Mshindi Nanenane ahenyea zawadi yake mwaka mzima

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,506
Hatua hiyo imemfanya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba, kuagiza alipwe fedha hizo haraka.

Mshandoo ambaye ni mshindi wa kwanza katika mashindano hayo, alifikisha malalamiko hayo jana mbele ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba, wakati wa mashindano ya mifugo katika viwanja vya Nanenane, Nzuguni nje kidogo ya Dodoma.

Kutokana na malalamiko hayo, Dk. Tizeba aliagiza Wizara kuhakikisha analipwa fedha hizo mara moja kwa kuwa ni haki yake.
Alisema hakuna sababu ya mtu kutolipwa fedha zake kama alishinda kihalali, hivyo kinachotakiwa ni utaratibu kufanyika ili alipwe.

akitoa malalamiko hayo, Parutu alisema ametumia Sh. 300,000 kufuatilia zawadi yake hiyo bila mafanikio. Alisema alikwenda kwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembi, mara tatu bila mafanikio.

Alisema alipokwenda mara ya mwisho aliambiwa kuwa kuna mfugaji mwingine alishapewa zawadi wilayani kwake.

Mshandoo alisema kuzungushwa kupata zawadi hiyo kumemfanya akate tamaa ya kushiriki katika maonyesho ya mwaka huu ingawa ana ng’ombe ambao wana ubora wa hali ya juu kulinganisha na wale wa mwaka jana.

Hata hivyo, alisema juzi alipata wazo la kufika katika viwanja vya Nanenane kuonana na waziri ili kuwasilisha malalamiko yake.

"Kwa maneno ya waziri kesho nitajaribu kufuatilia tena zawadi yangu, nadhani sasa nitapata," alisema Mshandoo na kuongeza kuwa akipata zawadi hiyo, mwakani atashiriki tena.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Ndejembi, alisema mfugaji huyo alikuja mwaka jana katika maonyesho kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa na kushinda mashindano hayo.

"Mfugaji huyu ameshakuja zaidi ya mara mbili kudai fedha zake au mtamba wa ng'ombe kama zawadi zilivyoainishwa katika mashindano hayo. Kushindwa kupata kwa zawadi hiyo kumemfanya kukata tamaa ya kushiriki mashindano hayo mwaka huu,” alisema.

Chanzo: Nipashe
 
Inasikitisha sana...
Mambo ya serikali yana mlolongo sana... Na ikatokea no one cares basi ndiyo kimoja... No one will listen to you...

Inakatisha tamaa sana...


Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom