Joseph Mshinga
JF-Expert Member
- Aug 27, 2014
- 232
- 143
MSIMAMO WANGU JUU YA UVUNJAJI WA DEMOKRASIA NA KATIBA YA ZANZIBAR.
na:Joseph Mshinga
Matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar yalifutwa kwa amri ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar (ZEC) bwana Jecha S. Jecha.
muda mfupi tu baada ya matokeo kufutwa nilisema wazi kuwa TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR HAINA MAMLAKA KISHERIA YA KUFUTA UCHAGUZI.
wapo walionibeza kuwa uamuzi ule ulikuwa haujakiuka sheria lakini niliendelea kushikilia msimamo wangu mpaka sasa kuwa TUME HAINA MAMLAKA KISHERIA KUFUTILIA MBALI UCHAGUZI.
Baadae ikaja kubainika kuwa uamuzi wa kufuta matokeo haukuwa wa Tume(kwa maana ya maamuzi ya pamoja kati ya mwenyekiti na wajumbe wake wote) bali uamuzi ule ulikuwa wa mwenyekiti peke yake.
Kama tume pamoja na wajumbe wake wote haina mamlaka kisheria ya kufuta matokeo na uchaguzi iweje mjumbe mmoja wa tume anaeitwa mwenyekiti wa tume awe na mamlaka ya kufuta matokeo? HUU NI UBAKAJI WA DEMOKRASIA.
kwa muktadha huo mimi msimamo wangu ni kwamba uchaguzi wa Zanzibar haujafutwa kwa kuwa amri iliyofuta uchaguzi ni amri haramu na mtu aliyefuta matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar hana mamlaka hayo na hakuna popote pale anapopewa mamlaka hayo.
Kwa kuwa mwenyekiti wa Tume yaani ZEC hana mamlaka ya kufuta uchaguzi basi maelekezo aliyotoa ya kurudiwa kwa uchaguzi wote nayo ni maelekezo HARAMU kwa kuwa hayatokani na sheria yoyote zaidi ya kuyaita kuwa ni maamuzi ya kidikteta kwa kuwa hayana msingi wowote wa kisheria.
huu ndio msimamo wangu.
1.tamko la Jecha S. Jecha kufuta uchaguzi ni tamko haramu.
2.Uchaguzi wa Zanzibar haujafutwa na bado unatambuliwa na kutambulika kikatiba na kisheria.
3.Tamko la kurejelewa upya kwa uchaguzi ni tamko haramu na linapaswa kupuuzwa na kulaaniwa kwa nguvu zote.
4.Tume imalizie kwa haraka kuyatangaza matokeo yaliyosalia kwa manufaa ya taifa letu na amani ya nchi yetu.Na baadae iwatangaze washindi halali walia wa baraza la uwakilishi na mshindi halali wa Urais.Matokeo yote yaliyotangazwa katika udiwani,uwakilishi yaheshimiwe.
nimesikia CCM wakiunga mkono tamko hilo haramu. Wamefanya hivyo mara kadhaa kupitia wasemaji mbalimbali kwa nyakati tofauti.
moja ya hoja za chama cha Mapinduzi kukubali uchaguzi urudiwe ni kuwa: uchaguzi wa October 25/10/2015 ulihujumiwa,rejea matamko mbalimbali ya CCM likiwemo la aliyekuwa makamu wa Pili wa Rais Zanzibar katika serikali ya Shein iliyomaliza muda wake.
rejea pia tamko la Jecha na sababu alizotoa.
CCM inajikita kusema uchaguzi ulihujumiwa na hivyo chama hicho kinaunga mkono kurudiwa kwa uchaguzi.
Madai ya CCM nayo hayapo kisheria na hivyo ni madai haramu na yanapaswa kupuuzwa.
Sheria zimeeleza mambo yanayopaswa kufanyika ama kufanywa na ni wakati gani yafanyike lakini hakuna hata dai moja linalotambuliwa na sheria kati ya madai ya CCM wala ya mwenyekiti wa Tume Jecha S. Jecha dhidi ya uamuzi uliochukuliwa ama unaopigiwa upatu na CCM.
Hakuna hata dai moja la CCM ambalo lina msingi wa kisheria zaidi ya viongozi wa CCM kuendelea kushikilia msimamo wao usio wa kisheria wala wa kikatiba kuwa uchaguzi urudiwe.
Hivyo nao wanapaswa kupuuzwa kwa nguvu zote.
uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulikuwa na dosari nyingi za kisheria,ukiukwaji wa sheria na kanuni nyingi,Matokeo kuchakachuliwa lakini pamoja na yote hayo matokeo ya wagombea Urais wa JMT yaliendelea kutangazwa mpaka mshindi akatangazwa bila kuzingatia kasoro zote hizo.
Sasa iweje hujuma za bara hazikuifanya Tume ya NEC nayo kufuta uchaguzi hasa kwa kuwa NEC na ZEC zinafanya kazi kwa kushauriana ama kwa pamoja?
