Msimamo wa Maalim Seif siku zote ni kuvunja muungano, na jino kwa jino. Huu ndio utakuwa msimamo mpya wa ACT-Wazalendo?

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
11,318
19,202
Nikitafakari juu ya muungano wa Seifu na Zitto, sikosi kufikiria ni jinsi gani wataendesha chama cha ACT-Wazalendo kwa kuwa na lugha moja. Najiuliza kama ni Zitto au Seifu ambaye atakubali sera za mwenzake, au wataamua kuzichanganya ili kukipa chama mwelekeo mpya. Angalau wana mambo kadhaa ambayo wanafanana - dini moja hivyo kukua katika malezi yanayofanana. Na wote wana historia ya kufukuzwa toka vyama vyao vya awali, CCM na Chadema, na huenda hii ikawaunganisha sana. Wameanza vizuri kwa Seifu kupewa kadi namna moja - japo haieleweki hii kadi namba moja ilikuwa inamngojea nani na Zitto amekuwa na kadi namba ngapi siku zote hizi!

Ila sasa, kwa upande wa pili, wengi watasema Zitto na Seifu wote ni wabishi sana, na kila mmoja ana hulka ya kuona bila yeye chama hakiwezi kwenda popote! Hilo itabidi waliangalie kwa makini.

Zaidi ya hapo, hatusahau kwamba siku zote Seif amekuwa na msimamo wa kutaka kuvunja muungano wa bara na visiwani, na mtazamo wa jino kwa jino pale anapohisi kuonewa na serikali. Je, tutarajie mabadiliko ya itikadi ya ACT-Wazalendo kuelekea kuvunja muungano na sera za jino kwa jino?
 
Nikitafakari juu ya muungano wa Seifu na Zitto, sikosi kufikiria ni jinsi gani wataendesha chama cha ACT-Wazalendo kwa kuwa na lugha moja. Najiuliza kama ni Zitto au Seifu ambaye atakubali sera za mwenzake, au wataamua kuzichanganya ili kukipa chama mwelekeo mpya. Angalau wana mambo kadhaa ambayo wanafanana - dini moja hivyo kukua katika malezi yanayofanana. Na wote wana historia ya kufukuzwa toka vyama vyao vya awali, CCM na Chadema, na huenda hii ikawaunganisha sana.

Ila sasa, kwa upande wa pili, wengi watasema Zitto na Seifu wote ni wabishi sana, na kila mmoja ana hulka ya kuona bila yeye chama hakiwezi kwenda popote! Hilo itabidi waliangalie kwa makini.

Zaidi ya hapo, hatusahau kwamba siku zote Seif amekuwa na masimamo wa kutaka kuvunja muungano, na mtazamo wa jino kwa jino pale anapohisi kuonewa na serikali. Je, tutarajie mabadiliko ya itikadi ya ACT-Wazalendo kuelekea kuvunja muungano na sera za jino kwa jino?

Muungano unakufaidi nini? kama kila upande kuna Rais wake, katiba yake na bendera?
 
Muungano gani?
 
Muungano unakufaidi nini? kama kila upande kuna Rais wake, katiba yake na bendera?
Bado ni muungano na upo kisheria. Kuwa na raisi Zanzibar isikupe shida, hata Yanga walishakuwa na raisi, na bendera hata maskauti wanayo. Katiba hata chama cha machangudoa nchi fulani wanayo.
 
Nikitafakari juu ya muungano wa Seifu na Zitto, sikosi kufikiria ni jinsi gani wataendesha chama cha ACT-Wazalendo kwa kuwa na lugha moja. Najiuliza kama ni Zitto au Seifu ambaye atakubali sera za mwenzake, au wataamua kuzichanganya ili kukipa chama mwelekeo mpya. Angalau wana mambo kadhaa ambayo wanafanana - dini moja hivyo kukua katika malezi yanayofanana. Na wote wana historia ya kufukuzwa toka vyama vyao vya awali, CCM na Chadema, na huenda hii ikawaunganisha sana. wameanza vizuri kwa Seifu kupewa kadi namna moja - japo haieleweki hii kadi namba moja ilikuwa inamgojea nani na Zitto amekuwa na kadi nammba ngapi siku zote hizi!

Ila sasa, kwa upande wa pili, wengi watasema Zitto na Seifu wote ni wabishi sana, na kila mmoja ana hulka ya kuona bila yeye chama hakiwezi kwenda popote! Hilo itabidi waliangalie kwa makini.

