Msiba:Mama Eugine Mwaiposa hatunaye!

Msiba:Mama Eugine Mwaiposa hatunaye!

Columbus

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
2,002
Reaction score
652
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Dar; Mama Eugene Mwaiposa, amefariki Dunia leo majira ya saa 4 asbuhi Mjini Dodoma. Chanzo hakijafahamika. Soma http://goo.gl/UoUk
 
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Dar; Mama Eugene Mwaiposa, amefariki Dunia leo majira ya saa 4 asbuhi Mjini Dodoma. Chanzo hakijafahamika. Soma http://goo.gl/UoUk


...Eugene Mwaiposa enzi za uhai wake.
MBUNGE wa Jimbo la Ukonga, Eugene Mwaiposa (CCM) amefariki dunia akiwa nyumbani kwake mkoani Dodoma leo baada ya kusumbuliwa na shinikizo la damu kwa muda mrefu.
Taarifa imetolewa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kwamba alikuwa na tatizo la shinikizo la damu kwa muda mrefu na amefariki akiwa nyumbani kwake Dodoma.
Ameongeza kuwa nyumbani kwa marehemu ni eneo la Chaduru jirani na jengo jipya la Hoteli ya Shabiby barabara ya Dar es Salaam.
Mwili wa marehemu umepelekwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi zaidi.
Shughuli ya kuaga mwili itafanyika kesho. Naibu Spika ametumia kanuni ya 152 kuahirisha bunge hadi keshokutwa Alhamisi kutokana na msiba huo.
 
Poleni watanzania wote, hasa jimbo la Ukonga. MUNGU akipenda mtapata mwakilishi mwingine si muda mrefu. Poleni pia familia yake. Shinikizo la damu ni ugonjwa mbaya sana. Na kwenye vipindi kama hivi vya uchaguzi huwa unapamba moto
 
Back
Top Bottom