Iweje kura iliyopigwa na mpiga kura X huko Zanzibar ya upande wa Muungano ikawa halali lakini kura ya mtu huyohuyo ikawa haramu upande Zanzibar? (ikumbukwe kuwa Wanzibari walipiga kura tano kuchagua Rais wa Jamhuri,Rais wa SMZ, mbunge wa bunge la Dodoma,Mwakilishi wa baraza la wawakilishi na diwani wa kata)
katika kura zilizopigwa na mtu mmoja,zikasimamiwa na wasimamizi walewale wanaohusika,zikahesabiwa na watu walewale wanaohusika,zikasafirishwa na watu walewale wanaohusika,zikajumlishwa na watu wale wanaohusika,zikabandikwa vituoni na watu walewale wanaohusika.
Eti ikawa hivi!!
[URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=Kura]#Kura [/URL] ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni safi na halali.
[URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=Kura]#Kura [/URL] ya Mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kura safi na halali.
[URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=Kura]#Kura [/URL] ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari siyo safi na ni haramu.
[URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=Kura]#Kura [/URL] ya Mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar siyo safi na ni haramu.
[URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=Kura]#Kura [/URL] ya diwani katika kila kata huko Zanzibar siyo safi na ni haramu.
Iweje CCM haikuja hadharani na kushinikiza uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano nao ufutwe kutokana na kugubikwa na kasoro nyingi?
kwa kuwa tumelalamikia muda mrefu ubovu wa sheria za uchaguzi hapa nchini na mwanya huo umekuwa ukitumika vibaya ikiwemo kukosekana kwa tume huru za uchaguzi. ZEC na NEC si tume huru.
Matokeo ya Rais kutohojiwa mahakamani.
Basi nasema sheria ni msumeno.
Wakati huu imekata upande wa CCM na kwa kuwa sheria haitoi mwanya wa kufutwa kwa uchaguzi wala matokeo na kutangazwa kwa uchaguzi mwingine basi CCM nayo iheshimu sheria hii ili haki ya Wazanzibar isipokonywe.
Binafisi naamini kuwa uchaguzi wa Zanzibar haukuhujumiwa kama inavyodai CCM na matokeo yake ni halali kama yalivyotangazwa na tume katika majimbo na kata mbalimbali kwa kutangazwa washindi.
vilevile naamini kuwa hoja ya kutaka kurudiwa kwa uchaguzi ina kusudio na mpango wa kuhujumu uchaguzi wa Zanzibar katika ngazi ya Urais,Uwakilishi na udiwani.Vilevile naamini kuwa mwanzo hujuma hazikufanyika ila hujuma zinataka kufanywa katika uchaguzi wa marudio kama utafanyika ili kuibeba CCM na kupoka maamuzi halali ya Wazanzibari.
hivyo naunga mkono msimamo wa CUF wa kukataa kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar na kukataa kushiriki kwa uchaguzi huo kwa kuwa hautakuwa kisheria wala kikatiba. Na kwa kufanya hivyo CUF itakuwa inaheshimu na kuilinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997,Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2010 . Vilevile uamuzi huu utakuwa unalinda na kutetea sheria za uchaguzi nchini.
Msimamo wangu kuhusu Maalim Seif kujitangazia matokeo na hivyo kuwa sehemu ya dosari katika uchaguzi ule kama ilivyodaiwa na Tume.
Kwa kuwa Seif alitangaza matokeo basi sheria ichukue mkondo wake.
Lakini kwa vyovyote vile kitendo cha Maalim Seif kutangaza matokeo hakiipi Tume mamlaka ya kufuta Matokeo na uchaguzi. Vilevile kitendo hicho hakimpi Mwenyekiti wa Tume mamlaka ya kufuta matokeo na uchaguzi.
Tume iendelee na Jukumu lake la kisheria na kama kuna haja na uhalali kwa Maalim Seif kuchukuliwa hatua za kisheria basi hilo litekelezwe kwa Seif kufunguliwa mashitaka lakini wakati huo tume iwe imeshatekeleza jukumu lake la kisheria la kutangaza matokeo na kumtangaza mshindi.
alafu tuiache mahakama iamue juu ya kitendo kile cha mgombea kutangaza matokeo lakini wakati huo nchi ina Serikali yake.
ieleweke pia kuwa Maalim Seif alitangaza Matokeo na hakujitangaza mshindi ila aliiarifu tume imtangaze kuwa ndiye mshindi halali kwa kuwa alipata kura nyingi kuliko mgombea yeyote kati ya walioshiriki.Maalim anajua fika kuwa mwenye mamlaka ya kumtangaza mshindi ni Mwenyekiti wa Tume ndio maana alimwambia kuwa akamilishe haraka ujumlishaji na amtangaze kwa kuwa hesabu zilikuwa zinaonyesha hivyo japo tume haikuwa imekamilisha ujumlishaji.
Na: Joseph Mshinga.
signature:09/11/2015.