yasini msangi
Member
- Nov 13, 2013
- 16
- 5
Alikutana na msichana wakatongozana wakapendana , wakawa wanawasiliana siku moja jamaa akataka kujua background ya msichana huyo, kwahiyo huyo msichana alimsimulia jamaa maisha yake kama ifuatavyo.
Yeye ni mtoto aliyezaliwa peke yake kwa baba yake ila mama yake ana watoto wengine kwa baba mwengine ambayo ni wakubwa wengine wameshaolewa. Mama yake yupo hai mpaka sasa na anaishi na huyo mwanaume mwenye hao watoto wakubwa ila baba yake yeye alishafariki na yeye alikuwa anakaa na bibi yake, ila maisha alokuwa anaishi na bibi yake hayakuwa mazuri, yaani yalikuwa ya manyanyaso , kwahiyo yeye akaamua kuondoka hapo kwa bibi yake na kuwaambia anaenda zake kutafuta maisha. Basi akaondoka na kwenda kupanga akapata kazi akawa anafanya kazi na huku anakaa kwake.
Ikafika kipindi kazi ikasimama akawa hana kazi ndo akamwambia jamaa naomba nije tukae wote huko kwako. Kipindi cha nyuma huwa anakuja kwa jamaa na kuondoka, sasa ilivyotokea kazi hana tena ikabidi amwambie jamaa naomba nije tuishi wote kwako. Jamaa akamwambia subiri kwanza nitakujibu nipe muda.
Siku kama mbili zikapita siku jamaa anarudi kazini anamkuta yule msichana amekuja yupo kwake na amefungua mlango na anapanga mabegi yake yaani amekuja full amehamia moja kwa moja. Jamaa akashituka alivyokuta mlango wake upo wazi wakati aliufunga alipoondoka kazini. Kumbe yule msichana alichukua moja ya funguo ya mlango bila kumwambia jamaa na akawa ameondoka nayo. Jamaa kamuuliza umefunguaje mlango na wakati funguo ni nazo mimi , msichana akamjibu kuwa nilichukua funguo moja bila kukwambia ila naomba nisamehe.
Jamaa akawa hana cha kufanya akamuuliza tena na vipi mbona umeleta vitu vyako umeamia moja kwa moja na wakati nilikwambia nitakujibu? Msichana akawa hana cha kusema akawa kimya. Jamaa akamwambia fanya mpango urudi tu kwasababu umejiamulia mwenyewe bila kunishirikisha mimi. Msichana akamwambia mimi kule nimesharudisha chumba na mwenye nyumba kashapata mpangaji mwengine ndo amenirudishia hela yangu ilobaki ambayo Tshs.100,000/=
Jamaa akawa hana jinsi akalala kwake. Siku ya pili jamaa akamwambia kwanini usirudi kwa bibi yako , au kwa mama yako? Msichana akamwambia mimi sina kwa kwenda kwasababu kwanza kwa bibi siwezi kurudi pili kwa mama pia hapaendeki kwasababu mama anaishi na baba mwingine na huyo baba hamtaki kwasababu yeye ni mtoto wa nje. Jamaa akamwambia kwahiyo inakuaje sasa maana mimi siwezi kundelea kuishi na wewe wakati simjui hata ndugu yako mmoja, pili sijakuoa hivi kwa mfano unapata matatizo mimi nitafanyaje?
Msichana akamwambia wewe kama hutaki nikae kwako bora niondoke nikatafute mwanaume yeyote yule niishi nae ila sio mimi kwenda nyumbani sitaki , na huku msichana akiongea hivyo huku akilalamika kumwambia jamaa kuwa anajua hampendi ndo mana anamwambia hivyo aondoke.
Sasa jamaa anaomba ushauri je afanye nini?
Karibuni wadau mumpe ushauri