Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,443
Nimeshitushwa na taarifa za polisi walipokuwa wanampongeza mwanamke aliyewagonga majambazi kwa gari yake pale walipompora kiasi cha shilingi 420,000.
Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam amenukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema "tunampongeza sana mwanamke huyu jasiri kwa kitendo chake cha kishujaa alichofanya na tunaomba watu, hususa wanawake, waige mfano wake, inapotokea nafasi kama hiyo waitumie".
Siamini kama kamanda Silo, ambaye amepitia mafunzo ya kijeshi, anaweza kutoa tamko kama hilo kwa raia. Ukweli ni kwamba Polisi walitakiwa kuwaonya wananchi kwamba wasiwe wanajaribu kutafuta ushujaa kwa kupambana na majambazi wenye silaha kwa sababu ni kuhatarisha sana maisha yao. Kiingereza tunasema ni "reckless and suicidal".
Polisi hawapaswi, na ni kosa kubwa sana, kujaribu kuwatia moyo raia, na hasa wanawake, wasio na mafunzo yeyote ya kijeshi, kukabiliana na majambazi wenye silaha. Raia anapovcamiwa na majambazi anapaswa kwa kila namna kuepuka kukabiliana nao (confrontation) hata ikibidi akabidhi kila kitu anachodaiwa na majambazi. Kazi ya kukabiliana na majambazi wenye silaha ni ya polisi sio raia wasio na mafunzo ya kijeshi!!!
Wito wangu kwa Polisi ni kwamba watoe tamko kukanusha tamko la Kamanda Silo kabla hatujaona madhara kwa raia ambao kwa kuitikia wito wa Kamanda Silo wanaweza kupoteza maisha yao bila sababu. Wao ni raia wasio na mafunzo ya mbinu za kukabiliana na majambazi ambao wengine wana mafunzo ya kijeshi!
Lazima tutamke wazi kwamba Kamanda Silo amefanya kosa kubwa kumpongeza mwanamke wa tukio hili hadharani na kuwataka wanawake wengine "kuiga mfano wa wake, nafasi kama hiyo ikitokea".
Raia yeyote atakayeuwawa akijaribu kupambana na askari wenye silaha, itamaanisha kwamba Polisi, na hasa Kamanda Silo, mtakuwa mnahusika kwa namna moja au nyingine.