Msichana amuua boyfriend wake kwa kumchoma kisu baada ya kulazimisha penzi kwa nguvu..!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,355
33,194
mbakwaji.jpg

Jamaa Achomwa Kisu cha Kifuani na Demu Baada ya Kumlazimisha Kufanya Nae Mapenzi Kwa Lazima na Kutaka Kumbaka

Onyinyechi Orakwuelum alikuwa akisheherekea siku yake ya kuzaliwa na alikuwa akitimiza umri wa miaka 18. Hata hivyo siku hiyo ambayo huwa ni ya furaha miongoni mwa binadamu wengi, imegeuka na kuwa ya

majonzi na matatizo baada ya mwanadada huyo kuwa anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua Kijana ajulikanaye kwa jina la Ayobami, ambaye binti huyo anadai alidhamiria kumbaka na katika kujitetea kwake alifanikiwa kumpiga kisu na kujisalimisha mwenyewe

Siku ya tukio Ayobami alimpigia simu binti huyo na binti akamwambia ya kwamba yupo nyumbani na ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, jamaa akamuuliza kama alikuwa na mipango yoyote ya

sherehe, binti akamwambia hapana ni mapumziko na kuikumbuka tu siku hiyo, Ayobami akamwambia wakutani mida ya saa 1 jioni maeno fulani, binti alikubali, na alipoeenda wakaenda mpaka nyumbani kwa

Ayobami ambaye alitumia muda mfupi kukaa katika laptop yake na baadae akamfuata na kumwambia ya

kwamba anampenda na anaomba awe mpenzi wake. Onyinye alikataa sababu alihisi ni utani lakini jamaa

alivyozidi kumsogelea karibu, binti huyo akagundua kuwa Ayobami amelewa, naye akakazania kupewa japo penzi kwa siku husika ikiwa hatamkubalia basi angemfanyia kitu mbaya.

Baada ya kukuru kakara za muda mrefu, jamaa akaelekea jikoni na kuchukua kisu ambacho alikuwa akimtishia msichana huyo huku akianza kumvua nguo kwa nguvu, kwa bahati kisu hicho kilidondoka chini na

ndipo Onyinye alikiokota na kumchoma nacho, akaskia sauti kutoka kwa Ayobami akilalama kwamba kamchoma, Onyinye alikimbia na kwenda kutoa taarifa kituoni, polisi walipofika eneo la tukio walimkuta

jamaa kashafariki na kisu kilimuingia katika moyo.
Mpaka sas binti huyo anashikiliwa na polisi mpaka uchunguzi utakavyo kamilika.



MSICHANA AMUUA BOYFRIEND WAKE KWA KUMCHOMA KISU BAADA YA KULAZIMISHA PENZI KWA NGUVU..! - GUMZO LA JIJI
 
huyu hawezi kufungwa kwa murder
ni defence against rape ataachiwa tu
lau kama jaji ni kilaza atamfunga kwa manslaugher(kuua bila kukusudia)..
itategemea alimchoma kisu mara ngapi katika kujihami na itategemea mazingira pia
 
huyu hawezi kufungwa kwa murder
ni defence against rape ataachiwa tu
lau kama jaji ni kilaza atamfunga kwa manslaugher(kuua bila kukusudia)..
itategemea alimchoma kisu mara ngapi katika kujihami na itategemea mazingira pia

ikiwa kama alimchoma mara 1 inakuwaje hapo?
 
kama alimchoma mara moja tu na mshikaji akawahi kuzimu
hapo hana hatia hata kidogo ni self defence na hakuwa na intetion ya kuua
hana gulity mind hapa.
kama alimchoma zaidi ya mara moja inategemea pia kama ilikuwa bado ni state of defence
au intention to kill itahitaji uthibitisho zaidi.
mahakama itatumia busara iishajiridhisha hali halisi.
ni sawa na umfumanie mwenza kwa ghafla umpige na kitu kikali mara moja akafa,,
na ungempiga mara 2 akafa hapa ni mazingira mawili kisheria.
hilo la kwanza hukua na nia ya kuuwa ila huyu wa pili alotwanga mara 2 huyu ni murder charge.
ikiwa kama alimchoma mara 1 inakuwaje hapo?
 
huyu hawezi kufungwa kwa murder
ni defence against rape ataachiwa tu
lau kama jaji ni kilaza atamfunga kwa manslaugher(kuua bila kukusudia)..
itategemea alimchoma kisu mara ngapi katika kujihami na itategemea mazingira pia

Nadhani unataka kuhukumu kwa kuendeshwa na emotions na sio facts.
Hii kesi ni ngumu kwa kuwa aliyetoa maelezo ya stori nzima ni mtuhumiwa na watu mnaanza kuamini hata bila kuwa na doubt. Ukweli wa kilichotokea anaujua mtuhumiwa. Lazima athibitishe ni self-defence.
Haingii akilini eti msichana anakubali kupelekwa nyumbani kwa mwanaume kuanzia mida ya saa moja usiku halafu asifikirie kwamba hayo ni mazingira hatarishi. Inawezekana pia walikuwa ni wapenzi.
Kwa hiyo, hukumu yeyote haitamfanya jaji kuwa kilaza bali itategemea na ushahidi utakaotolewa.
 
"Msichana amuua boyfriend wake baada ya kulazimisha penzi" huyu msichana alishindwa nini ku chill down nakumpa ngono zembe boyfriend wake kwakuwa wamesha amua kuunganisha sehemu zao za siri bila ndoa? na paka anaitwa ndani sehemu waliyozoea kulia hilotunda hakujua kuwa anaenda kupewa mambo? huyo binti angekataa na hata kumpigia kelele huyo mpenzi wake na siyo kumuua, shame on you bitch!
 
Haya mambo yataisha lini? Ni pale ambapo watu watamrejea Muumba wao kwa KISHINDO.
 
Back
Top Bottom