Zaidi ya hapo, hatusahau kwamba siku zote Seif amekuwa na masimamo wa kutaka kuvunja muungano wa bara na visiwani, na mtazamo wa jino kwa jino pale anapohisi kuonewa na serikali. Je, tutarajie mabadiliko ya itikadi ya ACT-Wazalendo kuelekea kuvunja muungano na sera za jino kwa jino?

Muungano una faida gani kwako? kama majority ya wazanzibari hawautaki muungano then hakuna haja ya kuwalazimisha muungano.
 
Sio maalim seif peke yake anayependa muungano uvunjike bali sote hatuhitaji muungano wa kiboya kama huu.

Hata kama utavunjika leo hii poa tu ni bora uvunjike nyie wadhalimu wa lumumba lazima mjikombe ilimradi muungano uwepo lakini muungano huu wa hovyo upo karibu sana utavunjika tu
 
Kwa hiyo huo ndio msimamo mliopeleka kwa Zitto kwenye ACT-Wazalendo?
 
Lete serikali tatu tusonge mbele, kama hizo serikali tatu hatuzipati basi vunjilia mbali muungano wa kuwekeana usiku tu!.
Huu umekuwa ni muungano wa CCM kupeana vyeo tu na kula kodi za wananchi hauna tija kwa Watanganyika wala Wazanzibari
 
Mkuu, unaongea mtazamo wako, sidhani kama ndio mtazamo uliopelekwa ACT-Wazalendo toka CUF.
 
Pamoja Na Madhaifu ya Chadema huwa nawapenda Kwenye baadhi ya aMambo ikiwemo wakionywa huwa wanaonyeka mfano walipoonywa kuhusu Mambo ya Operation Ukuta wakaachana nayo.

Sasa Kama ACT itapokea Kila kitu Cha CUF ikiwemo zile vurugu Za matawi yao ya Kosovo, Sijui Ukanda wa Gaza Sijui chechnia kwenda Kwenye Mikutano ya Hadhara wamejipaka Damu Na kuchochea Vurugu Kila Mara watapotea Kama walivyopotea CUF

Watanzania hawapendi Vurugu kwao Amani ndio kipaumbele Cha Kwanza
Zitto akiiga zile Siasa Za Chinja chinja tutawasahau soon
 
Bado ni muungano na upo kisheria. Kuwa na raisi Zanzibar isikupe shida, hata Yanga walishakuwa na raisi, na bendera hata maskauti wanayo. Katiba hata chama cha machangudoa nchi fulani wanayo.

Sheria ipi, kwani muungano ukiwepo kisheria vyama vingi na kazi za vyama vya kisiasa havipo kisheria?
 
Pamoja Na Madhaifu ya Chadema huwa nawapenda Kwenye baadhi ya aMambo ikiwemo wakionywa huwa wanaonyeka mfano walipoonywa kuhusu Mambo ya Operation Ukuta wakaachana nayo.

Sasa Kama ACT itapokea Kila kitu Cha CUF ikiwemo zile vurugu Za matawi yao ya Kosovo, Sijui Ukanda wa Gaza Sijui chechnia kwenda Kwenye Mikutano ya Hadhara wamejipaka Damu Na kuchochea Vurugu Kila Mara watapotea Kama walivyopotea CUF

Watanzania hawapendi Vurugu kwao Amani ndio kipaumbele Cha Kwanza
Zitto akiiga zile Siasa Za Chinja chinja tutawasahau soon

Akina maalim Seif wangekuwa ni watu wa vurugu kuna watu sasa hivi wangekuwa indicted the Hague, ila amepambana kwa kutumia mbinu zote za amani na za kisiasa lakini wameendelea kumuonea tu.
Kwa hiyo suala la amani wala lisikupe shida, ila watawala wakipandwa na kiburi kudhani kuwa wanaweza kufanya chochote basi ipo siku watashangaa masika yametokea wapi kwenye jua kali!
 
Ngoja washinde uchaguzi ndio tutajua. Pili, muungano ambao una matakwa ya wananchi hauwezi kuvunjika isipokuwa ule wenye maslahi ya wanasiasa. Sijawahi kusikia muungano wa USA, UK nk kuwa uko hatarini, lkn kinyume chake muungano wa maguvu kama USSR, Chekoslovakia, Yugoslavia, ndiyo iliyovunjika.

Tatu, kwenye demokrasia ya kweli, wanasiasa huwashirikisha wananchi wao yanapokuja masuala muhimu kama hayo, Muungano wa Tanzania hauwezi kuvunjika kwa matakwa ya wanasiasa. Nia ya chama cha siasa ni kushika dola, wanasiasa wanafuata upepo, hata kama nia ipo lazima asikilize umma unataka kitu gani.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom