Msiba si kusikitika/kulia tu bali TAFAKURI

blessings

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
6,983
6,238
Pamoja na ukweli kuwa msiba si jambo la kushangilia lakini wengi wetu (Watanzania) basi ukipata msiba mtu unajelegezaaa as if ndo hakuna maisha baada ya hapo.
1. Tunajikusanya maelfu kwenye eneo la msiba, makaburini na kurud nyumbani kuendelea kuongezea machungu familia ya mfiwa (ikiwemo gharama za kuwalisha na kuwanywesha waombolezaji).
** Nichukue fursa hii kupongeza KKKT Dayosisi ya Kaskazini chini ya Baba Askofu Dr. F. S. (PhD) kukataza waombolezaji kula misibani.
2. Hatujali mtu akiwa mgonjwa (kwa michango na sala) bali tunasubiri mtu afe tukapige selfie na kuuza madera na t-shirt. Wafiwa jipeni moyo punguzeni machungu kwa KuMUENZi marehemu kwa kufanya kazi kwa bidii na msisahau kutembea kifua mbele kuliko kulia tuuuu
 
Nini maana ya mantiki ya thread yako??
Unataka ubaki mwenyewe wewe pamoja na marehemu wako???

Sidhani kama tunaifilisi familia yako zaidi sisi ndo tunafilisika kwa kukuchangia wewe na marehemu wako Sanda, usafiri, jeneza, mochwari, madawa na manukato, Chakula, malazi ya wafiwa ikiwezekana na usafiri wa kuwarudisha wana ndugu walipotoka...

Isitoshe unaonekana huna mchango wowote kwenye misiba ni roho mbaya tu na ubahili..

Wacha tukusanyike tuwazike wapendwa wetu kwa amani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom