Msichana auwawa kikatili na mumewe Dar

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
November 16, 2009

MSICHANA Khadija Daudi (22), mkazi wa Mbagala Charambe aliuawa kikatili na mumewe kwa kuchomwa na kisu mgongoni kwa kile kilichodaiwa kuwa ni baada ya kukataa kuamka usiku kwenda kuokota embe.

Tukio hilo la kusikitisha lilitoka mwishoni mwa wiki huko Mbagala jijini Dar es Salaam.

Ilidaiwa kuwa chanzo cha kifo hicho ni mume wa msichana huyo aliyetambulika kwa jina la Shariff Kondo alimuamsha marehemu kumtaka aende nje ya nyumba yao majira ya saa kumi kasoro usiku, aende akaokote embe lakini marehemu aligoma na kudai kwa kuwa ni usiku asingeweza kwenda nje kufanya kazi hiyo.

Inadaiwa kuwa kutokana na majibu hayo mumewe alikasirika na ndipo alipochukua kisu na kumchoma nacho mgongoni.

Baada ya kuchomwa kisu hicho alipiga kelele na majirani walijitokeza kumpa msaada wa kumkimbiza Hospitali ya Temeke huku akiwaambia kilichomtokea kwa mumewe huyo.

Kwa bahati mbaya msichana huyo alipoteza fahamu na kufariki mara baada ya kufikishwa hospitalini hapo.

Wakithibitisha tukio hilo baadhi ya majirani wa marehemu huyo, wamedai kuwa walisikia kelele za kuomba msaada katika chumba cha mpangaji mwenzao na mara baada ya kuingia ndani kwake kujua kilichotokea ndipo walipokuta kitanda chake kimelowa damu na huku akiugulia maumivu.

Majirani hao wamesema kutokana na hali hiyo walikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi na baadhi yao walijaribu kumtafuta mumewe lakini hakupatikana ndipo walipokwenda kumwamsha baba mzazi wa msichana huyo anayeishi Charambe na kumuelezea yaliyompata binti yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Liberatus Sabasi, amesema kuwa, tayari mtuhumiwa aliyehusika na tukio hilo tayari ameshakamatwa yuko katika kituo cha polisi cha Chan’gombe na anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.

 
Du! haya maisha jamani!? yaani mtu anayaweka rehani kwa ajili ya embe dodo tu,hii ni kali au kuna sababu nyingine? Unayelala naye kitanda kimoja unamchoma kisu kisa embe? Mungu amlaze pema peponi
 
Kikwete alisema "Maisha bora kwa kila Mtanzania", ndiyo haya?
Amefanya nini Kikwete hapo? Lawama nyingine hazina msingi? Vituko vya mauaji havitokei wapi katia sayari hii? Hebu tusiwe people with character X.
 
Duh, inasikitisha sana, ni embe za kAWAIDA au marehemu aliamua kustiri ukweli? kwani ni msimu wa embe huko chalambe?....
 
My God huu ni unyama wa ajabu jamni kaondoa uhai wa mtu kisa embe nadhani thamani yake haizidi sh 500!!!
 
Duh, inasikitisha sana, ni embe za kAWAIDA au marehemu aliamua kustiri ukweli? kwani ni msimu wa embe huko chalambe?....

Mkuu bila kujali kama ni embe kweli au la hakuwana na sababu ya kumchoma kisu na kuondoa uhai wa mwenzake.He soon gonna be behind the bars unnecessarly!
 
Kikwete alisema "Maisha bora kwa kila Mtanzania", ndiyo haya?

Uzembe wa individuals hatuwezi kumbebesha rais......mbona kwa Obama watu wanaua mabinti na kuhifadhi maiti vyumbani mwao na hamsemi?? au kwa kuwa mnaogopa kufukuzwa huko???
 
Jamani hii ni hatari,katika hali ya kawaida haielezekei,utamuuaje mkeo unayeishi nae ,tena inaonyesha ndoa ni changa kabisa.Huyu lazima atakuwa na mapepo ya uuaji au kadanganywa na waganga kuua mkewe ili apate mali ,sababu haiwezekani uue mtu kwa embe.
 
Amefanya nini Kikwete hapo? Lawama nyingine hazina msingi? Vituko vya mauaji havitokei wapi katia sayari hii? Hebu tusiwe people with character X.

we banaa wee!!! na wewe acha kupoteza muda wako, utaumia kichwa bureee!!! kuna wengine hawajisikii raha bila kumlaumu Kikwete!!! Si ajabu ukasikia mtu anamlaumu Kikwete kwavile anakula kwa kijiko!!! na wengine ilimradi waandik, hata kama cha kuandika hawana wataandika tu!!! open up ur eyes bro!
 
mungu aiweke roho ya marehemu pema peponi
sina lingine la kuongeza

Nikiona ume-post tu lazima niangalie!!! ajabu nikifungua page, naacha kusoma ulicho-post na kuishia kuangalia macho yako!!! nimesikia ni wewe mwenyewe huyo, na wala sio photo ya mwenzako!!! lol
 
Back
Top Bottom