Mshtuko; Hadaa kwenye dini!

Kazwala mkuu

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
1,034
2,247
Salaam

Dini wengi wetu ndiyo inayotuunganisha na Mungu na kufanya yale yaliyoagizwa kupitia vitabu tunavyoviamini kulingana na dini zetu.

Kwa hapa Tanzania dini zile maarufu zililetwa na waarabu na wazungu na hawa watu hawakuja moja kwa moja kwa lengo la kujitoa Kimungu bali wapo waliokuja kututawala na waliokuja kufanya biashara na ndipo hapo wakapata kueneza kile wanachoamini wao, pamoja na kuwa walileta habari njema za kidini lakini bado walitesa wazee wetu, kuwapeleka utumwani, kuwauza na hata kuwauwa.

Yote si mali kitu na tumepokea Dini na kumjua Mungu kupitia wao hivyo tukapata kujua ya kesho yetu ikiwepo mema na mabaya, yote yale yamekwisha lakini Neno bado linaishi.

Miaka imekwenda na tumeijua Kweli katika dini zetu na siku hizi hatufanyi jambo mpaka kuwajumuisha viongozi wetu wa kidini ili kuleta baraka na kufanya tusiende nje ya mstari.

NYUMA YA PAZIA

Asilimia kubwa ya viongozi hawa wamekengeuka na wanatenda maovu huku wamejiziba na shuka ya dini.....mara kadhaa tumeona wakiwapa wake/binti zetu mimba, kuwalawiti watoto, kutembea na wake za watu, kuwatapeli watu mali zao kwa kivuli cha sadaka.

UKWELI MCHUNGU

Kwa kuwa imeshaonekana dini siku hizi zinalipa hivyo genge kubwa limevamia na kuanzisha ibada zao na mwisho wa siku kujilimbikizia mali na kupata utajiri mkubwa huku baadhi waumini wakiwa hawajimudu hata milo miwili kwa siku......tujiulize iwapo waliotumwa awali na Mungu walijijazia mali kama hawa wa leo.

USICHOJUA

Wengi husaka madawa ya kienyeji ili waonekane wana Muujiza na wengine huroga ili watawale na kuwa viongozi wa nyumba za ibada wapate kukusanya swadaka.

Wapo wakweli ila wamezibwa na tabaka la waovu na kuondoa maana rasmi ya ibada ya Mungu na imefika hatua kama wanaabudiwa wao.

Upotoshaji wa mapokeo haukuanza leo na watu namna hiyo ndiyo ndiyo waliosababisha kitabu kikawa cha dini moja ila madhehebu yakawa tofauti huku kila kundi likiamini Mungu yupo upande wao.

Hakika Mungu yupo na alishatabiri juu ya nyakati za mwisho na manabii wa uongo, hivyo sisemi tusiabudu bali tuabudu huku vichwa vikifanya kazi ili kuijua kweli.

Naam tuzidi kumuomba Mungu atufungulie kweli ili ibada zetu zisiingie mushkeli kwa sababu ya upotofu wa wengine, na atuhesabie mema yetu na wao awahisabie yao.
 
Back
Top Bottom