sifa za kujenga majumba ya fahari ya mamilioni ya shilingi badala ya kuwekeza katika kilimo na biashara. Ni Mtanzania gani amewekeza na kuajiri watanzania wenzake? Ni mtanzania anatumia pesa kwa busara na kuwasaidia watanzania wenzake kwa namna yoyote ile iwayo. Bila kuwa na mabadiliko ya sisi wenyewe kwanza hatuta fika mbali. Tuwe wabunifu, tuanze kutumia akili zetu na kufanya mambo ya kufanya wengine waige. Tuongee kidogo na tutafute miradi ili mwisho wa siku tuwe watanzania wenye ubunifu, miradi, rasilimali na kauli zenye nguvu. Tutabadilisha nchi kwa kuanza na mabadiliko ya sisi wenyewe. Kinyeme na hapo, tutakuwa watu wa kuzungumza tu. Mimi ni mtoto wa mkulima lakini nimejitahidi nina taasisi yenye wanafunzi takribani mia nane hivi. Tukiwa wengi katika secta mbali mbali mwisho wa siku tutasikilizwa tu. Tuwe na uwezo katika maeneo tafauti ya kusema wewe hautufai kuwa mbunge nk. Msisahau Tunapiga kelele za mafisadi wakati sisi na wazazi wetu ndo tuliowachagua. Tumemchagulia JK Wabunge gani wa kupewa uwaziri? Au sisi hatishiriki uchaguzi na tunabaki kulalamika. Mimi Kwa mfano nina uchukuwa mkoa wa Iringa na kuangalia ni nani wenye sifa ya kuwa mawaziri. Ni hawa: Mh. Lukuvi - Isimani, Mh. Mbega - Iringa Mjini, Mh. Prof. Msolla - Kilolo, Mh. Mungai - Mufindi, Mh. Malangalila - Kalenga, Mh. Makweta sehemu ya Njombe, Mh. Ann Makinda Sehemu ya Njombe, Mh. Kivela - Sehemu ya Njombe, Pro. Mwalyosi, Ludewa, Makete nimemsahau. Ni nani katika hao atakuwa waziri mzuri ambaye ataleta mabadiliko katika nchi? Nadhani wengi wao wamepata naafasi na hawana jipya. Yafaa tujue namna nchi inavyopata viongozi, tushiriki na tuone kama kweli sisi tunastahili kutoa maoni.
   
Loading...