Msikiti wa Mfalme Mohamed wa Sita

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,912
30,253
MSIKITI WA MFALME MOHAMED WA SITA

Naangalia picha ya msikiti uliojengwa ndani ya viwanja vya Kinondoni Muslim School akili yangu inarudi nyuma hadi miezi ya mwisho ya mwaka wa 1968.

Mwaka wa 1968 miezi mitatu ya mwisho wa mwaka ndani ya darasa moja katika shule hiyo iliyojengwa na East African Muslim Welfare Society (EAMWS) marehemu Tewa Said Tewa alikuwa anaongoza mkutano wa EAMWS yeye akiwa Mwenyekiti katika nafasi yake kama Rais wa jumuia hiyo kwa upande wa Tanganyika agenda iliyokuwa mezani ikiwa nini kifanyike kuepusha EAMWS isivunjike kwa kuwa mikoa mingi ilikuwa imejitoa baada ya kuzuka mgogoro ulioanzia tawi la EAMWS Bukoba.

Kisa hiki ni maarufu sana kwa Waislam.

Baadhi ya wajumbe katika mkutano ule walichangia mjadala katika mkutano ule wakibubujikwa na machozi kwani ilikuwa wazi EAMWS imefikia mwisho wake na inavunjika.

Kilichokuwa kinawaliza ni kuwa ule upande uliokuwa umejitenga ulikuwa umekataa sulhu wao wakishikilia kuwa EAMWS lazima ivunjwe hawana hajanayo.

Wakati ule EAMWS ilikuwa inajenga Chuo Kikuu katika uwanja wake wa Chang'ombe na kuvunjika kwake maana yake ni kuwa mradi ule na miradi mingine ya kujenga shule nchi nzima ndiyo itakuwa mwisho na Waislam watarudi palepale walipokuwa wakati wa ukoloni kwa kukosa elimu waliyotegemea sasa wataipata kwa juhudi zao wenyewe kupitia EAMWS na miradi ya elimu iliyokuwa inatekelezwa kinara wa juhudi hizi akiwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir.

Katika viongozi wa EAMWS waliokuwapo katika mgogoro ule walio hai ni wawili - Bilal Rehani Waikela na Advocate Mussa Kwikima wote kutoka Tabora na huu ndiyo mkoa ambao haukujitoa katika EAMWS.

EAMWS ikavunjika na Chuo Kikuu hakikujengwa na shule zilizokuwa zinajengwa zikasimama.

Leo ndani ya ardhi ile ya EAMWS pale Kinondoni Muslim School umesimama msikiti mkubwa wa fahari na wa kujivunia.

MSIKITI WA MFALME MOHAMED WA SITA.jpg
 
Miaka zaidi ya 50 mmeshindwa kujenga chuo kikuu kwa kisa cha mwaka 1968? Kuna kitu hakipo sawa ndani ya uongozi wa Waislam.

Vp ile ardhi ya Chang'ombe aliyouziwa Manji na Waislam wenzenu mmefanikiwa kuirudisha?
 
Miaka zaidi ya 50 mmeshindwa kujenga chuo kikuu kwa kisa cha mwaka 1968? Kuna kitu hakipo sawa ndani ya uongozi wa Waislam.

Vp ile ardhi ya Chang'ombe aliyouziwa Manji na Waislam wenzenu mmefanikiwa kuirudisha?
Kinyungu,
Katika miaka ya 1970 Waislam walitaka kujenga Chuo Kikuu kwa msaada wa Organisation of Islamic Conference (OIC)serikali ikakataa kutoa kibali chuo kijengwe Tanzania.

OIC wakauhamisha mradi ule wakaupeleka Uganda kikajengwa chuo hicho Mbale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
asalaamalaykum, mzee wangu MOHAMMED SAID. MUNGU akuongezee afya ya mwili na akili,INSHAALHA. ss tuliokuwa wengine hatuzaliwa ama tumezaliwa lkn ama bado tukiwa wadogo, wewe ni HAZINA YETU KUU KUPATA YALIYOPITA WAKATI HUO. ila kubwa ama kwa hakika sina hakika lkn pengine huo msikiti umejengwa kwa msaada labda, ila wazo langu mimi WAISLAMU WA NCHII HII HAWANA SHIDA KWA SASA YA MISIKITI, KAMA ILIVYOKUWA HUKO NYUMA LABDA. NAONA SHIDA KUBWA KWA SASA NI MASHULE NA HOSPITALI. eneo hilo lingetumika kujenga HOSPITALI INGELIKUWA BORA ZAIDI . na kama tumliamuliwa na wanasiasa ili wao na wenziwao wakubwa wenzao watu maarufu kama wanavyojulikana kuwa upatikane msikiti maalum wa kuswalia HAO bado hatujagusa shida ya msingi na pengine watambue kuwa misikiti yoote kwa hadhi iko sawa ukiondoa ule ulikoko MAKAA NA MADINA, bali kimsingi waislamu tunahitaji HOSPITALI TENA YENYE MAADILI YA KIISLAMU ZAIDI.
 
Back
Top Bottom